MBUNGE WA CCM JIMBO LA MOROGORO KUSINI ATEKELEZA ILANI YA CCM

  Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris  Akitoa hotuba yake Namna atakavyoshirikiana na Wanachama na Viongoizi wa Jim...

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris  Akitoa hotuba yake Namna atakavyoshirikiana na Wanachama na Viongoizi wa Jimbo la Morogoro Kusini bega kwa bega ili chama hicho kiweze kujitegemea kiuchumi kwajili ya kutekeleza Majukumu yake ya Kila siku Ikiwemo Kushinda kwa kishindo Uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2O15.

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris (kulia) Ahimkabidhi Pikipiki 11 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar Ikiwa Ni ahadi yake aliyoitoa ya Kukusaidia chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi. Mh Kalogeris Amekabidhi pikipiki hizo akiwa na lengo Kila kata Kuwa na Pikipiki moja, uwe Mradi wa Chama ili kuwezesha Kila kata Kuendesha Shuguli za Chama Bila kuwa wategemezi. Mbunge Kalogeris ameahidi kuhakikisha kata zote za jimbo hilo zinapatiwa Pikipiki. Mh Kalogeris amesisitiza Pikipiki hizo ni mali ya CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini na si mali ya watu binafsi.

 Mwenyekiti wa CCM Morogoro Vijijini Mh Jazar akisisitiza jambo wakati akitoa neno la Shukrani mara Baada ya Kupokea Msaada ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini  Mh Kalogeris aliyoitoa kwa ajili ya kukifanya Chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi.

 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar (Kulia) Akikabidi Pikipiki kwa Mmoja wa Mwakilishi wa kata zinazounda Wilaya ya Morogoro mjini Ikiwa kama mradi wa kukiwezesha chama hicho kujitegemea

             Wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya                                      Morogoro vijijini waliojitokeza wakati wa Kupokea Msaada huo.


Related

TUJUZANE 4767490862317969887

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item