UPOTOSHWAJI WA TAARIFA YA HALI MBAYA YA HEWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI        MAMLAKA YA HALI YA HEWA Simu: +255 22 2460706-8 Telefax: +2...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
       MAMLAKA YA HALI YA HEWA



Simu: +255 22 2460706-8
Telefax: +255 22 2460735, 2460700                                                                                                 S.L.P.   3056,
Barua pepe: met@meteo.go.tz                                                                                                          DAR  ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
                                                                                                                           05/05/2014
                             TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH : UPOTOSHWAJI WA TAHADHARI YA HALI YA HEWA KUHUSIANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini inapenda kukanusha kuhusiana na taarifa ya ujumbe mfupi wa simu na katika mitandao ya kijamii wenye maneno yafuatayo : ‘TMA warning heavy rains of strong easterly winds 100km an hour expected to hit Dar coast from Somalia, Heavy rains 120mm above sea level expected today and tommorrow. People must avoid Sea and areas near to Sea should be alert cautioned. Tanzania Meteorological Agency  www.tma.gov.tz’   
Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli  na ina  lengo la kupotosha umma na wala haijatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ina kuwakumbusha wananchi wote kuendelea kufuatilia taarifa zetu kupitia vyanzo husika vya Mamlaka vikiwemo utabiri wa kila siku utolewao kupitia radio, televisheni na tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz).
Taarifa sahihi za mwenendo wa mvua na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinatolewa  na zinapatikana kupitia njia rasmi za utoaji taarifa maalum za kiofisi (official weather statement).
Hivyo taarifa kuhusiana na mvua zinazoendelea imekuwa ikitolewa katika utabiri wa kila siku kupitia vyombo vya habari, mtandao wa kijamii  wa Mamlaka na tovuti ya Mamlaka.
Tunawatakia shughuli njema katika ujenzi wa Taifa letu.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Related

JERMAIN DEFOE ATUA SUNDERLAND

 Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza Jermain Colin Defoe amejiunga na timu ya Sunderland. Defoe mwenye miaka 32 aliekua akiichezea timu ya Toronto FC ya nchi Marekani ...

AMAVUMBI KUTUA MWANZA JANUARI 21

KIKOSI CHA AMAVUMBI Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) itawasili Mwanza, Tanzania Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars Maboresho itakayochezwa ...

MDEE: JIANDIKISHENI KATIKA DAFTARI KUEPUSHA WIZI WA KURA

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee Wakati miezi tisa ikiwa imebaki Tanzania kufanya uchaguzi mkuu, Watanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904769
item