HIZI NDIO MBINU ZA KUFANIKISHA ELIMU KWA MTOTO WA KIKE

Kwa kuwa watoto wa kike nao wana haki ya kuhitimu masomo kama ilivyo kwa wenzao wa kiume, chapisho lingine la HakiElimu liitwalo: Mbin...

Kwa kuwa watoto wa kike nao wana haki ya kuhitimu masomo kama ilivyo kwa wenzao wa kiume, chapisho lingine la HakiElimu liitwalo: Mbinu za kufanikisha elimu kwa wasichana, linapendekeza njia kadhaa za kuwanusuru wasichana ili hatimaye watimize ndoto za maisha yao. Chapisho linaeleza:
Wazazi na walezi kuwajengea watoto wa kike msingi mzuri wa malezi kwa kuongea nao na kuwaelekeza.
Tunaweza kuwajengea uwezo wasichana kutambua uwezo wao ili kujijengea msingi mzuri katika maisha yao, kwa kuwapa maadili ya msingi tangu wakiwa wadogo.
Kaya masikini ziwezeshwe kwa mitaji midogo midogo, mikopo, ruzuku za kilimo na kupunguziwa ushuru.
Mbinu hii itasaidia kupunguza makali ya umaskini kwa kaya zenye maisha duni. Watanzania ni wachapakazi, iwapo watawezeshwa wataweza kujiingizia kipato kitakachowawezesha kuwapatia watoto wao elimu.
Watoto wa kike wasome kwenye shule zilizo karibu na maeneo wanayoishi.
Hili litapunguza tatizo la wasichana kuacha shule na kupunguza uwezekano wa kupata vishawishi na vikwazo vya kielimu. Wazazi wanaowaandikisha watoto wa kike shule za mbali, hawana budi kuacha maana ni kuwajengea mazingira ya kupata vikwazo zaidi kimasomo..
Shule za mbali ziwe na mabweni kwa wasichana
Hili litapunguza tatizo la wasichana kuacha shule, hasa sehemu za vijijini ambako wasichana wanalazimika kutembea umbali mrefu. Wakijengewa mabweni itawasaidia kufanikisha masomo yao.
Wasichana waliopevuka wapewe elimu ya uzazi kwa uwazi zaidi
Kama wasichana wataelewa kuhusu mabadiliko yao kimakuzi na elimu ya uzazi kwa jumla, watakuwa wanajua wanachokifanya wakati wote, hivyo itakuwa rahisi sana kwao kujiepusha na vitendo vya ngono, pia kujikinga na mimba za utotoni zinazowagharimu elimu yao na afya zao.
Umuhimu wa kuendelea kuelimisha na kuhamasisha kuachana na mila kinzani zinazowaandaa wasichana kufeli maisha yao.

Lazima tuziepuke sherehe za unyago, jando na sherehe nyingine za kijadi zinazowakuza wasichana huku wakiwa na umri mdogo.
Sheria kali zichukue mkondo wake kwa wanaume wanaowasababishia wasichana kukatisha masomo na kuwaharibia maisha
Pia sheria ichukue mkondo wake hata kwa wazazi wanaokula njama na watoto wao kuruhusu uhusiano na mwanamume fulani ili wapate kipato.Tabia ya kusameheana kiujirani huku mtoto wa kike akikatishwa masomo yake imepitwa na wakati, wazazi, walezi wanapaswa kuwa wakali linapotokea jambo kama hili.
Wazazi wa kiume kuacha tabia za kizamani za kuwa mbali na watoto wa kike.Wazazi wote hawana budi kuongea na watoto wa kike na kuwasikiliza na kuachana na tabia ya kuwaachia kinamama kazi ya ushauri na kuongea na watoto wa kike. Wasichana wanahitaji ukaribu wa wazazi wa kiume.
Kuwe na dhamira ya kweli ya watendaji hasa wa Wizara ya Elimu kwenye ujengaji wa miundombinu ya shule na vifaa vya kujifunzia.
Mazingira rafiki ya shule kwa watoto wa kike yatasaidia kuwabakiza wasichana shuleni na hatimaye kuhitimu masomo yao. Maji shuleni, vyoo visafi, vyumba vya usiri na usalama , ni muhimu viwepo shuleni.
Elimu itolewe kwa jamii kuhusu umuhimu wa kumwendeleza mtoto wa kike na faida zake kwa msichana na jamii
Jamii kubwa ya Tanzania hasa sehemu ambazo zina mwamko mdogo wa elimu, bado zinahitaji kuhamasishwa zaidi. Wanaharakati, vyombo vya habari, Serikali za mitaa na jumuiya mbalimbali wanapaswa kutoa elimu kwa umma, hasa maeneo ya vijijini ambako kuna tatizo kubwa la uelewa.
Wazazi na walezi wawapunguzie wasichana wingi wa kazi za nyumbani.
Katika jamii zetu watoto hasa wa kike wamekuwa msaada mkubwa katika familia kusaidia majukumu madogo madogo, hasa ya kupika na shughuli nyingine za nyumbani na shambani.

Baadhi ya wazazi humfanya mtoto wa kike kama punda wa kumfanyisha kazi nyingi za nyumbani bila kuchoka wala kupumzika.
Kwa kuwa nyumbani ni shule pia, wazazi au walezi watambue kuwa mtoto anahitaji muda wa kutosha ili kukuza maarifa.
Kutokufanya vizuri shuleni kutamkatisha tamaa na kujisikia vibaya, na hatimaye hatokuweza kuendelea kuaibika kwa kufeli, matokeo yake anaacha shule.

MWANANCHI

Related

ELIMU 448004812174274579

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item