WABUNGE WANUNULIWA IPADS
Kumezuka malalamiko nchini Uganda baada ya wabunge kununuliwa tabiti au (iPads) kwa pesa za Umma. Afisaa mkuu wa Bunge amesema kuwa ta...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/12/wabunge-wanunuliwa-ipads.html
Kumezuka malalamiko nchini Uganda baada ya wabunge kununuliwa tabiti au (iPads) kwa pesa za Umma.
Afisaa mkuu wa Bunge amesema kuwa tabiti hizo zitawafanya wabunge kuwa makini wakati wa vikao vya bunge.
Kamishna wa bunge Emmanuel Dombo
amesema kuwa wabunge sasa wanaweza kupata stakabadhi zao rasmi wakati
hata wakiwa nje ya ofisi zao au wakiwa safarini.
Pia alisema kuwa pesa walizonunulia iPad hizo
zitasaidia kuepuka kutumia kiwango kikubwa cha karatasi na kupunguza
gharama ya matumizi.Wabunge wote wa bunge la Uganda ambao idadi yao ni 375, wanunuliwa zilizogharimu kima cha dola laki tatu na sabini.
Wakosoaji wanahoji ikiwa wanasiasa wanajua hata
kuzitumia tabiti hizo na kusema kuwa tayari wananchi wanalipa pesa
nyingi sana kwa mishahara ya wabunge. Mwaka jana wabunge wa Uganda walipiga kura kutaka mishahara na marupurupu yao kuongezwa kwa asilimia arobaini. Pia walipokea marupurupu ya zaidi ya dola 40,000 ili kujinunulia gari jipya.
Mbunge wa Uganda kwa sasa hulipwa, dola elfu nane , ingawa nchi hiyo inakumbwa na matatizo ya kiuchumi. Wananchi wanasema kua hatua hii ya serikali ni
kuharibu pesa za mlipa kodi, ikizingatiwa kuwa wabunge hao wanalipwa
mishahara ya juu ambayo inawawezesha kujinunulia vifaa hivyo wao
wenyewe.
BBC SWAHILI