WWF YAENDESHA MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI WA MANISPAA YA KINONDONI KUHUSU HEWA UKAA

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la WWF,limeendesha mafunzo kwa wafanyakazi wa idara mbalimbali za Halmashauri ya Manispaa ya K...



SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la WWF,limeendesha mafunzo kwa wafanyakazi wa idara mbalimbali za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) kuhusiana na ueneaji wa hewa ukaa na matumizi sahihi ya nishati jadidifu nchini.
Mafunzo hayo yametolewa na Mtaribu wa Programu hiyo kutoka WWF  Teresia Olemako alisema lengo la mafunzo hayo ni katika kuhakikisha kuwa watumishi wa Idara mbalimbali wanakuwa na ufahamu juu ya kukabiliana na madhara ya hewa ukaa na umuhimu wa kutumia nishati jadilifu.
Alisema mafunzo hayo yatahusu watumishi kutoka mikoa mitatu ambayo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha ambao majiji na miji yao imeingia katika shindano la kimataifa la kukabiliana na utunzaji wa mazingira ambalo litafanyika mwakani kwa kushirikisha nchi 18 duniani Tanzania ikipata nafasi kwa mara ya kwanza.
Olemako alisema juhudi za WWF kwa kushirkiana na ICLEI ni kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya nishati jadilifu kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira ambao unachangia kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi kote duniani.

“WWF kama shirika lisilo la Kiserikali tumejipanga kushirikiana na watumishi wa mikoa hiyo niliyoitaja hapo juu katika kuhakikisha kuwa suala la kupunguza hewa ukaa na kuhimiza matumizi ya nishati jadilifu ni moja ya majukumu yao ambao nao watatumia mafunzo hayo kuwapatia wananchi elimu zaidi”, alisema.

Mtaribu huyo wa Programu ya Nishatu Jadilifu alisema mradi huo utakuwa ukitambaulika kwa kauli mbiu ya (Chakula, Nishati, Taka Ngumu na Maji) kutumika kama njia mbadala ya kukabiliana na uharibifu mazingira katika maeneo husika.

Alisema nishati jadilifu ikitumika ipasavyo itakuza uchumi wanchi pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na ukweli kuwa haina madhara na ipo kwa wakati wote hivyo ni vema kila mmoja kuwa balozi mzuri katika kuelimisha jamii.


Akizungumzia juu ya shindano hilo alisema ni vema kwa mikoa husika kufanya kila liwezekano ili kuweza kuleta ushindani wa kweli jambo ambalo linaweza kupelekea Tanzania kuibuka na ushindi ambao utakuwa kichochoe cha utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati jadilifu kuongezeka zaidi.

Aidha alisema kutokana na tahmini iliyofanywa na shirika hilo,inakadiriwa kuwa hadi mwaka 2025 jiji la Dar es salaam litakuwa na wakazi zaidi ya mil.6.2 huku mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka mara mbili zaidi ya sasa jambo ambalo linahitaji kufanyika maandalizi mapema kabla hali haijawa mbaya.


Akifungua semina hiyo,Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Injinia Mussa Natty,alisema kila idadi ya watu inapoongezeka,miundombinu na mahitaji ya kibinadamu pia huongezeka hivyo kuifanya jamii kuhakikisha inaboresha mahitaji muhimu.

Natty alisema kutokana na hali hiyo WWF inapaswa kuongeza juhudi zaidi za kutoa elimu na kusaidia utekelezaji wa miradi ambayo inaweza kuwa na tija kwa Taifa na wananchi wake kwa vizazi vijavyo kwani kutokufanya hivyo kunaweza kuwa sababu ya kuleta mitafaruku mijini.

Mkurugenzi huyo alisema miradi kama hiyo ikiwa endelevu ni wazi kuwa kila mwanajamii atakuwa balozi mzuri wa kuhitaji mbadilo chanya ambao hayatamuathiri yeye na kizazi chache.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza WWF Tanzania kwa kushirikia na WWW Sweden kwa kuja na mradi huu na manispaa yangu ikawa moja wapo naamini tutaufanyia kazi vizuri kwani sisi Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla tumeathirika sana na mabadiliko ya Tania nchi”, alisema.

“Pia nasema kwa kila mmoja wetu ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es salaam,anahitaji kuwajibika katika sehemu yake ili kuhakikisha mahitaji muhimu ya kibinadamu yanapatikana jirani na jamii ili kuiondoa jamii katika hali ya umasikini unaosababisha ukataji na uharibifu wa misitu”,alisema.

Naye Mwanasheria wa Jiji la Dar es Salaam Philip Mwakyusa ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Jiji Wilson Kabwe alisema jiji wameupokea mradi kwa mikono yote na watatoa ushirikiano kwa WWF ili iweze kutekeleza mradi huo kwa mafanikio makubwa na ya yenye tija kwa jiji.

Alisema mikakati ya jiji ni kuhakikisha kunakuwepo na ushirikiano baina yake na wadau wengine ambao kwa pamoja watasaidia kuwepo kwa mabadiliko katika utunzaji wa mazingira ambao utakuwa ni faida kwa jiji la Dar es Salaam.

Mwakyusa alisema bila kuwepo kwa ushirikiano ni wazi kuwa yapo mambo mengi yanakwama kutokana na ufinyu wa bajeti hivyo wadau wanaombwa kujitokeza ili kukabiliana na hali ongezeko ya hewa ukaa inapungua kama sio kuisha kabisa.

Related

TUJUZANE 8668362425191616472

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item