KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO CHALINZE: VYAMA VYASHAURIWA KUWATUMIWA MAWAKALA WA JIMBO HUSIKA
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damiani Lubuva TUME ya Taifa ya uchaguzi imevitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki kwe...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/04/kuelekea-uchaguzi-mdogo-chalinze-vyama.html
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damiani Lubuva
TUME
ya Taifa ya uchaguzi imevitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki kwenye
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kuhakikisha kuwa wanawatumia
mawakala wanaotoka katika maeneo au vituo husika vya kupigia kura,ambao
watawafahamua na kuwatambua wapiga kura wa eneo husika.
Akizungumza
katika mkutano baina ya vyama vya siasa na tume hiyo,Mwenyekiti wa Tume
hiyo,Jaji mstaafu Damiani Lubuva amesema kuwa pamoja na kuwa sheria
haikatazi kwa vyama kuteua mawakala wa vyama kutoka majimbo mengine ya
uchaguzi,lakini ni vyema kuwateua wale wanaotoka katika maeneo hayo ili
kuweza kuwatambua wapiga kura wao.
“Kumekuwa
na mazoea kwa baadhi ya vyama vya siasa kuteua mawakala wanaotoka
majimbo mengine ya uchaguzi japokuwa sheria haikatazi lakini ni vema
vyama vikatumia busara ya kuwateua mawakala kutoka katika maeneo hayo
ili kuweza kuwatambua wapiga kura” alisema Jaji Lubuva.
Akizungumzia
kuhusu umuhimu wa wananchi kujitokeza kupiga kura,Lubuva alisema kuwa
tume inatambua juhudi za viongozi wa vyama vya siasa kuwahamasisha
wananchi kujitokeza kushiriki katika uchaguzi lakini akawataka viongozi
hao kuhakikisha kuwa wanawahamasisha zaidi wapiga kura kujitokeza kwa
wingi siku ya kupiga kura.
Akizungumzia
kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi huo mdogo wa Chalinze,Msimamizi
msaidizi wa uchaguzi wa jimbo hilo,ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Samweli Sarianga alisema kuwa vifaa
vyote na maandalizi yamekamilika japokuwa kumekuwako na changamoto
nyingi ikiwamo uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua kubwa
zilizonyesha hivi karibuni na kusisitiza kuwa iwapo hali ya hewa itakuwa
ni nzuri basi kuna uhakika wa vifaa vyote vya uchaguzi vitakuwa
vimefikishwa katika maeneo husika tayari kwa ajili ya kusambazwa katika
vituo vya kupigia kura.
Jumla
ya vyama 5 vinatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo mdogo wa Chalinze
ambapo lina idadi ya wapiga 92,939,ambapo vyama hivyo ni
CCM,CHADEMA,NRA,CUF na AFP.