TAARIFA RASMI KUTOKA JESHI LA MAGEREZA DHIDI YA UZUSHI KUWA BABU SEYA NA MWANAE WAMEACHIWA HURU

TANGU majira ya mchana kuna taarifa zilizagaa kwamba Babu Seya na mwanae Papi Kocha walikuwa wameachiwa huru na kuanza kusambazwa ujumbe...


TANGU majira ya mchana kuna taarifa zilizagaa kwamba Babu Seya na mwanae Papi Kocha walikuwa wameachiwa huru na kuanza kusambazwa ujumbe mfupi wa simu za mkononi na kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo Jeshi la Magereza limefunguka na kuweka bayana juu ya ukweli wa taarifa hizo kama taarifa yao inavyosomeka hapo chini;

Hivi sasa kuna taarifa zimesambaa kupitia Ujumbe mfupi wa simu (SMS) na mitandao ya kijamii zikihusisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wanaotumikia Kifungo cha Maisha gerezani. Wafungwa hao wanaotajwa ni Nguza Vicking(Maarufu kwa jina Babu Seya) na Johnson Nguza(Maarufu kwa jina la Papii Kocha).

Napenda kuufahamisha Umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo zote zilizotolewa kupitia njia hizo ni za Uongo na uzushi mkubwa na zinalenga kuipotosha jamii kwani wafungwa hao wapo gerezani na wanaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha Maisha gerezani kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Magereza nchini linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uhalifu huo na linawataka wale wote wanaotumiwa ujumbe wa aina hiyo waepuke kuusambaza ujumbe huo kwa wengine bali waufute, kwani kuendelea kuusambaza ni kosa kisheria.

Aidha, Jeshi la Magereza linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwabaini wanaosambaza ujumbe huo likishirikiana na Vyombo vingine muhimu kwa lengo la kuwakamata wahalifu hao ili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake.

Imetolewa na;
Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM.
Septemba 8, 2014

Related

OTHER NEWS 7208800537743420182

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item