HATEMAYE MUME WA JOYCE KIRIA AONEKANA MAHAKAMANI MKOANI TABORA KWA TUHUMA ZA KUMWAGIA MTU TINDIKALI
Bw.Henry Kileo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabo...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/06/hatemaye-mume-wa-joyce-kiria-aonekana.html
Bw.Henry Kileo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza. |
Ulinzi katika Mahakama hiyo uliimarishwa ipasavyo. |
Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013 |
Na Josephat Isango wa Tanzania Daima.
KAIMU Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, anashikiliwa na polisi , akihusishwa na tukio la kumwagiwa tindikali, Musa Tesha. Tesha alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana Septemba 9, mwaka juzi kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, uliomuweka madarakani Dk. Kafumu Dalali.
Akizungumza juzi na Tanzania Daima kabla ya kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi, Kilewo alisema hajui anachoitiwa na kwamba anatekeleza wito wa jeshi hilo kuwa afike ofisini kwao. “Sijui ninachoitiwa, nimepigiwa simu naenda kutekeleza wito, nimesha wataarifu mawakili wangu ninaowaamini, kwa kuwa chochote kinaweza kutokea cha msingi Watanzania wapenda mageuzi waniombee kwa Mungu,” alisema Kilewo.
Wakili wa Kilewo, Peter Kibatala, alisema baada ya mteja wake kuhojiwa kwa muda wa saa tano juzi alielezwa kuwa anapelekwa Igunga, mkoani Tabora kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya kutumia tindikali na kujeruhi.
Kibatala alisema anasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kumnyima dhamana mteja wake ilhali kosa wanalomtuhumu linadhaminika na kwamba hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kumzuia mtu kwa zaidi ya saa 24 pasipo kumfikisha mahakamani. Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia tindikali na kudhuru watu ni pamoja na Oscar Kaijage wa Shinyanga na Evodius Justinian wa Bukoba.