KUJERUHIWA KWA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI MHE. JOSHUA NASARI, APIGWA NA GREEN GUARD

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amepigwa na kujeruhiwa vibaya, damu zinamtoka puani. Amepigwa na vijana wa Kisomali, katika eneo...



Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amepigwa na kujeruhiwa vibaya, damu zinamtoka puani.

Amepigwa na vijana wa Kisomali, katika eneo la Zaburi kata ya Makuyuni Jimbo la Monduli.

Taarifa za awali zinasema baada ya Nassari kuondoka na gari  jingine, waliokuwa wanafuatana naye Kiongozi wa CHADEMA aliyetambulika kwa jina la Teddy Ndossi na dereva wa Nassari walienda kujibanza sehemu. 

Dereva wa Nassari Guardian  Palangyo amepigwa mdomoni amevunjwa meno mawili, na kwa sasa wamempiga Katibu wa CHADEMA wa eneo hilo anayeitwa Kilongola, wapo Kituo cha Polisi Makuyuni kutafuta msaada zaidi.


Habari kutoka kwenye blogu ya HabariMseto
 

Related

OTHER NEWS 6417522186522754574

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item