NEC KUTANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA

JULIUS MALABA - MKURUGENZI WA UCHAGUZI Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema wiki hii itatangaza tarehe ya uchag...

JULIUS MALABA - MKURUGENZI WA UCHAGUZI


Dar es Salaam.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema wiki hii itatangaza tarehe ya uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga, lililopo wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wake, Dk William Mgimwa (CCM) kufariki dunia Januari Mosi mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Licha ya Kalenga, tume hiyo imesema uchaguzi mdogo pia utafanyika Jimbo la Chalinze baada ya Mbunge wake, Said Bwanamdogo (CCM)  kufariki dunia Januari  22 mwaka huu.
Akizungumza  ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Malaba alisema uchaguzi mdogo hauwezi kufanyika kama jimbo litakuwa wazi miezi 12 kabla ya Uchaguzi Mkuu.
“Wabunge hawa wamefariki dunia ikiwa imebaki miezi zaidi ya 12 kabla ya  Uchaguzi Mkuu na kuvunjwa kwa Bunge, hilo linamaanisha  chaguzi zitafanyika na wiki hii NEC itatangaza tarehe ya uchaguzi jwa Kalenga,” alisema Malaba.
Alifafanua kuwa mbunge anapofariki au vyovyote vile na jimbo kubaki wazi, NEC inatakiwa kutangaza tarehe ya uchaguzi ndani ya siku 90.
Malaba alisema daftari la kudumu la wapigakura litakalotumika ni lile lililotumika  Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Katika hatua nyingine, tume hiyo imeeleza kuwa ipo  hatua za mwisho za maandalizi ya kuboresha Daftari la Wapigakura.
“Nawahakikishia Watanzania ukifika wakati wa kupiga kura ya maoni kupata Katiba Mpya, Daftari la Wapigakura litakuwa limeshafanyiwa maboresho tupo hatua za mwisho na tutaeleza njia ambazo tutazitumia,” alisema Malaba.
Wakati NEC ikieleza hayo, Shirika la Vijana (TYVA) jana, limeitaka tume hiyo kuhakikisha vijana wote waliotimiza umri wa kupigakura wanaandikishwa katika daftari hilo.
Akizungumza Ofisi za Idara ya Habari (Maelezo), Mwenyekiti wa shirika hilo, Eric Ahimidiwe alisema kama maboresho hayo hayatafanyika, ni wazi kuwa vijana wengi watashindwa kupiga kura kupata Katiba Mpya.  “Kuna kundi kubwa la vijana wenye haki ya Kikatiba ya kupigakura, lakini hawajaandikishwa. Tunaiomba NEC iondoe ukimya na kutaja siku rasmi,” alisema.

MWANANCHI

Related

OTHER NEWS 5705871676301836981

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item