POLISI WAPONGEZWA KUPUNGUZA UHALIFU
Na Kija Elias, Moshi. S ERIKALI imelipongeza jeshi la polisi kwa kupunguza uhalifu wa kimataifa kufikia asilimia 1.1 tofauti na ilivy...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/polisi-wapongezwa-kupunguza-uhalifu.html
SERIKALI imelipongeza jeshi la polisi kwa
kupunguza uhalifu wa kimataifa kufikia asilimia 1.1 tofauti na ilivyokuwa mwaka
2012.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira
Ame Silima, alitoa pongezi hizo wakati akifungua mkutano mkuu maafisa wandamizi
wa jeshi la polisi, uliofanyika ukumbi wa chuo cha polisi Moshi.
Alisema
pamoja na Tanzania kutajwa kuongoza katika utekelezaji wa maazimio ya
mikakati ya kukabiliana na uhalifu wa kimataifa kati ya nchi wanachama wa
INTERPOL, kuongezeka kwa matukio ya uhalifu wa mitandao na uhalifu wa
kimataifa, ni moja ya changamoto zilizokuwa zikichafua sura ya taifa kimataifa.
Alisema
ushirikiano huo umesaidia
kuongeza imani kwa wananchi na
vyombo vya dola, imani ambayo haitokani na matumizi ya nguvu dhidi ya
wahalifu, bali limewezeshwa kwa kiasi
kikubwa kwa utekelezaji wa sheria ya
ugaidi ya mwaka 2002 na sheria ya fedha chafu ya mwaka 2006.
Hata hivyo, alisema kuna viashiria mbalimbali
vinavyoonesha kuongezeka kwa aina hizo za uhalifu na kutolea mfano wa ongezeko
la fedha chafu zinazopatikana na hutumika kutanua mitandao ya kihalifu kitaifa
na kimataifa.
Aidha aliongeza kuwa jeshi la polisi linapaswa kuongeza
ushirikiano ili kurudisha imani kwa wananchi na vyombo vya dola.
Kwa upande wake Mkuu wa jeshi la polisi nchini,
IGP Ernest Mangu,alisema jeshi lake
limejiandaa ipasavyo
kukabiliana na vurugu ambazo zinazojitokeza hususani nyakati za uchaguzi.
Alisema wakati nchi ikijiandaa na mchakato wa
upatikanaji wa katiba mpya suala la amani, usalama na utulivu ni moaj ya
vipaumbele ambavyo jeshi lake
imejipanga
kulishughulikia.