WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2013, KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 NA JKT MWAKA 2013 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI BAADA YA USAILI KUKAMILIKA

HAYA NDIO MAELEZO MUHIMU: 1. Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2013, kidato cha nne mwaka 2012 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo,...


HAYA NDIO MAELEZO MUHIMU:

1. Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2013, kidato cha nne mwaka 2012 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.

2.Wahitimu hawa waliochaguliwa baada ya usaili wanatakiwa kuripoti tarehe 08/11/2013 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa kuwapeleka Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi tarehe 09/11/2013.
3.Zoezi la usajili litaanza chuoni hapo tarehe 10/11/2013 hadi tarehe 15/11/2013.

4.Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi.

5.Vijana hawa watalazimika kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
a)Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). 
Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

b)Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
c)Chandarua chenye upana futi tatu
d)Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
e)Pasi ya Mkaa
f)Ndoo moja
g)Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingihamsini na mia nne tu (50,400/=).
h)Pesa kidogo ya kujikimu.

6.Kwa mujibu wa kanuni za chuo ni marufuku kufika chuoni na simu ya mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa chuoni hapo. Chuo kitaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.

Kuona majina ya waliochaguliwa bofya hapa chini:
 WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 NA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI

NA

Related

ELIMU 8500015309435071864

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item