MWANAFUNZI WA MWAKA WANNE WA SHERIA ALIYEJERUHIWA KWA RISASI USIKU WA KUAMKIA LEO ANAENDELEA VYEMA BAADA YA KUONDOLEWA RISASI MWILINI

Mwanafunzi aliyejeruhiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo amefanyiwa operation na zoezi hilo limemalizika salama na hivi sasa yupo kwenye m...


Mwanafunzi aliyejeruhiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo amefanyiwa operation na zoezi hilo limemalizika salama na hivi sasa yupo kwenye moja za wodi za hospitali ya Muhimbili. Taarifa hiyo imetolewa muda si mrefu na mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam Pro. Mukandara, wakati alipopewa nafasi ya ufunguzi wa mjadala wa kigoda cha Mwalimu unaondelea muda huu kwenye ukumbi wa Nkuruma wa chuo kikuu cha Dar es salaam.

TUJIKUMBUSHE
Usiku wa kuamkia leo wanafunzi wa mwaka wa nne wa chuo kikuu cha mlimani wanaochukua shahada ya sheria
walivamiwa na majambazi maeneo ya Yombo chuoni hapo. Wanafunzi hao walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha,  na majambazi kuanza safari yao.

Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.

Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi.

Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili chuoni hapo. 

Related

BREAKING NEWS!!!!!! RAIS ATENGUA UTEUZI WA MAWAZIRI 4, KAGASHEKI ATANGAZA KUJIZULU BUNGENI

TAARIFA ILIYOTELEWA BUNGENI USIKU HUU NA WAZIRI MKUU, RAIS AMETENGUA UTEUZI WA MAWAZIRI WAKE 4, KABLA YA TAARIFA YA WAZIRI MKUU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KAGASHEKI ALITANGAZA KUJIUZULU R...

MWALIKO KWA MAKUNDI MBALIMBALI KUPENDEKEZA MAJINA YA WATAKAOTEULIWA KUWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA TANZANIA INFORMATION SERVICES PRESS RELEASE                P.O. Box 9142, Dar es Sal...

NEC YATANGAZA UCHAGUZI KWA KATA 27

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kata 27 nchini ambazo zipo wazi kutokana na madiwani wake kufariki dunia na wengine kupoteza sifa, uchaguzi wake utafanyika Februari 9 mwakani.Akizungumz...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904759
item