SHEKHE ANG'AKA; ASEMA CHADEMA SI CHAMA CHA WAKRISTO

SHEKHE wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shabani Kitilla, amewang’akia watawala na Viongozi wanaopotosha ukweli, akipinga kuwa Chama cha Demokra...

SHEKHE wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shabani Kitilla, amewang’akia watawala na Viongozi wanaopotosha ukweli, akipinga kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) si Chama cha Kikristo, Kikabila au Kiukanda.
Kitilla alisema hayo jana slipohojiana na Gazeti hili, alipotakiwa kutoa msimamo wake kuhusu vurugu zinazodaiwa za kidini zinaoendelea kutokea nchini, yakiwemo matamko ya wanasiasa wanaoshindana kisera, na Mwingine akishindwa anadai Chama cha mwenzake ni cha Kidini, Kikabila na Kiukanda.
 
Akijibu Maswali, Kitilla alisema, Kama Viongozi wa Dini wanavyowafahamu waumini wanaozingatia Ibada za Dini zao, Ndivyo tunavyovifahamu Vyama na Wanasiasa walivyo, maana Wahusika hao ni waumini wetu; Lakini Chadema si Chama cha Wakristo na kinavyotajwa,  mbona wamo na Wa-Islamu?.
“Kama Chadema ni cha Kikristo, Kikabila na Kikanda, Basi Msajili wa Vyama kabla ya kushitakiwa kuachia Ngazi maana alikiuka Sheria za kusajili Vyama na amekiacha kikue katia Uongo huu hadi kinakuwa na Wabunge 48” alisema Kitilla akisisitiza, Waislamu na makabila mengine waliomo ni nani?.
 
Aliongeza kusema, Uongo huo ndio uliopandwa kwa Chama cha Wananchi (CUF) ukaota, ukamwagiliwa mpaka mavuno yakavunwa kwa sababu kilikuwa kinaimalika.leo tena Uongo uleule ndio unaotaka kutumika kuwapumbaza watanzania. Ninachoamini, mtu hadanganywi mara Mbili.; Viongozi waache!
 
Kuhusu Udini alisema, “Tunapougua na kuhitaji damu tunauliza ni ya Dini ya Kikristo au Mu- Islamu? Je Hewa tunayovuta tunauliza kama ni ya Mkristo au Mu-Islamu? Nawashauri Wakristo na Wa-Islamu wasidanganywe, Amani yetu ikatoweka kwa sababu ya watu wachache wenye Uroho wa Madaraka.
 
Aidha Kitilla aliyetaja namba zake  0754-512347 alidai, anawamatafuta Viongozi wakuu wa Chadema wasio Wakristo Mbunge Said Arfi, Zitto Kabwe (MP), Prof. Abdalah Safari, Halima Mdee (MP), Hamad Yusuph, Issa Mohamed na wengine ili awaulize M4C kuna udini? Wakisema hakuna atajiunga huko!
 
SOURCE: Chadema Social Media

Related

OTHER NEWS 6012936792317384061

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item