ZITTO KABWE KUTOJADILIWA NA KAMATI KUU LEO, MAHAKAMA KUU YATOA MAAMUZI
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika Mahakama Kuu ya Tan...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/zitto-kabwe-kutojadiliwa-na-kamati-kuu.html
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika
Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam leo, ambapo aliwasilisha ombi la
pingamizi la yeye kutojadiliwa kwenye kikao cha Kamati Kuu ya chama
hicho kinachofanyika leo, hadi rufaa yake ya kupinga
kuenguliwa wadhifa huo kwenye Baraza Kuu la chama hicho. Kushoto ni
Wakili wa Zitto, Albert Msando. Mahakama Kuu imekubaliana na Zitto Kikao
cha Kamati Kuu ya Chadema kinachofanyika leo kutomjadili
kwa namna yoyote.
Wanasheria wa Chadema, Tundu Lisu (kushoto) na Peter Kibatala waliofika kupinga hoja hiyo mahakamani.
Tundu Lisu na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana jambo wakati wakisubiri uamuzi wa mahakama
Zitto ana wakili wake Msando
wakiwasiliana na marafiki zao walipokuwa wakisubili uamuzi wa mahakama,
ambapo Zitto aliibuka kidedea kwa pingamizi lake kukubaliwa hivyo kikao
cha Kamati Kuu kinachofanyika leo kukatazwa kumjadili kwa namna yoyote Zitto.