AJALI YAUA WATU 6 MKOANI MBEYA
Basi la Ndenjela lililogongwa na kupinduka eneo la Nanyala Mbeya Adelina Malipesa moja wa majeruhi katika ajali hiyo ambae pia ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/ajali-yaua-watu-6-mkoani-mbeya.html
Basi la Ndenjela lililogongwa na kupinduka eneo la Nanyala Mbeya
Adelina Malipesa moja wa majeruhi katika ajali hiyo ambae pia aliporwa pesa na vibaka waliojifanya wasamaria wema
Emmy Charles moja kati ya majeruhi akiwa katika hospitali ya Ifisi
Lori lililosababisha ajali likiwa limepinduka upande mwingine baada ya kuligonga basi la Ndenjela
MBEYA.
Watu Sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni Ndejela Express
lenye namba za usajili T 257 CMP aina ya TATA likiendeshwa na Dereva wa kike
Vailet Mbinda(31) mkazi wa Sokomatola
kugongwa kwa nyuma na roli la mizigo kisha kupinduka Kijiji cha Nanyala
Kata ya Nanyala wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.
Ajali hiyo
imetokea majira ya saa tisa alasiri barabara ya Tunduma/Mbeya ambapo roli
lenye namba T 369 AWM aina ya
SCANIA likendeshwa na Dereva asiyefahamika likiwa katika mwendo kasi liligonga
basi kwa nyuma kisha magari yote mawili kupinduka.
Miongoni
mwa
waliofariki ni Zainabu Mohammed aliyekuwa kondakta wa basi hilo
linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Sumbawanga kila siku, Padri
Barnaba Lwemba 35 wa Morogoro Emmanuel Philipo 1 wa Sumbawanga Neusta
Jacob Mafuga 27 wa iringa Milika Mbingamno 38
Mwanaume mmoja
na Mwanamke mmoja walifariki eneo la tukio na wawili walifariki wakati wakipatiwa matibabu katika
Hospitali ya Rufaa Mbeya wakati majeruhi wanane walikimbizwa Rufaa kutokana na
hali zao kuwa mbaya.
Kamanda wa
Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba
chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na juhudi za kumtafuta Dereva wa roli
zinaendelea.
Aidha
amewataka wamiliki wa magari na madereva kuyafanyia matengenezo na ukaguzi wa
mara kwa mara magari yao ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
Muuguzi Mkuu
wa Hospitali Teule ya Wilaya ya MbeyaIfisi, Sikitu Mbilinyi amewataja majeruhi
kuwa ni Dereva amewataja majeruhi kuwa ni Fred,Maiko Malema(16),Justin
Komb(24),Amir Ramadhan(26),Nausi Bakari(28),Jackson Kambo(19),Anoria Ndezi(13)
na Lucy Edson(17).
Mbilinyi
amewataja wengine kuwa ni Groly Paul(27),Moyo Safi(1),Rahma Peter(3),MaryKitine(57),Mariam,Karen Naiman,Mecy,Adelina Malipesa(52),Suzana Athas(35),Adelina
Essau(28),Frola Essau(64) na Emmy Charles(21).
Wengine
waliolazwa ni pamoja na Diana Jumbe(19),Esther Seleman(21),Paul
Mayeta(45)ambaye ni Dereva msaidizi,Bahati Julius(33) na Joeph Komba(34).
Kwa mujibu
wa Muuguzi Mkuu hali za majeruhi zinaendelea vizuri na wanafanya kilajitihada
za kuokoa maisha yao na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kuchangia damu kwani
Hospitali hiyo ina uhitaji mkubwa kutokana na kuwa karibu ya barabara kuu na
ajali zinazojitokeza mara kwa mara ingawa hupatiwa damu kutoka Benki ya Damu
salama.
Hata hivyo
baadhi ya abiria wamelalamikia kitendo cha baadhi ya wananchi wa Nanyala badala
ya kusaidia majeruhi walikuwa wakiwapora mizigo,simu na fedha pia waliokuwa na
vito vya thamani kama heleni.
Jackson
Kambo ambaye ni mmoja wa wahudumu wa basi hilo amesema kuwa kama ushirikanowa
wananchi hao wangeutoa mapema kondkta wake aingefariki lakini badala ya
kusaidia walikuwa wanan’gan’gania mkoba wa fedha hadi walipofanikiwa kuchukua
fedha ndipo walianza kutoa msaada marehemu akiwa amelaliwa mkono na basi.
Kambo
amesema kama si juhudi binafsi Dereva wa basi angepoteza maisha kutokana na
kubanwa na mkanda hivyo kulazimika kuukata na kuanza kusaidia kuokoa abiria
wengine.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu