HANDBAGS ARRANGEMENT

Habari wadau! Leo tujfunze namna ya kupangilia handbags zetu huko majumbani, ili kuwe na muonekana mzuri. Kuna mipangilio mingi ambayo hata ...

Habari wadau!
Leo tujfunze namna ya kupangilia handbags zetu huko majumbani, ili kuwe na muonekana mzuri. Kuna mipangilio mingi ambayo hata wewe mdau unaifahamu na kuitumia, na pengine katika haya ninayoandika unaitumia si vibaya kurudia kujifunza na wengine wasiofahamu wajue. Mara nyingi njia hizi hutumika pia  kupangilia viatu, karibu.
  1. Cubicle storage


Mpangilio huu ni mzuri kwa sababu inakusaidia kupangilia pochi zako vizuri na kuwa na muonekano mzuri. Unaweza kupangilia pochi zako kwa rangi, ukubwa au style na inashauriwa ziwe sehemu ya juu (above eye level) ili iwe rahisi kuona kwa haraka unapohitaji kutumia moja wapo. 

2.  Closet Door Storage
Hii ni njia ni nzuri kama nafasi kwenye shelves/racks imejaa, hii style naiita "nyuma ya mlango style" na imekuwa ikumika sana na watu wengi kutokana na ufinyu wa nafasi kwenye nyumba zetu hasa kwa sie tunaopanga. Unaweza kutumia hooks maalum zitakazo endana na ukubwa wa pochi yako. Njia hii ni nzuri kwani inakupa urahisi wa kuona pochi zako zote kwa wakati mmoja na kuchagua ipo unayoihitaji kwa muda huo, pia inaondoa gharama za kutumia shelf.


 3. Hang with shower Rods
Njia nyepesi na rahisi ya kupangilia ni hii, wote tunazijua shower curtain rings na zinapatikana kwa urahisi. Shower rings  zina clamps ambazo zinauwezo wa kushikilia handbags zako vizuri. kuning'iniza handbags inasaidia kuzipa nafasi shelves na pia unaziona pochi zako kwa urahisi.


Njia zingine tutaendelea nazo next time, kwa leo tuishie hapo. Enjoy!


Related

TUJUZANE 1205228546888570269

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item