NEC YATANGAZA UCHAGUZI KWA KATA 27

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kata 27 nchini ambazo zipo wazi kutokana na madiwani wake kufariki dunia na wengine kupoteza s...

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kata 27 nchini ambazo zipo wazi kutokana na madiwani wake kufariki dunia na wengine kupoteza sifa, uchaguzi wake utafanyika Februari 9 mwakani.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema uchaguzi huo utafanyika katika halmashauri 23 baada ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa.

Alizitaja kata hizo na halmashauri zake zikiwa kwenye mabano ni Segela na Mpwayungu (Chamwino), Ukumbi na Ibumu (Kilolo), Nduli (Iringa), Malindo (Rungwe) na Santilya (Mbeya).

Nyingine ni Tungi (Morogoro), Mkwiti (Tandahimba), Mkongolo (Kigoma), Sombetini (Arusha), Mrijo (Chemba), Magomeni na Kibindu (Bagamoyo), Mtae (Lushoto), Ubagwe (Ushetu) na Namikago (Nachingwea).

Kata nyingine ni Partimbo na Loolera (Kiteto), Kiwalala (Lindi), Kilelema (Buhigwe), Kiomoni (Tanga), Kasanga (Kalambo), Rudewa (Kilosa), Kiborloni (Moshi), Njombe Mjini (Njombe) na Nyasura (Bunda).

Alisema uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Januari 15, wakati kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 16 hadi Februari 8 na siku ya kupiga kura itakuwa Februari 9.

Alipoulizwa kama Kata ya Kisesa iliyopo Mwanza itaingizwa katika uchaguzi huo baada ya aliyekuwa diwani wake, Clement Mabina kuuawa na wananchi, alisema haitaingizwa katika uchaguzi huo.

Alisema utafanyika baada ya Halmashauri ya Ilemela kupeleka maombi ya kuomba uchaguzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)

Related

MTWARA HALI SI SHWARI

Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani n...

MSEMAJI MKUU WA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI VIJANA NA MICHEZO WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013) 1. UTANGULIZIMheshimiwa Spika, Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohaba...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item