KIDATO CHA KWANZA 2014 KUDAHILIWA KIELEKTRONIKI

Profesa Eustella Bhalalusesa WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuanzia mwaka huu imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki kwa wa...


Profesa Eustella Bhalalusesa

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kuanzia mwaka huu imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza.

Imeelezwa kuwa utaratibu huo mpya wa udahili unaoshirikisha Taasisi za sekta binafsi zinazoendesha shule za sekondari, umelenga kuondoa nafasi za wazi au kujirudia.

Kamishna wa Elimu wa Wizara hiyo, Profesa Eustella Bhalalusesa, alisema hayo juzi mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Kassim Majaliwa, kabla hajakaribishwa kufunga kikao cha kazi cha Maofisa Elimu wa Mikoa na wa Halmashauri za Wilaya nchini, mjini Morogoro.

Hivyo alisema kuchelewa kuwapanga wanafunzi wa kidato cha kwanza shule mbalimbali za Serikali ni kutokana na kufanyika kwa kikao cha pamoja kati ya wawakilishi wa shule binafsi za sekondari na Serikali kwa ajili ya kufanyika kwa udahili huo wa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Kamishina wa Elimu nchini alisema kuanzia sasa mfumo huo utakuwa endelevu na umelenga kuondokana na mazoea ya chaguo la pili la wanafunzi ambao wanakosa nafasi licha ya kufaulu vizuri.

Alisema miaka ya nyuma kulikuwa kukijitokeza nafasi kuwa wazi baada ya wanafunzi kuchaguliwa zaidi ya mara moja kuingia kidato cha kwanza katika shule binafsi za sekondari na pia kuwa wamechaguliwa shule za Serikali.

“Kuanza kutumia mfumo wa udahili wa pamoja kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kumesababisha kutokea uchelewashaji wa kuwapanga wanafunzi, licha ya matokeo kuwa yameshatangazwa,” alisema.

“Tunatarajia kazi hii inamalizika siku si nyingi, kabla ya kumalizika Desemba mwaka huu,” alisema Kamishina huyo.

Hata hivyo alisema mfumo huo pia utatoa unafuu kwa wazazi na walezi kulipita ada za watoto wao zaidi ya shule moja ya sekondari hasa za binafsi, kutokana na mfumo huo kuingiza jina moja la mwanafunzi na katika shule moja pekee na si zaidi ya hapo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, Majaliwa aliwataka Maofisa Elimu wa Mikoa nchini kuharakisha upangaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kabla ya kwa mwezi Januari 2014.

Alisema wazazi, walezi pamoja na wanafunzi wenyewe wanahitaji wajue iwapo wamefaulu wamepangiwa shule zipi ili kuanza kidato cha kwanza na pia walezi

Related

ELIMU 6541110158638695225

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item