WALIOITWA KAZINI SERIKALINI MWEZI AUGUST 2014

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 1...

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 18 hadi 21 Juni, 2014 waliofaulu usaili husika mchakato wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilishwa. Orodha ya majina yao ni kama yanavyoonekana katika Tangazo hili. Orodha hii inajumuisha pia baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda ambao umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira. Barua za kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao.

Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.

KUONA MAJINA YA WALIOITWA BOFYA HAPA

Related

KAZI 1242651437729385736

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item