TAARIFA YA HALI YA MAJERUHI WA MLIPUKO WA BOMU LA SOWETO, ARUSHA

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha, Dk Josiah Mlay amewamtaja marehemu wa mlipuko uliotokea jana mkutanoni Soweto, Arusha kuwa...

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha, Dk Josiah Mlay amewamtaja marehemu wa mlipuko uliotokea jana mkutanoni Soweto, Arusha kuwa ni Judith Mushi, (46) mkazi wa Sokoni One, jijini Arusha.Mama Judith Moshi ambaye aliwahi kuwa M/Kiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Wilaya ya Arusha Mjini na mpaka mauti yanamkuta alikuwa ni Katibu wa Chama Kata ya Sokoni.  Na mwingine ni kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 15-16 asiyetambulika jina bado, ambaye alifia katika hospitali ya AICC.

Dk Mlay, amesema katika tukio hilo hospitail hiyo imepokea majeruhi 10, kati yao 9 ni wanaume na mwanamke mmoja aitwaye Sharifa  Jumanne, ambaye hali yake imeelezwa kuwa mbaya. Amesema kuwa katika uchunguzi wa awali imegundulika kuna kuipande cha chuma kwenye mapafu ambacho kinatokana na mlipupuko huo.

Aidha, amesema kuwa majeruhi mwingine aliyepata majeraha ya kichwa  amehamishiwa kwenye hospitali ya Seliani ya Arusha  kwa uchunguzi zaidi akisubiriwa kupelekwa kwenye hospitali ya rufani ya KCMC, Moshi.

Dk Mlay, amesema hali za majeruhi wengine waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru, zinaendelea vizuri.

Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, amewatembelea majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa mahospitalini.

Viongozi mbalimbali wa CHADEMA wametembelea eneo la tukio.


SOURCE: CHADEMA SOCIAL MEDIA

Related

OTHER NEWS 4060955309227017563

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item