MAISHA PLUS REKEBISHA: WASHIRIKI KUTOKA RWANDA, BURUNDI, KENYA NA UGANDA WAKO MORO
Dar es alaam. WASHIRIKI wa shindano la Maisha Plus ambayo kwa mwaka 2014 inatambulika kwa jina la Maisha Plus Rekebisha, kutoka nchi...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/03/maisha-plus-rekebisha-washiriki-kutoka.html
Dar es alaam.
WASHIRIKI
wa shindano la Maisha Plus ambayo kwa mwaka 2014 inatambulika kwa jina
la Maisha Plus Rekebisha, kutoka nchini Kenya, Rwanda,Uganda na Burundi
tayari wameshawasili nchini na jana wameelekea wako mkoani Morogoro
kushiriki shughuli za kijamii.
Mratibu
wa onyesho hilo, Ally Masoud Kipanya amesema hili ni kundi la tatu
kushiriki shughuli za kijamii, ambapo kundi la kwanza lilikuwa Iringa,
kisha la pili likaenda Zanzibar na hili la tatu linaenda Morogoro
kushiriki shughuli za kijamii, huku lengo kubwa likiwa ni kubadilisha
maisha ya wanajamii wa huko.
"Hii
ndio sababu Maisha Plus ya mwaka huu inaitwa Maisha Plus Rekebisha,
ambapo lengo kuu ni kuangalia matatizo ya eneo husika na kuangalia jinsi
ya kutatua, na sio kulalamika, tunataka kurekebisha wananchi wenye
fikra za kusubiri kufanyiwa, kuwa wepesi wa maamuzi na kutatua matatizo
waliyonayo", alisema Masoud
“Wananchi
wengi hulalamikia serikali juu ya maswala mbalimbali ambayo hata wao
wenyewe wanaweza kuyarekebisha bila kusubiri kufanyiwa”,alisema.
Washiriki
kutoka nchi jirani ni walio mkoani Morogoro kwa sasa ni Loveness
Asantely ,Mary Sidi(kutoka Kenya), Borandanginye Aurore, Mvano Ciza, na
Abdou Karim(kutoka Burundi), Aminata Siira(kutoka Uganda), Uwamahoro
Fatima, Ngabozinza Khalid, na Ngabozinza Daniel (kutoka Rwanda)
Kupitia
Maisha Plus Rekebisha mwaka huu, wananchi watapata elimu juu ya
kuepukana na mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo magonjwa kama
malaria, kipindupindu, homa ya manjano na mengineyo.
Washiriki
wote kwa ujumla kutoka nchi za jirani wanatakiwa kuwa 12
nambili,waliofika nchini ni 10 wawili wanaotambulika kwa majina Said
Rashid (Uganda) na Caron Abisai (Kenya) bado hawajafika.