BOMU ARUSHA LAJERUHI WATU 6, ASKOFU LOBULU ALAANI

Askofu mkuu wa kanisa la Katoliki, jimbo kuu la Arusha Josephat Lobulu akitoa pole kwa baadhi ya majeruhi wa bomu.  ARUSHA Watu s...

Askofu mkuu wa kanisa la Katoliki, jimbo kuu la Arusha Josephat Lobulu akitoa pole kwa baadhi ya majeruhi wa bomu. 

ARUSHA
Watu sita wamejeruhiwa na kile kinachodhaniwa ni bomu la kurusha eneo la lake tatu USA river wilayani Arumeru mkoani Arusha siku ya mkesha wa mwaka mpya  walipokuwa wakitoka kanisani kuelekea majumbani kwao.

Wakizungumza na BERTHA BLOG, kwa nyakati tofauti katika hospitali ya Tengeru iliyopo wilayani Arumeru, baadhi ya majeruhi wa tukio hilo walisema kuwa siku ya mkesha wa kuupokea mwaka 2014 walipokuwa wakitoka kanisani (Kanisa katoliki parokia ya USA river) waliweza kusikia mlio mkubwa wa kitu kama bom la kurusha ndipo baadhi yao walioangukiwa na bom hilo kuweza kujeruhiwa vibaya na kuanguka chini huku wakivuja dam nyingi sehem mbalimbali za mwili.

Walisema kuwa bom hilo lililorushwa na Askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha lilikuwa na lengo la kuwatawanya watu waliokuwa wakichoma matairi barabarani katika eneo hil  ikiwa kama sehemu ya kusherehekea mwaka 2014.

Kwa upande wake Askofu mkuu wa kanisa la katoliki jimbo kuu la Arusha, Josephat Lobulu akizungumzia tukio hilo alisema kuwa ni tukio la kulaaniwa, hivyo ameliomba jeshi la polisi kushughulikia jambo hilo.

Alisema kuwa amesikitishwa na tukio hilo, lakini yeye kama mtumishi wa Mungu anapaswa kuwaombea wote walioathrika na tukio hil ikizingatiwa wamepatwa na tukio hilo mita chache tu kutoka katika nyumba ya Mungu (Kanisani).

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
 Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas akizungumza na waandishi wa habari, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kulifuatilia kufaham chanzo cha tukio hilo
"Taarifa nimezipata lakini uchunguzi unaendelea kujua chanzo na muhusika sambamba na ukweli wa mlipuko huo ili kujua kama kweli ni bom na ni la aina gani".

Related

MNUNUZI WA NYUMBA/KIWANJA HII NI NAMNA YA KITAALAM YA KUJUA ENEO UNALONUNUA KAMA LINA MGOGORO AU HAPANA

  Na   Bashir   Yakub Makala zilizopita  nilieleza   mambo au taarifa muhimu  zinazopaswa kuwa kwenye  mkataba wako  unapokuwa unanunua  nyumba/k...

JAJI MUTUNGI AVIONYA VYAMA VYA SIASA VINAVYOENDEKEZA MIGOGORO

 Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi. Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa. Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi h...

MAGARI YA ABIRIA NA WATALII KUTOKA TANZANIA YARUHUSIWA KENYA

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, LAZARO NYARANDU   WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema serikali ya Kenya imekubali kuyaruhusu magari ya abiria na watalii kutoka Tanzania...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904782
item