WANANCHI WAJUMUIKA KWENYE MAZISHI YA SHEIKH ILUNGA JIJINI DAR ES SALAAM JANA
Maalim Seif akishiriki katika mazishi ya Sheikh wa Ilunga Shekh.Hassan Kapungu yaliofanyika katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni D...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/05/wananchi-wajumuika-kwenye-mazishi-ya.html
Maalim Seif
akishiriki katika mazishi ya Sheikh wa Ilunga Shekh.Hassan Kapungu
yaliofanyika katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Dar es Salaam.
akijumuika na Wanancjiji Dar-es-Salaam.
Wananchi wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga Hasaan Kapungu
katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam.
Wananchi wakishiriki katika mazishi ya
Shekh Ilunga Hasaan Kapungu katika makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu
jijini Dar-es-Salaam. (Picha na Salmin Said OMKR)
Na Hassan Hamad (OMKR).
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewaongoza maelfu ya waislamu katika mazishi ya sheikh maarufu wa Mkoa wa Mwanza na mwanaharakati wa dini ya Kiislamu marehemu sheikh Ilunga Hassan Kapungu.
Sheikh Ilunga amefariki dunia mjini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Katika uhai wake
sheikh Ilunga Kapungu alikuwa mwanaharakati ambaye mara nyingi alikuwa
akiendesha mihadhara ya wazi ya dini ya Kiislamu, ambapo mwishoni mwa
mwaka 2013 alikamatwa kwa tuhuma za uchochezi mkoani Tabora na baadaye
kuachiwa huru.
Kwa mujibu wa
taarifa za kimtandao, kabla ya kukamatwa kwake na kuachiwa huru Disemba
mwaka 2013, marehemu sheikh Ilunga alikwenda nchini India kwa matibabu
baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo pamoja na sukari.
Akizungumza katika
mazishi hayo sheikh Basaleh wa Dar es Salaam, amesema marehemu sheikh
Ilunga alikuwa mwanaharakati imara na ni mfano mzuri wa kuigwa katika
harakati za dini ya Kiislamu.
Mazishi yake
yameweka historia baada ya maelfu ya waislamu kujitokeza kushiriki kwao,
hali iliyopelekea mchanga wa kaburi lake kufukiwa kwa mikono badala ya
kutumia mapauro na majembe kama ilivyozoeleka.
Masheikh kutoka Mikoa mbali mbali ya Tanzania wameshiriki mazishi hayo akiwemo sheikh Kishki.