SABABU 18 ZINAZOKULAZIMU UPUNGUZE UZITO WAKO NA UOGOPE UNENE!

1. Unene unaongeza kiwango cha mafuta mwilini, ambayo huongeza uwezekano wa kupata kensa. 2. Unene unaongeza mafuta mwilini, ambayo hu...


1. Unene unaongeza kiwango cha mafuta mwilini, ambayo huongeza uwezekano wa kupata kensa.

2. Unene unaongeza mafuta mwilini, ambayo hufanya matibabu ya kensa yawe magumu zaidi.

3. Unene huongeza mafuta mwilini ambayo huushinikiza nu kuubana moyo.

4. Mtu mnene huwa mvivu kufanya mazoezi, suala ambalo humuongezea zaidi unene.

5. Mafuta mengi mwilini yana madhara kwa ubongo.

6. Unene huathiri hata tabia na miamala ya mtu.

7. Unene huongeza uzito katika mifupa na viunga vya mifupa (bone joints).

8. Unene husababishwa kibofu cha mkojo kibanwe suala linalopelekea matatizo mbalimbali ya mkojo.

9. Unene hupunguza uwezo wa mtu wa kijinsia.

10. Unene hupunguza uwezo wa kuzaa na hata kupelekea utasa na ugumba.

11. Unene hupelekea mwili upatwe kwa wepesi na magonjwa mbalimbali kama vile kisukari na presha.

12. Watu wanene wanapohudhuria mahospitali upimaji wao pia huwa wa matatizo.

13. Unene husababisha ujauzito kuwa wenye matitizo mengi.

14. Unene huathiri pia afya ya mtoto mchanga anayezaliwa.

15. Unene hufanya matibabu ya athma yawe magumu.

16. Unene hupelekea mtu asilale vizuri, na wakati mwingine mtu mnene anapolala hupanwa na pumzi suala linalompelekea kuamka mara kwa mara.

17. Unene humfanya mtu ashindwe kuwajibika vizuri kazini, na hata huweza kuathiri ajira yake.

18. Unene hufanya matumizi ya fedha yawe makubwa.







***Kama wewe ni mnene basi fanya jitihada upishane nao mbali***

Related

TUJUZANE 170515759000191844

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item