MNYIKA ASHINIKIZA KUPATA HATI YA MUUNGANO

  Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, John Mnyika, amesema atawasilisha hoja kuzuia shughuli za Bunge hilo kuendelea mpaka wajumbe wa...

 
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, John Mnyika, amesema atawasilisha hoja kuzuia shughuli za Bunge hilo kuendelea mpaka wajumbe watakapopatiwa hati halisi ya Muungano.

Mnyika, ambaye ni Mbunge wa Ubungo (Chadema) alitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya wajenzi na kusema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo kwa vile hadi sasa serikali haijatoa hati halisi ya Muungano ingawa ni muhimu wajumbe waione.

Alikumbusha kuwa baada ya kupitishwa kwa Kanuni za Bunge alitaka kanuni ziruhusu wajumbe wa Bunge wapewe nyaraka wanazotaka katika utendaji wao wa kazi.

“Niliposema hivyo, Mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka, alisemama na kupinga na akasema huyu Mnyika anataka kudai hati ya Muungano, naomba kanuni hiyo isiwepo”alisema.

Alisema Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alisimama na kusema kuwa hati hiyo ipo katika Sheria ya Muungano, lakini hakuna hati halisi wakati taarifa zingine zikisema kuwa ipo Umoja wa Mataifa.

“Hata hivyo baada ya kanuni hiyo kupita, nilimwandikia barua Katibu wa Bunge kuomba hati halisi ya muungano, lakini hadi sasa hivi ninavyozungumza sijapewa hati hiyo.“
Alisema msingi wa Rasimu ya Katiba ni Hati ya Muungano na kwamba umefika wakati sasa wajadili rasimu huku wakiwa na hati halisi.

“Hawa CCM wanadai uwazi kwa kukataa kura ya siri sasa inabidi waonyeshe mfano kwa kuweka wazi Hati ya Muungano, wakikomaa tutawashtaki kwa wananchi,” alisema.

Related

MSANII WA FILAMU ZA KISWAHILI TANZANIA LULU MICHAEL AKABIDHIWA TUZO YAKE YA ZIFF

LULU AKIPOKEA TUZO YA ZIFF YA MSANII BORA WA KIKE KATIKA FILAMU ZA KISWAHILI AKIONYESHA TUZO NA CHETI, KAZI NZURI BINTI KEEP IT UP!

MWENYEKITI WA CHADEMA MBOWE MBARONI

  MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya jeshi hilo, vyombo vya d...

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JOHN TENDWA KUKIFUTA CHADEMA

Msajjili wa vyama vya siasa, John Tendwa Hatimaye msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa ameibuka na kusema sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA. Kat...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item