RAIS KIKWETE AWAPANDISHA VYEO MAOFISA WA JESHI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Jakaya Kikwete, amewapandisha cheo maafisa wakuu kutoka Kanali kuwa B...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Jakaya Kikwete, amewapandisha cheo maafisa wakuu kutoka Kanali kuwa Brigedia Jenerali.

Taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi, ilieleza jana kuwa Rais amezingatia Kanuni za Majeshi ya Ulinzi, Aya ya 7.01 Kifungu cha 13 Juzuu ya Kwanza (Utawala).

Maafisa Wakuu hao ni Kanali Denis Raphael Janga, Kanali Jason Nestor Musikula, Kanali Jackson King Mrema, Kanali Martin Amos Kemwaga, Kanali Joseph Cosmas Chengelela, Kanali Martin Nikubuka Mwankanye, Kanali Harold Kidundi Mziray, Kanali Emmanuel Peter Kapesa na Kanali Mwita Wambura Isamulyo.

Wengine ni Kanali Francis Asilia Njau, Kanali Pendo Uledi Kamungwele, Kanali Moses Adolph Shinyambala, Kanali Ibrahim Abdarahamani Kimario, Kanali Michael Garo Luwongo, Kanali Nelson Hosea Msanja, Kanali Blasius Kalima Masanja, Kanali Aloyce Damian Mwanjile, Kanali Rajabu Goma Hanti, Kanali Ignas Beatus Mubofu na Kanali Dominic Basil Mrope. 

Pia wamo Kanali Hamis Issa Majumba, Kanali Salehe Omari Semtaua, Kanali Henry Sweko Kamundo, Kanali Sylivester Msafiri Minja, Kanali John Bangantagoka Bishoge, Kanali Anselm Shigongo Bahati, Kanali Robinson Mboli Mwanjela na Kanali Kaisy Philip Njelekela. 

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samueli Ndomba kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, aliwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuleta tija na maendeleo katika JWTZ na Taifa kwa ujumla.

Aidha, Luteni Jenerali Ndomba alisisitiza kusimamia nidhamu na ueledi.

Related

OTHER NEWS 4753592731746959310

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item