TRAFIKI FEKI KUMBE NI MFUNGWA ALIYETOROKA JELA

  Na Mwandishi Wetu MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam am...

 
Na Mwandishi Wetu
MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko  Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani, Amani lina mpya hiyo.
Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.

JINA HALISI
Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda.
“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.

YADAIWA ALIKUWA ASKARI MAGEREZA
Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.

ADAIWA KUNASWA UJAMBAZI, ATUPWA JELA MIAKA 30
Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.
 “Mwaka 2002 mpaka 2003, Kinanda alipata kesi ya ujambazi akiwa na wenzake, sikumbuki idadi yao. Kesi iliisha kwa hukumu ya miaka 30 jela kwenye Gereza la Isanga hapa Dodoma,” alisema mnyetishaji huyo.
“Akiwa gerezani, Kinanda alionekana mtiifu kiasi kwamba alipewa cheo cha kusimamia wenzake, yaani mnyapara wakiamini anaendelea vizuri na kifungo chake hicho.
“Hakuna aliyejua kama jamaa anaweza kutoroka. Ama kweli moyo wa mtu anaujua mwenyewe. Hivi hapa (Gereza la Isanga) wafungwa wenzake wameshangaa kusikia jamaa amekuwa trafiki huko Dar es Salaam,” kilidai chanzo.

ADAIWA KUTOROKA JELA
Habari zaidi ziliendelea kudai kwamba, Desemba 10, 2012 akiwa gerezani, mfungwa huyo alitoroka katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya uangalizi wa askari magereza aliyejulikana kwa jina moja la Shaibu.

Ilidaiwa kuwa, baada ya picha yake kuonekana kwenye gazeti, askari magereza wa Isanga waliutaarifu uongozi mara moja ambapo nao ulituma wachunguzi  jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumtia mikononi mfungwa huyo ili akamalizie kifungo chake cha miaka thelathini jela.
Inadaiwa kuwa, wachunguzi hao ambao ni askari magereza  wapo Dar wakisubiri siku ya kesi ya kujifanya trafiki itakapopelekwa kusikilizwa kwa hakimu.

HABARI MPYA, ADAIWA KUFARIKI DUNIA SEGEREA, DAR
Wakati mnyetishaji wetu kutoka gerezani Isanga Dodoma akianika madai ya siri hiyo nzito, Agosti 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mwandishi Wetu, Makongoro Oging’  alipata taarifa kuwa, mtuhumiwa huyo wa kutenda kosa la kujifanya trafiki amefariki dunia ghafla akiwa gerezani Segerea.

Ilibidi mwandishi wetu amtafute Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Mtiga Omar na kumuuliza kuhusu madai hayo ya kifo ambapo alisema:
“Si kweli kwamba amekufa, bali ana tuhuma nyingine ya kutoroka gerezani ambapo tutamfungulia mashitaka mengine  ya kutoroka akiwa gerezani anatumikia kifungo chake.”
Juhudi za kumpata Mkuu wa Gereza la Isanga, Dodoma zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

James Hussein kama ndiye Ali Kinanda yupo Gereza la Segerea, hadi Septemba 5, 2013 kesi yake itakaporudi tena mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde kwa ajili ya kusikilizwa.

SOURCE: Global Publishers

Related

MUUAJI WA TARIME AFARIKI DUNIA

KAMANDA WA POLISI MKOANI MARA - JUSTUS KAMUGISHA  TARIME MTUHUMIWA wa mauaji ya watu tisa na unyang'anyi wilayani Tarime mkoani Mara, aliyekuwa akihojiwa Polisi kwa tuhuma zilizokuwa z...

MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI ULIOFANYIKA 09/02/2014 KATIKA KATA MBALIMBALI NCHINI, CCM YASHINDA KWA KISHINDO KATA 23, CHADEMA WAAMBULIA KATA 3 NA NCCR YAPATA KATA 1

MATOKEO YA JUMLA NDIYO YALIVYOLIPOTIWA KUTOKA VYANZO MBALIMBALI VYA UDIWANI.CCM YAPATA KATA 24 HUKU CHADEMA IKIPATA KATA 3MATOKEO YA UDIWANI KATA YA SOMBETINI ARUSHA. CHADEMA KURA 2548CCM...

MBUNGE AUAWA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Mbunge mmoja wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele kupinga mauaji ya Waislamu nchini humo, ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui. Jean-Em...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904759
item