MWANAMKE ALIYEHUKUMIWA KIFO NCHINI SUDAN KWA KUASI DINI AACHIWA HURU
Meriam alihukumiwa akiwa mjamzito na kujifungulia gerezani Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini ameachiliwa hu...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/mwanamke-aliyehukumiwa-kifo-nchini.html
Meriam alihukumiwa akiwa mjamzito na kujifungulia gerezani
Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini ameachiliwa huru.
Wakili wake Elshareef Ali, ameambia BBC kuwa
mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kuolewa na mwanamume mkristo
aliachiliwa huru Jumatatu
Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya
Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika
la habari la Sudan Suna.
Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na
alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada
ya kukata kukana kuwa yeye ni mkristo.
Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.
Mumewe Meriam akiwa na wanawe wawili
'Hamu kumuona mkewe'
Mumewe Meriam Daniel Wani, alisema kuwa ana hamu sana kumuona mkewe kwani taarifa hiyo ilitolewa bila yeye mwenyewe kuitarajia.
Ameambia BBC kuwa anataka familia yake kuondoka nchini Sudan haraka iwezekanavyo.
Wanandoa hao waliona kanisanmi baada ya kukutana mwaka 2011.
Hukumu ya kifo dhidi ya Meriam Yahia Ibrahim
Ishag, ambaye alijifungulia gerezani, ilisababisha gadhabu sana hadi
katika ulingo wa kimataifa.
"Tuna furaha sana kuhusu hatua hii ya serikalli na tunaelekea sasa kumchukua,'' alisema wakili wa Bi Meriam Elshareef Ali.
Bwana Ali alisema kuwa Bi Meriam alionyesha ujasiri mkubwa sana wakati huu wa masaibu yaliyomkumba.
''Ni ushindi kwa uhuru wa dini na imani,
tunaamini kuwa katika siku za usoni hakuna mtu atakayelazimika kupitia
masaibu kama yaliyomkumba Meriam,'' alisema wakili wake.
Babake Meriam alikuwa muisilamu ingawa mamake alikuwa mkristo na Meriam akaamua kuolewa na mwanamume mkristo.
Amekuwa gerezani tangu mwezi Februari pamoja na mwanawe mdogo.
Hata hivyo bwana Ali alisema kuwa hajaona hukumu
ya mahakama ya rufaa na kwamba alipokea taarifa hizo kupitia kwa vyombo
vya habari.