MBOWE AWA MBOGO

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameonya kuwa iwapo kiongozi yeyote wa chama hicho ataruhusu mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa ngazi yoyote ya uongozi katika uchaguzi, kupita bila kupingwa katika eneo lake, atawajibika.

Alitoa onyo hilo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Bavicha, jijini Dar es Salaam jana.

“Misiruhusu uongozi, kuanzia serikali ya mtaa kupita bila kupingwa. Ikitokea hivyo, na wewe kiongozi (wa Chadema) jiandae kuwajibika,” alisema Mbowe.

Aliutaka uongozi mpya wa Bavicha utakaochaguliwa kuendeleza kazi nzuri iliyoachwa na uongozi wa baraza hilo uliopita.

Kazi hizo ni pamoja na namna ya kuwaandaa vijana, wazee na wanawake, kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura na kushiriki chaguzi zote, kuanzia ule wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, udiwani, ubunge na urais mwakani.

Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) alisema muda mwafaka ukifika, watakutana na viongozi wenzake wa vyama vinavyounda umoja huo vya CUF na NCCR-Mageuzi kuangalia namna watakavyofanya kazi pamoja katika chaguzi zijazo.

Alisema kifungu cha 6 (3) na (4) cha katiba ya Chadema kinaelezea ukomo wa uongozi, hivyo akasema wana kazi kubwa ya kupanua wigo wa chama.
Kwa kuzingatia hilo, alisema watakuwa na kazi ya kutathmini utendaji wa kila kiongozi katika chama kila baada ya miezi sita kuona namna alivyochangia kukuza na kukiimarisha chama.

“Kiongozi atakayeruhusu katika eneo lake chama kisikue, atawajibika kabla ya miaka mitano,” alisema Mbowe.

Alisema Chadema siyo ya fujo, bali ni chama chenye dhamira ya kweli, hivyo akaonya kuwa iwapo mwanachama wake yeyote anayegombea uongozi kwa kutumia mbinu chafu, ikiwamo rushwa, atang’olewa hata kama atakuwa amekwishakupitishwa katika uchaguzi.

Awali, akimkaribisha Mbowe kufungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Bavicha anayemaliza muda wake, John Heche, alisema Chadema imekua na kwamba, kigezo cha hilo ni namna ilivyofanikiwa kufanya kwa mara ya kwanza uchaguzi, kuanzia ngazi za msingi.

Aliushukuru uongozi wa Chadema kwa kuwashughulikia wasaliti ndani ya chama na kusema kamwe vijana hawatavumilia kuona mtu yeyote anakivuruga chama hicho.

Mapema, Katibu Mkuu wa Bavicha anayemaliza muda wake, Deogratius Munishi, alisema wajumbe waliotakiwa kuhudhuria ni 336 na kwamba, hadi kufikia saa 5.40 asubuhi, waliosajiliwa walikuwa 301 sawa na asilimia 89 ya akidi ya wajumbe wote wa mkutano huo.
Source: chademablog.blogspot.com

Related

MKASA WA MOTO GEREZANI RWANDA: WATU 3 WAUAWA

Watu watatu wamefariki na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa wakati gereza moja liliteketea moto magharibi mwa Rwanda, karibu na mpaka wa DRC. Tukio hili linatokea mwezi mmo...

MAOFISA 13 UWANJA WA NDEGE WAFUKUZWA KAZI

Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi akitoa ufafanuzi wa kufukuzwa kwa wafanyakazi 13 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwl. Nyerere. Zaidi ya Maofisa kutoka wizara tatu wapato 13 walioku...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904758
item