NDESAMBURO AMKINGIA KIFUA LOWASA

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionekana kutikiswa na ushawishi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wa kutaka kutimiza saf...

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionekana kutikiswa na ushawishi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wa kutaka kutimiza safari yake ya kuwapatia Watanzania elimu bure, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), amejitokeza kumkingia kifua na kutaka asisakamwe.

Kauli ya Ndesamburo inakuja siku chache wakati kukiwa na harakati za wazi wazi kuwapinga wanaotajwa kutaka kuwania urais, zikishika kasi ndani ya CCM na kuonekana kuzigonganisha vichwa jumuiya zake.

Akitoa salamu zake za mwaka mpya jana, pamoja na kuzungumzia hali ya kisiasa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani, Ndesamburo alisema Lowassa hapaswi kushambuliwa kwa kigezo cha kutangaza safari yake.

“Wanaotangaza nia mbona wako wengi sana huko CCM na wala siyo Lowassa peke yake? Kwenye urais na hata huku chini kwenye ubunge na hata udiwani wako wengi tu wanafanya hivyo. Ina maana hao wanaomnyooshea kidole Lowassa hawa wengine hawawaoni?

“Hata huku kwenye vyama vyetu CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wapo wanaotuvuruga, lakini sasa hivi habari ya mjini ni Lowassa, Lowassa… kama kweli hatupendezwi na hali hiyo tuwanyooshee wote basi, kama hatuwezi wamwache aendeleze ndoto yake. The best way to predict the future is to invent it,” aliongeza Ndesamburo.

Alisema kwa mantiki hiyo, njia sahihi aliyoitumia Lowassa ya kutamka hadharani kusudio la kukamilisha majaliwa ya ndoto zake, ni namna alivyonyambulisha kile kinachoshabihi mawazo yake ya muda mrefu ya kuwatumikia Watanzania wenzake.

Ndesamburo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, alisema haijalishi kwamba yeye ni mpinzani wa CCM, lakini kumshambulia Lowassa peke yake, ingali kuna vinara wengine wanaokigawa chama chao si haki. 

“Haijalishi ya kuwa mimi ni mpinzani na najua hata wao wanalijua hilo kwamba  Ndesamburo ni nguli wa siasa za mageuzi ya kifikra katika taifa, nasema wawatizame na hao wengine wanaopita huko huko makanisani na misikitini kujitangaza kwa kisingizio cha kualikwa katika harambee,” alisema Ndesamburo.

Hata hivyo, Ndesamburo amewaomba Watanzania kuwachagua wagombea wa CHADEMA watakaopitishwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kwa kuwataka kuwakataa watu wanaotaka kuwachagulia viongozi wa kuwaongoza.

Katika siku za karibuni kumekuwa na matamko ya makatazo kutoka kwa viongozi wa CCM wakiwemo wale wa jumuiya, yakimtaka waziri huyo mstaafu kuacha kuendelea na kile kinachodaiwa kuwa kampeni za chini kwa chini za kuusaka urais.

Related

GHANA YAIBAMIZA ZAMBIA BAO 2 - 1

Ghana National Team Timu ya taifa ya Ghana imefanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Zambia bao 2 - 1 katika mchezo uliochezwa leo kuwania kushiriki kombe la dunia 2014

AJALI SHINYANGA

Zaidi ya watu 10 wamejeruhiwa vibaya baada ya gari waliyokuwa wakisafiria aina ya Noah waliyopanda kupinduka wakati ikijaribu kukwepa mkokoteni wilayani kahama leo. Dereva wa gari hilo amefariki d...

KATIBU MKUU MPYA WA UVCCM SIXTUS MAPUNDA AKABIDHIWA MADARAKA RASMI

KATIBU Mkuu mstaafu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Martine Shigela (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu mpya wa UVCCM, Sixtus Mapunda, faili wakati wa makabidhiano ya Ofisi, waliyofanya jana, Ma...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item