Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa? Soma Hapa

  Baadhi ya wanawake wanakunywa maji ya Kondo la Nyuma saa chache baada ya kujifungua Hugeuka kuwa uchafu pindi mama anapojifungua...

Baadhi ya wanawake wanakunywa maji ya Kondo la Nyuma saa chache baada ya kujifungua

Hugeuka kuwa uchafu pindi mama anapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya wanawake wanaamua kula Kondo la nyuma au Placenta ikiwa mbichi ?
Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni.

Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri kuitupa.

Njia za kula Kondo la Nyuma
•    Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vile
•    Inaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembe
•    Kupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama

Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata madini muhimu wakati anapoendelea kupata nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma.

'Mama ale Kondo la Nyuma?'
Baadhi ya wanawake husaga kondo la nyuma na kunywa maji yake saa chache tu baada ya kujifungua, baadhi wanaihifadhi na kutengeza tembe ambazo wanameza na wengine wanaikata vipande vipande kwa kuweka chini ya ndimi zao.

Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa ya mama kuongezeka.
Kampuni moja nchini Uingereza inayotengeza biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo la Nyuma, hulipisha watu kati ya pauni 150 au dola elfu kumi na saba kwa kila tembe na chini ya dola hamsini kwa maji ya kondo hilo linaposagwa.

Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi kutupwa tu.
Lakini kampuni hiyo inakumbwa na kesi mahakamani ambayo huenda ikaisababisha kufungwa.
Kampuni hiyo ilishitakiwa na wataalamu wanaohofia kuwa bidhaa hizo zinaweza kuwa na Bakteria ambayo inaweza kusababisha athari za kiafya kwa wanaotumia bidhaa zinazotokana na kondo la nyuma.

Charlie Poulter, kutoka mtaa wa Reading, anaamini kuwa alipokunywa maji ya kondo la Nyuma pindi baada ya kujifungua ilimwezesha kupata nguvu.
"nilikunywa harakaharaka, kwa sababu sikutaka kutafakari kuhusu harufu na ladha yake, alisema Charlie''
"nilikuwa nimejifungua na nilihisi kuishiwa na nguvu sana na pia kwa kiasi kidogo nilijidharamau. Kwa hivyo nilihisi kuwa ikiwa nitakunywa maji hayo ingenisaidia kupata nguvu na kupona haraka,'' alisema mama Charlie.

 Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda

'Kondo la Nyuma ni nini?'
Hii huwa ni kiongo cha mwili ambacho huwa kimeshikana na nyumba ya mtoto pamoja na kitovu.
Kiungo hicho hubeba hewa ya Oxygen na madini kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Pia husafirisha uchafu kutoka kwa mtoto hupitia kwa kiungo hicho hadi kwa mama.

Baada ya mtoto kuzaliwa kiungo hicho hutoka mwilini mwa mama anaposukuma mtoto au hutolewa na madaktari mama anapofanyiwa upasuaji.
Binadamu kwa kawaida hajulikani kwa kula sehemu hiyo ya uzazi. Ni kawaida kwa baadhi ya wanyama wa baharini na wanyama wengine wa kufugwa. Lakini kwa mwanmadamu , bila shaka ni jambo geni.

Nchini China baadhi ya madaktari wa kienyeji hutumia sehemu hiyo ya mwili kutengeza dawa za kienyeji lakini utamaduni huu wa watu kula Kondo la Nyuma umeanza tu kusikika katika mataifa ya magharibi.

'Je wanasayansi wanasemaje?'
Hadi leo hakuna utafiti wowote kuhusu wanawake wanaokula Kondo la Nyuma.

Chanzo: BBC SWAHILI.

Related

TUJUZANE 815656126095007393

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item