KAMPENI ZA UCHAGUZI KALENGA, CCM YAZIDI KUCHANJA MBUGA
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa akisalimiana na vijana na wananchi kwa jumla baada ya kuwas...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/03/kampeni-za-uchaguzi-kalenga-ccm-yazidi.html
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa
akisalimiana na vijana na wananchi kwa jumla baada ya kuwasili jana
katika kijiji cha Elandutwa, katika jimbo hilo, Iringa Vijijini kwa
ajili ya mkutano wake wa kampeni
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akimnadi Mgimwa katika Kijiji cha Elandutwa, Iringa Vijijini.
Wananchi
wa Kijiji cha Elandutwa, Iringa Vijijini wakionyoosha mikono kuahidi
kumpa kura zote Mgomwa katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wakati wa
mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jana.
Mgimwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kijiji cha wafugaji cha Elandutwa, Iringa Vijijini
Kinamama wa Elandutwa wakimshangilia mgombea wa CCM katika mkutano wa kampeni
Mtoto aliyebebwa mabegani (kushoto) akishangilia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Itwaga.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Irimga, Jesca Msambatavangu (wanne kushoto) akiongoza
warm-up ya aina yake kabla ya kuanza mkutano wa kampeni katika kijiji
cha Elandutwa
Kada wa CCM kutoka Makao Makuu ya UVCCM, Mtela Mwamopamba,akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Itwaga
"Jamani
nchi yetu ya Tanzania ilipata Uhuru kwa kumwaga damu? Sasa tazama rangi
za bendera ya chama hiki cha wenzetu. Rangi hii nyekundu inaashiria
nini kwenye bendera yao?" Mwenyekiti wa CCm mkoa wa Iringa, Jesca
Msambatavangu, alisema hayo wakati akionyesha kofia yenye mpangilio wa
rangi za bendera ya Chadema, kwenye mkutano wa kampeni za CCM
uliofanyika kijiji cha Udumka,jana.
"Nitatumia
ilani hii ya CCM kuhakikisha kero zinazowakabili wananchi katika jimbo
la Kalenga zinapata ufumbuzi", anasema Mgombea wa CCM katika uchaguzi
mdogo wa jimbo hilo, Godfrey Mgimwa wakati akiomba kura kwenye mkutano
wake wa kampeni kijiji cha Itwaga.
Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akihutubia mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Elandutwa
Makamanda
wa ukweli wa CCM, wakiwa wamepozi kiambazani mwa nyumba ya mwanakijiji
katika kijiji cha Elandutwa, wakati wakisubiri kupanda jukwaani mmoja
baada ya mwingine, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji
hicho. Baadhi yao kutoka kushoto ni Mtela Mwampamba, Katibu wa CCM mkoa
wa Iringa Salum Mtenga na Akwilombe
"Huyu
si Kijana Mwenzenu, tena Msomi? sasa wakati wenu ni huu kumchagua",
Katibu wa Jumuia ya Wazazi ya CCM akiwaambia Vijana wakati wa mkutano
wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Udumka
Mashabiki mbalimbali wa CCM wakiagana na mgombea wa chama hicho, Mgimwa baada ya mkutano wa kampeni wa Udumka.