SAKATA ZIMA LA KUPIGWA KWA MBUNGE WA KASULU KIGOMA MHE. MOSSES MACHARY
Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospita...
Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana jana jioni mjini Dodoma.
Shuhuda aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema Mh. Machalli alipigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.
Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu.