BUNGE MAALUM LAANZA KUSIKILIZA TAARIFA ZA KAMATI
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta amesema mjadala kuhusu taarifa za Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Katib...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/04/bunge-maalum-laanza-kusikiliza-taarifa.html
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,
Samuel Sitta amesema mjadala kuhusu taarifa za Sura ya Kwanza na ya
Sita za Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
unatarajia kuanza wiki ijayo katika Bunge hilo mara baada ya kumaliza
kupokea taarifa za Kamati.
Sitta alisema hayo katika ukumbi wa
Bunge hilo mjini Dodoma baada baadhi ya wajumbe kumwomba kuchangia
mjadala wakati ripoti hizo zikiendelea kuwasilishwa.
Alisema mdajala wa kuchangia sura hizo
utaanza mara baada ya Kamati 12 za Bunge Maalum la Katiba
kuwasilisha taarifa zao za Sura ya Kwanza na ya Sita kuhusu Rasimu
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge hilo.
Aliongeza kuwa kwa kujibu wa Kanuni ya
namba 33(6) ambayo inasema baada ya hoja za taarifa za Kamati Namba
Moja hadi Namba Kumi na Mbili kutolewa katika Bunge Maalum na
Mwenyekiti kuelekeza hoja hizo zijadiliwe , mjadala kuhusu taarifa hizo
utaanza.
Mwenyekiti huyo aliwataka baadhi ya
wajumbe hao kusubiri mpaka uwasilishaji wa taarifa hizo utakapokamilika
ndio watapata nafasi ya kuchangia kwa muda mrefu na kuwezesha wajumbe
wengi kupata nafasi hiyo.
(Picha na Bunge Maalum la Katiba)