KAULI YA ZITTO KABWE BAADA YA MAHAKAMA KUMPA USHINDI DHIDI YA CHADEMA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana alitinga  mahakama kuu  kupinga kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao a...



Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe jana alitinga  mahakama kuu  kupinga kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao ambacho kilikuwa kikutane leo.

Hii  ni  kauli  yake  baada  ya  mahakama  kumpa  ushindi;
"Jana tulikwenda mahakamani kwa ajili ya jambo moja tu kutaka haki itendeke kwa sababu mahakaama ndiyo chombo cha juu kabisa kwenye nchi yetu cha kuweza kutenda haki mara baada ya kamati kuu ya chama changu kufanya maamuzi ya  kunivua nafasi zangu ambayo niliandikiwa makosa 11

"Nilikata rufaa kwenye baraza kuu la chama ili baraza kuu liweze kuona kama kamati kuu ilifuata taratibu za chama kufikia maamuzi yale japo mimi naamini haijafuata taratibu za chama lakini kwa bahati mbaya viongozi wangu wa chama changu wameamua kuendelea na kikao cha kamati kuu.

"Hawajajibu barua yangu ya nia ya kukata rufaa na kuweza kupatiwa taarifa na mwenendo wa kikao ili niweze kukata rufaa kwa mujibu wa chama. Kwa hiyo nimekwenda mahakani ili mahakama iweze kutoa maamuzi ya mimi kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa na kujadiliwa.

"Nashukuru Jaji John Utamwa ametoa amri ya muda ya kuzuia kamati kuu ya chama kunijadili mpaka hapo Chadema watakapoweza kujibu hoja zilizotolewa na mwanasheria wangu Albert Msando.

"Leo tunarudi mahakamani kwa ajili ya kuendelea na kuweza kupokea majibu kutoka Chadema lakini kikao cha leo kamati kuu imezuiliwa na mahakama kujadili hoja yoyote inayonihusu,lakini pia mapingamizi yote mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu aliyokua ameyaweka dhidi ya mwanasheria wangu Jaji ameyatupilia mbali kwa hiyo kesi inaendelea.

Mahakamani Leo:
Mahakama kuu ilimaliza kusikiliza hoja za Chadema na  Zitto Kabwe leo, na kutoa taarifa ya kuwa itatoa uamuzi siku ya jumatatu.

Related

OTHER NEWS 5700572050738851598

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item