BAADA YA TIMU YA TAIFA YA ITALIA KUTOLEWA KOMBE LA DUNIA, CESARE PRANDELLI AJIUZULU
Cesare Prandelli Kocha Cesare Prandelli ametangaza kubwaga manyanga baada ya Azzuri kutolewa kwenye mashindano ya Kombe la dunia yan...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/baada-ya-timu-ya-taifa-ya-italia.html
Cesare Prandelli
Kocha Cesare Prandelli ametangaza kubwaga manyanga baada ya Azzuri kutolewa kwenye mashindano ya Kombe la dunia yanayoendelea nchini Brazil.
Italia
iliondolewa baada ya kufungwa kwa goli 1-0 na Uruguay katika mechi ya
mwisho ya makundi. Baada ya mchezo Prandelli akiwa kwenye mkutano wa
waandishi wa habari alitangaza kujiuzulu kuifundisha timu
hiyo.“Nilichagua mfumo fulani wa ukufunzi na ndio sababu ninajiuzulu,
kwa sababu haukufanya kazi,” alisema.
Aliongezea:
“Kuna jambo ambalo limebadilika tangu nilipotia saini mkataba mpya.
Sijui kwanini lakini sina haja ya kutafuta sababu .”
Kocha
huyo aliingia mkataba mpya na Italy Mei mwaka huu ambao ungemfanya
aendelee kuifundisha Italy hadi baada ya mashindano ya kuwania ubingwa
wa Euro ya mwaka wa 2016.
Prandeli amechukua hatua hii baada ya kujiuzulu kwa rais wa shirikisho la kandanda la Italia Giancarlo Abete.
“Nilizungumza
na rais wa shirikisho na naibu wa rais Demetrio Albertini na nikawapa
barua ya kujiuzulu kwangu. Ni jambo lisilobadilika,”
Wakati huo huo FIFA imeanza kuchunguza tukio la mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez la tuhuma za kumng'ata begani beki wa Italia Giorgio Chiellini.