MSAADA UNAHITAJIKA KWA MTOTO GRACE
Grace ni mtoto wa miaka 14,mwenye uzito wa kilo 111.kwa zaidi ya miaka kumi Grace amekua akiishi maisha ya tabu,shida na maumivu makali...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/msaada-unahitajika-kwa-mtoto-grace.html
Grace ni mtoto wa miaka 14,mwenye uzito wa kilo 111.kwa zaidi ya miaka
kumi Grace amekua akiishi maisha ya tabu,shida na maumivu makali kimwili
na kisaikologia yaliyoletwa na uzito mkubwa /unene alionao.Alilazimika
kuacha shule akiwa darasa la nne baada yakushindwa kukabiliana na
unyanyapaa aliokutana nao katika maisha yake yakila siku,hasa shuleni na
barabarani.
Grace alizaliwa na afya nzuri na alifurahia maisha yake kama watoto
wengine ,Ingawa alianza kunenepa akiwa na miaka miwili unene wake ulikua
wakaaida. Hali ilibadilika alipofikisha miaka mitano ambapo alinenepa
sana,na unene wake haukua wakawaida kwani ulikua unene wakuvimba
mwili.Siku hadi siku Grace alizidi kuongezeka adi kufikia hivi alivyo
leo.
Hali hii ya unene iliambatana na matatizo mengine ya afya ,aliumwa sana
kichwa hasa sehemu ya paji la uso na wakati mwingine alihisi kichwa
kizito sana.Alipata shida kupumua na wakati mwingine alilazimika kulala
milango na madirisha yakiwa wazi.Miguu yake ilikua na maumivu wakati
wote
Grace Alipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu,na alipewa rufaa mwenda
hospitali ya mwimbili kwa ajili ya uchunguzi wa kina na matibabu mwaka
2010.Kwa bahati Mbaya Gharama za vipimo zilikua kubwa sana na wazazi
wake hawakua na uwezo wakulipa gharama hizo za shilingi laki nane.
Wazazi walijitahidi na kumpeleka katika hospitali zingine ambazo
waliweza kumudu garama zake,huko alifanyiwa uchunguzi mdogo,uchunguzi
huo ulibaini kua ,moyo wake umezungukwa na mafuta mengi,maini yake
yanasumu nyingi,mishipa yake ya damu inamafuta mengi na homoni zake pia
zinatatizo.Alipata matibabu ya dawa zenye asili ya chakula,ambazo
anatumia adi sasa.
Nilipoongea na Mtoto Grace aliniambia anatamani sana kurudi shule ilia
some nakutimiza ndoto yake yakua Daktari.Nilipomuuliza juu ya unyanyapaa
anaokabiliana kila siku,alisema “wananiita majina mabaya,bonge
nyanya,fupi nyundo,chabunene,alafu wengine wananifunua nguo
wananichungulia na kunicheka,sikunyingine wananimwagia michanga” Haya si
maisha yanayomsahili mtoto huyu.
Afya ya Grace si njema,bado anakabiliwa na changamoto zote zilizoelezwa
hapo juu. Anahitaji msaada wa matibabu ili kunusuru afya na maisha yake.
Tollyzkitchen kupitia kampeini yake ya PUNGUZA KILO MOJA ambayo ni
maalumu kwa ajili yakupunguza uzito na kukabiliana na magonjwa
yasababishwayo na unene na chakula ,tunafanya juhudi za kuchangisha
fedha ili kumsaidia mtoto huyu
Ukiwa kama mpenzi na mtumiaji wa jiko hili,naomba uungane nasi katika
kumsaidia mtoto huyu.Msaada wako wowote niwathamani sana kwake na kwetu
pia , uwezo wakumpa maisha anayoyatamani uko mikononi mwako .
Tumia namba hii kutuma msaada wako O713 755 741,ukituma Tigo pesa
itaandika majina:AKII CHAWACHI. Mpesa 0769 003 955 itaandika majina
SAUDA MBARUK
Tunatanguliza shukurani na Mungu akubariki,akuzidishie pale ulipotoa.
Tutatoa maendeleo ya Mtoto Grace kupitia www.tollyzkitchen.wordpress.com au www.tollyben.com kadri tutakavyokua tunafanikiwa katika kumsaidia.