NAPE AJIBU MAPIGO KATIBA MPYA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema madai yaliyotolewa bungeni dhidi ya chama hicho hayana ukweli. Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uen...


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema madai yaliyotolewa bungeni dhidi ya chama hicho hayana ukweli. Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alimtupiakombora Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) akimfananisha na mgonjwa mwenye kifafa cha siasa.

Kauli hiyo ya CCM imekuja siku chache baada ya Tundu Lissu, kudai bungeni kuwa CCM ilimeteka nyara mchakato wa Katiba mpya ikiwamo kuandika barua kwa viongozi wake wa ngazi zamikoa.

Nnauye aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa matamshi ya Lissu hayana mashiko mbele ya Watanzania.

Alisema ni wajibu wa CCM kuhakikisha nchi inapata katiba iliyokubalidika na wananchi bila kupata shinikizo kutoka mawakala wa mabeberu.

Nape alisema CCM kama ilivyo taasisi yoyote makini na yenye uzalendo kwa nchi yake, katika mchakato wa uundwaji wa katiba mpya ina jukumu la kuwahamasisha wanachama na wasio wanachama wake kushiriki mchakato wa katiba nchini kwa kutambua umuhimu wake.

Alisema tofauti kati ya CCM na CHADEMA katika hilo ni kwamba wakati CCM wanahamasisha watu washiriki kwenye mchakato wa katiba nchini, chenyewe (Chadema) kinahamasisha watu wavuruge au wasishiriki mchakato wa kupatikana Katiba mpya ya nchi.

"Mfano mzuri ni jitihada zao za kususia mchakato huu kwa visingizio vya kitoto kabisa. Juhudi zao za kumtaka Profesa Baregu ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na ambaye wao wenyewe walimpendekeza kwenye tume, eti sasa ajitoe kwenye tume zimegongwa mwamba.

"CCM inampongeza kwa dhati Profesa Baregu kwa uzalendo na ukomavu wa siasa aliouonyesha kwa kuwakatalia kujitoa kwenye tume na kuweka mbele maslahi ya taifa lake.

“Kukataa kwake kujitoa kwenye tume kwa hoja za kitoto za CHADEMA ilipaswa kuwa fundisho kwa vibaraka hawa.

"CHADEMA ni kama nguruwe ambaye huweza kuzaa watoto wake kisha akishikwa njaa huanza kuwala watoto wake mwenyewe. Mchakato wa katiba nchini ni matunda ya viongozi wa CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM,” alisema na kuongeza:

"Ifahamike kuwa mawasiliano na mjadala juu ya mchakato wa uundwaji wa katiba mpya nchini hayakuanza jana ndani ya CCM, bali yalianza siku nyingi kwa Chama kuunda kamati iliyopitia na kuja na maoni ya CCM juu ya nini kiwamo kwenye katiba mpya.

"Taarifa hiyo haikufanywa siri. Iliwasilishwa mbele ya vikao kadhaa vya Chama na kisha kutangazwa kwa umma, hivyo hoja kwamba mawasiliano ndani ya chama juu ya mchakato huo wa Katiba nchini umelenga kuhujumu mchakato huo hayana maana yoyote.

“Badala yake hoja hiyo imebeba mtazamo finyu wa wanasiasa wenye tabia za nguruwe za kula watoto wake mwenyewe apatapo njaa."

SOURCE: MTANZANIA

Related

OTHER NEWS 6908179793951503802

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item