TUNISIA YAPATA KATIBA MPYA
Bunge la Tunisia limeidhinisha katiba mpya,ikiwa ni ya kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Ben Ali, ya...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/tunisia-yapata-katiba-mpya.html
Bunge la Tunisia limeidhinisha katiba mpya,ikiwa ni
ya kwanza tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo
Ben Ali, yapata miaka mitatu iliopita.
Spika wa bunge hilo Mustapha Ben Jaafar ameitaja
katiba hiyo kama mojawapo ya makubaliano yaliyoafikiwa kwa mustakabali
mwema wa Tunisia.
Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa wanasiasa wana imani ya
kutuma ujumbe wa udhabiti na umoja kwa raia wa taifa hilo pamoja na
jamii ya kimataifa.
Wakati huohuo waziri mkuu nchini humo Mehdi Jomaa amesema ameunda serikali mpya.
Baraza la mawaziri linashirikisha wataalam na
watu wasioegemea upande wowote wa kisiasa, linatarajiwa kuongoza
serikali hadi uchaguzi mpya utakapofanyika.
Mehdi Jomaa alichaguliwa kama waziri mkuu mnamo
mwezi Disemba,baada ya serikali ilikuwa ikiongozwa na chama cha Ennahda
kukubali kujiuzulu kufuatia ongezeko la hali ya wasiwasi kati yake na
upinzani wenye misimamo wa kadri.