SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI DR WILLIAM MGIMWA KUTOKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha na Uchumi n...


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha na Uchumi na Mbunge wa Kalenga, Dkt. William Mgimwa ambaye amefariki akiwa kwenye matibabu Afrika Kusini.

Kwa masikitiko makubwa CHADEMA kinatuma salaam za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuondokewa na msaidizi wake wa karibu na mtumishi mwenzake serikalini.

Chama kinatoa salaam za dhati kwa familia ya marehemu Mgimwa kwa kuondokewa na baba na mpendwa wao, katika wakati ambao tunaamini walikuwa bado wakimhitaji sana kama moja ya nguzo za familia.

CHADEMA pia inatuma salaam za pole kwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na msiba huo wa kuondokewa na mmoja wa wanachama na wabunge wake.

Mwenyezi Mungu awapatie moyo wa subira wakati huu wa majonzi mazito ya kuondokewa na mpendwa wao, Dkt. Mgimwa.

Kurugenzi ya Habari

Related

CHADEMA YAPATA VIONGOZI WA KAMATI YA UTENDAJI, MNYIKA ASHIKA NAFASI ILIYOKUWA YA ZITO KABWE

   Kutoka kushoto ni Naibu Mkuu zanzibar Mh Salum Mwalimu Juma, Katikati ni Naibu katibu Mkuu Bara Mh John Mnyika na Kulia ni Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa.  Katibu Mkuu Dr Wilb...

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA KUFANYIKA DESEMBA 14

Imeandikwa na SIFA lubasi, Dodoma KIPENGA cha kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa, kinatarajiwa kupulizwa Novemba 30 mwaka huu na uchaguzi kufanyika Desemba 14 chini ya sheria zilizopo. ...

OSCAR HATIANI KWA KUUA BILA KUKUSUDIA

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya Akitoa uamuzi wake jaji Thokozile Masipaal alisema kuwa mwanariadha ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904746
item