WATUHUMIWA WAWILI WA UJAMBAZI BENKI YA NMB WAUAWA

Watuhumiwa wawili wa ujambazi wameuawa jijini Dar es Dalaam na wananchi katika jaribio la kufanya tukio la uporaji katika eneo la ben...

Watuhumiwa wawili wa ujambazi wameuawa jijini Dar es Dalaam na wananchi katika jaribio la kufanya tukio la uporaji katika eneo la benki ya NMB Wilaya ya Ilala.Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakijaribu kumpora mteja aliyekuwa ndani ya benki hiyo akichukua fedha kwa kutumia silaha mara baada ya kutoka ndani ya benki hiyo.Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao ambao idadi yao haijafahamika walifika katika eneo la benki hiyo tawi la Uwanja wa Ndege wakiwa na pikipiki tayari kufanya tukio hilo.
“Hawa walikamatwa kufuatia taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna watu wenye pikipiki ambao wanahisi wanataka kufanya uhalifu. Polisi waliweka mtego nje ya benki lakini waliwashtukia polisi na kuanza kukimbia kila mmoja kwa njia yake,” alisema.
Alisema wakati wahalifu hao wakikimbia, mmoja alifyatua risasi kwa lengo la kupambana na askari, lakini askari hao walifyatua risasi juu kwa lengo la kumuamuru asimame.
“Walifanikiwa kumkamata na alipopekuliwa alikutwa na bastola aina ya Browing yenye namba 230787 iliyotengenezwa nchini Chekoslovakia ikiwa na risasi tatu. Hata hivyo wananchi waliokuwa wengi waliwazidi nguvu polisi wakamshambulia.

“Walimshambulia kwa mawe lakini polisi walifanikiwa kumuokoa na kumkimbiza hospitali lakini alifariki akiwa njiani,” alisema Kova.
Alisema jambazi mwingine ambaye alikimbilia katika eneo la Karakata, wananchi na askari walimkimbiza, lakini hakusimama hata askari walipopiga risasi juu kumtaka asimame.

Alisema baada ya polisi kuona mtuhumiwa huyo anakaidi agizo la kusimama, walimpiga riasasi miguuni na alianguka na kuishiwa nguvu kabla ya kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitali.

Kova alisema baadaye jioni jana, watuhumiwa wengine watatu walikamatwa. Aliwataja kuwa ni Salum Seleman (28), Samwel Clips (32) na Said Salehe ambaye ni mganga wa kienyeji.

Alisema Seleman na Clips walikamatwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari baada ya kugundulika kuwa ni watuhumiwa wa ujambazi katika tukio hilo, ambalo wenzao waliuawa.

“Hawa walifika kituoni pale wakiwa wamebadili nguo na kujifanya ni wateja wa kawaida, lakini lengo lao ni kuangalia hatma ya wenzao, lakini waligundulika kuwa nao walishiriki na baada ya kuwakamata na kuwahoji wamekiri kuhusika na wao ndiyo walikimbia,” alisema

Related

OTHER NEWS 5654037915303110195

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item