SEHEMU YA MAJENO YA CHUO CHA POLISI MOSHI CCP YAUNGUA MOTO, TAZAMA PICHA

  Wanafunzi wa chuo cha taaluma ya polisi Moshi wakijaribu kuzima moto na kuokoa mali zilizokuwa zikiungua katika moja ya stoo ya kuhi...

 Wanafunzi wa chuo cha taaluma ya polisi Moshi wakijaribu kuzima moto na kuokoa mali zilizokuwa zikiungua katika moja ya stoo ya kuhifadhia vitu mbalimbali zikiwemo nguo baada ya kuzuka kwa moto katika jengo hilo.









 Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akiwa na mkuu wa Chuo cha taaluma ya Polisi kamishana msaidizi wa polisi Matanga Mbushi wakishuhudia zoezi la uzimaji moto katika jengo hilo.

Picture Credit: Matukio Michuzi



MOTO uliozuka jana katika ghala la Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), umeteketeza vitu mbali mbali vilivyokuwa katika jengo hilo ambalo limekuwa likitumika kama stoo
ya kuhifadhi majora ya vitambaa pamoja na nguo za askari.
Moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika ulizuka majira ya saa 9:00
alasiri katika jengo hilo na kuzua mtafaruku mkubwa kwa askari na
wanafunzi wanaochukua mafunzo ya Polisi.
Mkuu wa chuo hicho, Kamishana Msaidizi wa Polisi, Matanga Mbushi, ambaye alikuwa eneo la tukio pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema ni mapema mno kuzungumzia moto huo ila ni
kweli umetokea.
“Nyote mmeshuhudia kweli moto umetekeza hili jengo na shughuli za
kujaribu kuuzima ndiyo zinaendelea lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia
chochote hadi kesho tutakuwa tumewaandalia taarifa rasmi,” alisema mkuu huyo wa chuo kwa kifupi.
Gazeti hili lilifanikiwa kufika eneo la tukio na kushuhudia wanafunzi wa
chuo hicho na maofisa wa serikali wakijaribu kuokoa vitu mbalimbali
kutoka katika jengo hilo ambalo baadhi ya vifaa hivyo viliteketea.
Vifaa vilivyoungua ni pamoja na  sare  za askari
ambazo zimekuwa zikitumiwa wakati wa sherehe za kuhitimu mafunzo ya
Polisi, viatu, kofia za Polisi, mikanda pamoja na magodoro yaliyokuwemo
katika jengo hilo.

Tanzania Daima

Related

OTHER NEWS 6554665678258419354

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item