REDBRIGADE NI UASI SI SAWA NA GREEN GUARD YA UVCCM
KATIBU MKUU WA UVCCM, MARTINE SHIGFELLA AMZEZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA KELEZA MAMBO MATATU MUHIMU LIKIWEMO HATUA YA CHADEMA K...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/07/redbrigade-ni-uasi-si-sawa-na-green.html
KATIBU MKUU WA UVCCM, MARTINE SHIGFELLA AMZEZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA KELEZA MAMBO MATATU MUHIMU
LIKIWEMO HATUA YA CHADEMA KUTAKA KUANZISHA MGAMBO KINYUME CHA SHERI.
SASA FUATILIA MAELEZO HAYA KAMA YALAIVYOTAYARISHWA NA ASENGA ABUBAKAR WA MAKAO MAKUU YA UVCCM
1.kuanzishwa kwa REDBRIGED ya chadema hakukubaliki, chadema lazima
watofautishe kati ya vijana wa CCM ambao wanapewa mafunzo ya ukakamavu
juu ya chama katika kueneza sera na kuandaliwa kama viongozi wa baadae
na kikundi cha kijeshi kinachoanzishwa na wao kwa maana wanaosema ya
kujilinda DHIDI YA POLISI
CCM haina kikundi cha kujilinda dhidi
ya polisi au wanajeshi.UVCCM inavikundi kwa ajili ya ukakamavu wa
vijana wake,je chadema hawatakuwa na haja ya kuwa na askar polisi kwenye
mikutano yao? so hilo tunalilaani na hatuliungi mkono
2.Tunataka vijana wetu toka kwenye mashina matawi ,kata na wilaya
washiriki vyema kuwaaambia wajumbe wa mabaraza ya katiba maoni wanayoona
yanafaa kwenye katiba mpya
hatuungi mkono ujio wa serikali
tatu , gharama za serikali hizo ni mzigo kwa watanzania lakini pia
mchakato wa kuleta serikali ya tatu haukubaliki,unawezaje leo upate
mtoto wakati mzazi mmoja haujamtafuta?
inamana zanzibar wanakatiba yao, bara unasema hawana katiba yao eti itakuja baadae?
walipaswa kwanza waje na mapendekezo ya rasimu ya jinsi serikali ya zanzibar inavyopaswa kuwa katika serikali ya muungano
pili waje na mapendekezo ya katiba ya jinsi serikali ya bara itakavyokuwa
na mwisho waje na rasimu ya serikali ya muungano ili kila upande ujijue
na si tuanze na serikali ya muungano alafu eti bara tuje tujijue baadae
PILI katika huo mchakato wa katiba kuna mambo mengi ambayo hayapo sawa,
mfano eti wanataka vijana wagombee ubunge wakiwa na umri wa miaka 25
hii si sawa,mimi nilizani wangesema kwa kuwa vijana wana haki ya kupiga
kura wa kiwa na miaka 18, basi wawe na haki ya kugombea ubunge pia
wakiwa na miaka hiyo hiyo.
Hao wajumbe wa katiba walipata uteuzi wa kuwa mabalozi nje ya nchi wakiwa na miaka 18 mfano dk salim A salim
sasa wanataka kuwachelewesha tu vijana ambao mtakubaliana nami kuwa
sasa wamekuwa kiakili zaidi kuliko vijana wawakati ule wa analojia na
wakati huu wa dijitali
na kwakuwa hakuna kijana aliegombea
ubunge akiwa na chini ya maiaka 25 ameonyeshwa kushindwa majukumu yake
basi tunaomba umri ubaki ule ule wa awali wa miaka21 au uwe miaka 18.
3. Mwisho kutakuwa na uchaguzi wa chipukizi taifa mwaka huu 2013 na
fomu zinaanza kutolewa tar 5/7-30/07/2013 fomu zitatolewa mikoani,UVCCM
zanzibar na UVCCM makao makuu zanzibar
nafasi zinazogombea ni
1.mwenyekiti wa chipukizi taifa nafasi 1
2.makamu mwenyekiti taifa nafasi 1
3.wajumbe wa wili wa baraza kuu taifa kutoka chipukizi nafasi moja bara na moja zanznibar
4. wajumbe wanne wakamati ya uendeshaji taifa wawili toka zanznibar na wa wili toka bara
5.wajumbe watatu wa mkutano mkuu wa UVCCM taifa chipukizi kwenda
mkutano mkuu wa UVCCM Taifa ,nafasi mbili toka bara na nafasi moja toka
zanzibar
KATIBU MKUU WA UVCCM, MARTINE SHIGFELLA AMZEZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA KELEZA MAMBO MATATU MUHIMU LIKIWEMO HATUA YA CHADEMA KUTAKA KUANZISHA MGAMBO KINYUME CHA SHERI.
Posted by
Unknown