UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, kufuatiataarif ailiyowasilishwa hapa
Bungeni na Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda
naBiashara, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lakoTukufu likubali kupokea,
kujadili na kupitishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya
Fedhakwa mwaka 2014/15.
- Mheshimiwa Spika, awali ya yote napendakumshukuru Mwenyezi Mungu
mwingi wa rehema kwakuniwezesha kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara
yamwaka 2014/15. Aidha, natoa shukrani zangu za dhatikwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuniteua
kuwa Waziriwa Fedha. Ninaahidi kwamba nitatekeleza jukumu hilikwa weledi
na uadilifu.
Vile vile, nawapongeza Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mhe.
AdamKighoma Ali Malima (Mb) kwa kuteuliwa kuwa NaibuMawaziri wa Wizara
ya Fedha. Kadhalika, namshukurupia aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha Mhe.
JanethZebedayo Mbene (Mb) kwa utendaji kazi wake mahiri natunamuombea
Mwenyezi Mungu ampe nguvu na afyanjema katika kazi zake mpya Wizara ya
Viwanda naBiashara. Nichukue pia fursa hii kumpongeza Bw.1Rished M. Bade
kwa kuteuliwa kuwa Kamishna Mkuuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
- Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewemwenyewe, Naibu Spika
pamoja na Wenyeviti wa Bungekwa kuongoza vyema majadiliano ya Bunge la
Bajeti.
-
Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hiikuishukuru kwa namna ya
pekee Kamati ya Kudumuya Uchumi, Viwanda na Biashara chini ya
Mwenyekitiwake Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mbunge wa Kisesa)na Makamu
wake Mhe. Dunstan Luka Kitandula(Mbunge wa Mkinga) kwa maoni, ushauri
namapendekezo waliyoyatoa kwa Wizara wakati wakuchambua mapendekezo ya
Bajeti ya Wizara ya Fedha.Aidha, nachukua nafasi hii kumshukuru
Mwenyekitiwa Kamati ya Kudumu ya Bajeti Mhe. Andrew JohnChenge (Mbunge
wa Bariadi Magharibi) pamoja naKamati nzima kwa ushauri wao.
Katika uandaaji wahotuba hii, Wizara imezingatia ushauri na
mapendekezoya Kamati hizo pamoja na ushauri na maoni ya hojambalimbali
zilizotolewa wakati wa mjadala wa bajeti yaWizara kwa mwaka 2013/14.
- Mheshimiwa Spika, kama unavyofahamu, Wizarailipata pigo kwa
kuondokewa na kiongozi wetu mkuuMarehemuDkt.WilliamAugusta
oMgimwa.Tunawashukuru Viongozi wa Serikali, WaheshimiwaWabunge,
Washirika wa Maendeleo, Taasisi mbalimbalipamoja na wananchi kwa
ushirikiano waliotupa kipindichote cha msiba. Tumeendelea kuenzi misingi
imaraaliyotujengea marehemu katika kutekeleza majukumuya Wizara. Aidha,
tunapenda kutoa pole kwa ndugu na2jamaa kufuatia kifo cha aliyekuwa
Mbunge wa ChalinzeMarehemu Saidi Ramadhani Bwanamdogo. MwenyeziMungu
azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.Amina.
Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza, Mhe.Yusuf Salim Hussein Mbunge
wa Chambani, Mhe.Godfrey William Mgimwa (Mbunge wa Kalenga) na
Mhe.Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mbunge wa Chalinze) kwakuchaguliwa kwao.
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekeenapenda kutoa pongezi zangu za
dhati kwa Mhe.Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa
Tanzania na
Mbunge wa MpandaMashariki kwa hotuba yake nzuri ambayo
imetoamwelekeo wa shughuli za Serikali kwa mwaka 2014/15.
Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu nitaanzakuelezea mapitio ya
utekelezaji wa mipango ya Wizarakatika mwaka 2013/14. Nitaelezea pia
mikakatimbalimbali ambayo Wizara imeweka kwa mwaka2014/15 ili kuendelea
kuboresha utekelezaji wamajukumu yake ya msingi yakiwemo: usimamizi
waBajeti ya Serikali; ukusanyaji mapato ya Serikali;usimamizi wa misaada
na mikopo; ulipaji wa Deni laTaifa; usimamizi wa matumizi ya fedha za
umma;usimamizi na udhibiti wa ununuzi wa umma;usimamizi wa utekelezaji
wa MKUKUTA; na usimamiziwa mashirika na taasisi za umma.
Mheshimiwa Spika, mwisho nitawasilisha bajetiya mwaka 2014/15 kwa
mafungu saba ya wizara yafedha ambayo ni fungu 7, 10, 13, 21, 22, 23 na
fungu50 pamoja na fungu 45 la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za
Serikali.
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETIYA WIZARA KWA MWAKA 2013/14 NA MALENGO YA MWAKA 2014/15
- Mheshimiwa Spika, uandaaji, utekelezaji nausimamizi wa Mpango na
Bajeti ya Wizara umezingatiamalengo ya Mpango Mkakati wa Wizara wa
mwaka2012/13 – 2016/17 ambao utaiwezesha Wizara kufikiamalengo ya Dira
ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025;Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano
2011/12 -2015/16; Mkakati wa Kukuza Uchumi na KupunguzaUmaskini Tanzania
(MKUKUTA II); Malengo yaMaendeleo ya Milenia 2015; Mkakati wa Pamoja
waMisaada Tanzania (MPAMITA) pamoja na Programu yaMaboresho ya Usimamizi
wa Fedha za Umma – PFMRP.Aidha, Mpango na Bajeti ulizingatia Ilani ya
Uchaguziya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 pamoja naMfumo wa Tekeleza
Sasa kwa Matokeo Makubwa (BigResults Now – BRN).
Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2013/14,Wizara ilipanga kutekeleza
yafuatayo: kuongeza mapatoya ndani kufikia uwiano wa Pato la Taifa wa
asilimia20.9 kwa mwaka 2013/14 ikilinganishwa na asilimia17.7 kwa mwaka
2012/13; kukamilisha Ripoti za Utafitiwa Mfumo Bora wa Kodi wa Serikali
ya Jamhuri ya4Muungano wa Tanzania; kuandaa na kusimamiautekelezaji wa
bajeti ya Serikali; kusimamia utekelezajiwa MKUKUTA-II; kufanya ukaguzi
wa miradi yamaendeleo na kutoa ushauri wa kitaalamu kwawatekelezaji wa
miradi hiyo; kukamilisha Sera ya Maliya Umma; kufanya tathmini
yausimamizi nautekelezaji wa malipo ya mishahara ya watumishi waumma;
kusimamia utekelezaji wa mipango kazi yaukaguzi na uzingatiwaji wa
miongozo ya ukaguzi katikaWizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za
Serikali, naMamlaka ya Serikali za Mitaa; kuratibu na
kusimamiaupatikanaji wa misaada na mikopo nafuu kutoka NchiWahisani,
Mashirika na Asasi za Fedha za Kimataifa;kuidhinisha miradi ya Ubia kati
ya Sekta ya Umma naBinafsi (PPP); na kukamilisha Sera ya Taifa ya
Ununuziwa Umma.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Wizarapia ilipanga
kukamilisha miradi ya MCA-T na kukabidhimiradi iliyokamilika kwa taasisi
husika; kusimamiautekelezaji wa Mpango Mkakati wa Programu yaMaboresho
ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu yanne (PFMRP IV); kufanya uhakiki wa
Wastaafu waliopokatika Daftari la Pensheni la Hazina; kuunganishaHazina
Ndogo na Sekretarieti za Mikoa 24 katika mfumowa malipo kwa njia ya
elektroniki kupitia Benki Kuu yaTanzania (Tanzania Inter- Bank
Settlement System -TISS); kuimarisha utendaji kazi wa Ofisi ya Msajili
waHazina; na kuandaa na kuhuisha kanuni na miongozoya utekelezaji wa
Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramuna Ufadhili wa Ugaidi.5Mfumo wa
Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,kupitia Tekeleza Sasa kwa
Matokeo Makubwa, Wizaraya Fedha katika maabara ya utafutaji wa
rasilimalifedha iliwekewa malengo yafuatayo: kuongeza mapatomapya ya
kodi ya shilingi trilioni 1.16; kuongezamapato mapya yasiyo ya kodi ya
shilingi bilioni 96.7;kudhibiti matumizi; na kutafuta fedha za
utekelezaji wamiradi ya Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa katikasekta
zinazotekeleza miradi hiyo.
Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili 2014,ukusanyaji wa mapato kutoka
vyanzo vilivyoibuliwachini ya BRN umefikia shilingi bilioni 338 sawa
naasilimia 29.14 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni1.16. Matokeo
yasiyoridhisha yalisababishwa na baadhiya mapendekezo ya BRN
kutokutekelezwa katikamwaka 2013/14. Mapendekezo hayo ni
kubadilishamfumo wa ushuru wa bidhaa zisizo za petroli kutokaspecific
kwenda advalorem (makisio shilingi bilioni 386)na kuanzisha kodi ya zuio
ya asilimia tano kwenyebidhaa zinazotoka nje ya nchi (makisio shilingi
bilioni225.6). Kwa vile ukusanyaji wa mapato ndio msingi wakufanikiwa
kwa BRN, Serikali inachambua vyanzombadala vya kufidia mapato haya ili
kuhakikisha lengokuu la kuongeza mapato kwa shilingi trilioni
3.48linafikiwa ifikapo mwaka 2015/16.6Mwenendo wa Uchumi.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Benki Kuu
iliendelea na jukumu lakuandaa, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa
seraya fedha inayolenga kuwa na kiwango kidogo chamfumuko wa bei kwa
ajili ya kuhakikisha gharama zamaisha haziongezeki. Kutokana na juhudi
hizi,mfumuko wa bei umeshuka kutoka wastani wa asilimia16 mwaka 2012
hadi kufikia wastani wa asilimia 7.9mwaka 2013. Katika kipindi hiki
uchumi umeendeleakuimarika huku ukuaji halisi wa Pato la
Taifaukiongezeka kwa asilimia 7.0 katika kipindi cha mwaka2013
ikilinganishwa na asilimia 6.9 katika mwaka2012. Shughuli za kiuchumi
zilizokua kwa kiasikikubwa ni pamoja na mawasiliano asilimia 22.8,huduma
za kifedha asilimia 12.2, ujenzi asilimia 8.6, nauuzaji bidhaa wa jumla
na rejareja asilimia 8.3. Katikamwaka 2014/15, Wizara kupitia Benki Kuu
itaendeleakushirikiana na wadau wote katika kuhakikishakwamba lengo la
msingi la utulivu wa bei na ukuaji wauchumi linadumishwa.Uandaaji na
Usimamizi wa Utekelezaji wa Bajeti yaSerikali
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara imeratibu uandaaji wa
Mwongozo wa Mpango naBajeti kwa kipindi cha 2014/15 – 2016/17 kwa
Wizara,Idara zinazojitegemea, Mikoa na Mamlaka za Serikali zaMitaa na
kusambaza kwa wadau mwezi Desemba kama7ilivyopangwa. Aidha, Wizara
imeandaa na kuchapishavitabu vya bajeti ya Serikali vya mwaka
2014/15(Volume I, II, III na IV) kama vilivyowasilishwa Bungenikwa ajili
ya mjadala wa Bunge la Bajeti la mwaka2014/15 unaoendelea; kitabu cha
tafsiri rahisi ya bajetiya Serikali (Citizen’s Budget) kwa mwaka
2013/14; naKitabu cha Budget Background and Medium TermFramework –
2013/14 – 2015/16.
Mheshimiwa Spika, Serikali inakusudia kuanzakutumia mfumo wa Programu
katika uandaaji,uidhinishaji na utekelezaji wa Bajeti. Mfumo
huuutasaidia Serikali kugawa rasilimali kwa kuzingatiamatokeo na kuweka
viashiria vya kufikia malengo.Katika hatua za awali za maandalizi ya
utekelezaji wamfumo huu katika mwaka 2013/14, Wizara ilitengafedha kwa
ajili ya mafunzo kwa wataalam wa Wizaranane za mfano. Maandalizi haya ya
kimkakati nakimfumo yataendelea katika mwaka 2014/15.
Wizarazilizotengwa kwa majaribio na ambazo tayarizimefanyiwa mafunzo ni
Wizara ya Maji, Wizara yaUjenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Elimu
naMafunzo ya Ufundi, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wizara ya Kilimo,
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsiana Watoto na Wizara ya Fedha.
Wizara hizi kwa sasazinaendelea na zoezi la kuandaa programu na
viashiriavya kupima utekelezaji kabla ya mfumo kuanzakutumika.
Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu kikao kazicha wataalamu wa wizara,
mikoa na halmashaurikuhusu mfumo wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji
wataarifa za utekelezaji wa Bajeti. Katika kipindi hicho,8Wizara pia
ilifanya kikao kazi kilichohusisha washirikikutoka wizara, idara za
Serikali zinazojitegemea, mikoana Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
kwa lengo lakutathmini uandaaji na uwasilishwaji wa Bajeti yaSerikali
kwa mwaka 2012/13 na kufanya mkutano wamwaka wa wadau ambao ulijumuisha
Washirika waMaendeleo kwa lengo la kutathmini utekelezaji waBajeti ya
Serikali.
Mheshimiwa Spika, katika kusimamia nakudhibiti utekelezaji wa bajeti
ya Serikali ikiwemokufuatilia matumizi ya fedha za umma, Wizara
ilifanyaufuatiliaji na ukaguzi wa matumizi ya fedha zilizotolewakwa
ajili ya maendeleo kwa miradi ya ASDP na DASIPikihusisha wizara nne,
mikoa sita na halmashauri 33.Aidha, ufuatiliaji na ukaguzi ulifanyika
kwa mapato namatumizi ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa yaChakula
(NFRA) na kwa fedha zilizotolewa kuhudumiavituo 16 vya Makazi ya Wazee
katika mikoa 14 nchini.
Mheshimiwa Spika, katika ukaguzi huo, Wizarailibaini kuwapo kwa
upungufu na changamoto katikamaeneo haya ikiwa ni pamoja na: fedha
kutowafikiawalengwa kwa wakati kama ilivyopangwa; udhaifukwenye udhibiti
wa ndani wa matumizi na hivyokusababisha kuwapo kwa huduma duni; na
miradikutokamilika kwa wakati na kuwepo kwa bakaa yafedha za maendeleo.
Aidha, zimekuwepo changamoto zakubadilika mara kwa mara bei ya kununulia
nafaka nagharama za usafirishaji, hivyo kuathiri malengoyaliyopangwa
ikiwemo kusababisha madeni. Wizaraimewasiliana na wahusika na kutoa
nyaraka zamaelekezo ya kuhakikisha kwamba udhibiti wa ndani9wa matumizi
unaimarishwa katika ngazi zote zausimamizi na inapobidi hatua za
kisheria zichukuliwekwa wahusika.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara inatarajia kutekeleza
yafuatayo: kupitia mfumowa uwasilishaji wa bajeti za wizara, idara za
Serikali,mikoa na halmashauri na kuhakikisha kuwa sera namipango ya
kitaifa na ile ya kisekta vyote vimezingatiwaipasavyo katika Bajeti ya
Serikali na kutengewa fedha;kufanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya
Serikali,kuendelea kuboresha mfumo wa mpangilio wa Bajeti
yaSerikalikwakuzingatiaprogram umbalimbali;kuimarisha mifumo ya kompyuta
ya uandaaji bajeti ilikukidhi mahitaji ya taarifa mbalimbali
zinazohitajika;kuendelea kujenga uwezo wa wizara, idara za
Serikali,mikoa na halmashauri katika uandaaji wa Bajeti yaMuda wa Kati,
usimamiaji wake na utoaji taarifa zautekelezaji ikiwa ni pamoja na
ufuatiliaji na tathminikwa wakati; kutayarisha taarifa mbalimbali
zautekelezaji wa Bajeti ya Serikali ili kuhakikisha uwazina uwajibikaji
unazingatiwa; na kufuatilia matumizi yafedha za umma zikiwemo fedha za
mishahara, matumizimengineyo na fedha za miradi.Usimamizi wa Misaada na
Mikopo
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara ilifanikisha kusainiwa
kwa mikataba 18 kwa ajiliya misaada na mikopo nafuu yenye thamani ya
jumlaya shilingi bilioni 958.027 kutoka kwa Washirika waMaendeleo.
Aidha, Wizara imeendelea kuratibuukamilishaji wa Mwongozo mpya wa
Ushirikiano wa10Maendeleo – Development Cooperation Frameworkambao
utachukua nafasi ya Mkakati wa Pamoja waMisaada Tanzania (MPAMITA).
Mwongozo huu unalengo la kusimamia ushirikiano wa maendeleobaina ya
Serikali na Wadau wa Maendeleo nakuendeleza mafanikio yaliyopatikana
wakati wautekelezaji wa MPAMITA. Lengo la ujumla nikupatikana ufanisi
katika misaada kutoka kwaWashirika wa maendeleo na kubainisha wajibu
wakila mdau wa maendeleo wakiwemo raia, wabunge,asasi zisizo za
kiserikali na sekta ya habari.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara imepanga kufanya
yafuatayo: kuzinduaMwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo na kuandaampango
kazi wake pamoja na kuhamasisha matumiziyakekwa Washirika wa Maendeleo,
Wizara, IdaraZinazojitegemea, Serikali za Mitaa, Taasisi Binafsi
naWaheshimiwaWabunge; kutathmini utekelezaji wamiradi na programu
mbalimbali inayotekelezwa kwafedha toka Washirika wa Maendeleo kwa nia
yakuhakikisha kwamba thamani ya fedha inapatikanakatika miradi hiyo;
kushiriki kwenye majadiliano naJumuiya za kikanda na kimataifa; na
kuendeleakutafuta fedha za misaada na mikopo nafuu kwa ajili
yautekelezaji wa miradi ya maendeleo, na Misaada yaKiufundi kutoka kwa
Mashirika ya Kimataifa na nchiwahisani.11Ulipaji wa Deni la Taifa
Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa limeendeleakusimamiwa na Sheria ya
Madeni ya mwaka 1974 namarekebisho yake ya mwaka 2004. Wizara
imeendeleakutoa kipaumbele katika ulipaji wa madeni kwa wakatiili
kuepuka malimbikizo ya riba. Katika kipindi chaJulai, 2013 hadi Aprili,
2014 malipo ya deni la ndaniyalifikia shilingi bilioni 1,694.53 ambapo
kati ya malipohayo riba ni shilingi bilioni 581.20 na Mtaji
(principalrollover) ni shilingi bilioni 1,113.33. Aidha, deni la
njelimelipwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 340.22, kati yakiasi hicho
malipo ya riba ni shilingi bilioni 201.52 nadeni halisi – principal ni
shilingi bilioni 138.70.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara itaendelea kulipa
madeni ya ndani na nje kwawakati ikiwa ni pamoja na kulipa kwa wakati
madenimbalimbaliambayoserikali imeingiamikataba(Contractual Liabilities)
na madai ya dharura(Contingent Liabilities) pindi yanapotokea.Usimamizi
wa Matumizi ya Fedha za Umma
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kujengauwezo wa usimamizi wa
matumizi ya fedha za ummakwa kudhamini mafunzo ya muda mrefu
kwawatumishi 313 wa kada ya uhasibu, ugavi na kompyutakutoka kwenye
wizara, idara za serikali, sekretariati zamikoa,manispaa, halmashauri za
miji na wilayawaliopo vyuoni na watumishi 218 walipewa mafunzo yamuda
mfupi kwa lengo la kuongeza ufanisi katikausimamizi wa matumizi ya fedha
za umma. Aidha,12Wizara imeendelea kusambaza Mfumo wa Malipo
waKielektroniki -TISS mikoani ambapo hadi sasa jumla yamikoa 20
imeunganishwa katika mtandao huo. Mikoailiyounganishwa kwenye mtandao
huo ni Iringa,Morogoro, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa,Ruvuma,
Lindi, Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita, Mara,Mtwara, Kigoma, Shinyanga,
Njombe, Dar es Salaam naKatavi. Vile vile, mikoa mipya ya Geita, Simiyu,
Katavina Njombe imeunganishwa kwenye mtandao wa malipowa Serikali
(Intergrated Financial Management System).
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea nampango wa kutekeleza mfumo wa
uandaaji wa taarifaza hesabu kwa kuzingatia Viwango vya Kimataifa
vyaUandaaji wa Taarifa za Hesabu katika Sekta ya Umma -IPSAS Accrual
Basis ambapo hesabu za majumuisho zamwaka 2012/13 zimeandaliwa kwa
kutumia mfumohuo kwa mara ya kwanza na kuwasilishwa kwaMdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwawakati.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,pamoja na mambo mengine,
Wizara itaendeleakuboresha usimamizi wa fedha za umma kwa
kufanyayafuatayo: kuendelea kutoa udhamini wa masomo yamuda mrefu na
mfupi kwa wahasibu, wakaguzi,maafisa ugavi na wataalamu wa kompyuta
kutokaSerikali Kuu na serikali za mitaa; kuweka mitambokatika hazina
ndogo zote ili kuwezesha sekretariati zamikoa na hazina ndogo kufanya
malipo kwa kutumiamifumo ya malipo ya kielektroniki
-TISS/EFT;13kuendelea kutoa mafunzo ya TISS/EFT kwa wahasibuna watumishi
wa kada zingine ili kuimarisha mfumo wamalipo; na kuanza ujenzi wa
jengo la ofisi ya HazinaNdogo Arusha.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 ilikuinua kiwango cha fani ya
uhasibu sambamba nakuimarisha usimamizi wa fedha za umma Tanzaniaitakuwa
mwenyeji wa mkutano wa Wahasibu Wakuu waSerikali wa nchi za Mashariki
na Kusini mwa Afrika –ESAAG.Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha
zaUmma – Public Finance Management ReformProgramme (PFMRP)
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Programu yaMaboresho ya Usimamizi wa
Fedha za Ummaimekamilisha utafiti wa mfumo wa kupeleka fedhakwenye
Serikali za Mitaa, mpango wa utekelezaji wautafiti huo umeandaliwa na
utekelezaji wake utaanzamwaka wa fedha 2014/15. Aidha, utafiti juu ya
mifumoya fedha inayotumiwa na Serikali kwa lengo lakuiunganisha mifumo
hiyo ili kuboresha usimamiziwake umekamilika. Vile vile, Wahasibu 522
kutokaWizara mbalimbali, hazina ndogo na sekretarieti zamikoa walipata
mafunzo juu ya Viwango vya Kimataifavya Uandaaji wa Taarifa za Hesabu
katika Sekta yaUmma na watumishi wengine 34 ambao wanasimamiaprogramu
hii kutoka katika wizara na taasisi walipatamafunzo ya kusimamia
Mabadiliko na Kuandaa14Mipango Mkakati -Change Management and
StrategicPlanning. Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo wakuandaa
mipango na bajeti inayolenga katikakutekeleza maboresho ya usimamizi wa
fedha za umma.
Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2014/15,Wizara itaendelea kuboresha
usimamizi wa fedha zaumma kwa kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Nneya
Programu ya PFMRP kwa kufanya yafuatayo: kupitiana kuboresha mifumo ya
kifedha na kuangalia njia boraya kuiunganisha baada ya utafiti
kukamilika;nakuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani katika wizara,idara,
wakala za Serikali na halmashauri za Serikali zaMitaa juu ya ukaguzi wa
mifumo ya fedha, usimamizina ukaguzi wa vihatarishi, ukaguzi wa bajeti
namishahara, na ukaguzi wa miradi.Sera ya Ununuzi wa Umma
Mheshimiwa Spika, katika kusimamia Sekta yaUnunuzi wa Umma nchini,
Wizara imeendeleakutekeleza yafuatayo:kuandaa Sera ya Taifa yaUnunuzi wa
Umma; kuandaa mapendekezo ya muundowa Vitengo vya Usimamizi wa Ununuzi
na UgaviSerikalini; na kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzokwa
maafisa ununuzi na ugavi walioko katika Mamlakaza Serikali za Mitaa; na
kuendelea kuhuisha taarifa zamaafisa ununuzi na ugavi Serikalini, ambapo
taarifa zamaafisa 332 katika mikoa ya Shinyanga, Kagera,Mwanza na Mara
zimehakikiwa na kuingizwa katikadaftari la maafisa ununuzi na ugavi.15
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara imepanga kufanya
yafuatayo: kuandaa Mkakatiwa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ununuzi wa
Ummana kusimamia utekelezaji wa Sera hiyo; kuhuishamuundo wa vitengo vya
usimamizi wa ununuzi na ugaviserikalini; kuipitia Sheria ya Ununuzi wa
Umma Na.7ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013;kukamilisha tathmini
ya mahitaji ya mafunzo kwamaafisa ununuzi na ugavi Serikalini; na
kufanyatathmini juu ya ufanisi wa ununuzi wa umma nchini.Udhibiti wa
Ununuzi wa Umma
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Mamlaka ya
Udhibiti wa Ununuzi waUmma imetoa mafunzo kuhusu sheria, kanuni
nataratibu za ununuzi kwa taasisi za umma 32 ambapowatumishi 747
walihudhuria mafunzo hayo. Aidha,Mamlaka ilitoa mafunzo kuhusu mfumo wa
upokeaji nausimamizi wa taarifa za ununuzi nchini katika vituovinne vya
Morogoro, Arusha, Mwanza na Mbeya ambapojumla ya washiriki 330 kutoka
taasisi 191 walishiriki.Vile vile, Mamlaka imeendelea kusimamia mfumo
waupokeaji na usimamizi wa taarifa za ununuzi
nchiniambapokatikakipindihicho ,taasisi191ziliunganishwa na kupatiwa
mafunzo ya kutumiamfumo huo na hivyo kufanya jumla ya
taasisizilizounganishwa na kupatiwa mafunzo kufikia 364,sawa na asilimia
80 ya taasisi zote.16
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka yaUdhibiti wa Ununuzi wa
Umma imefanya ukaguzikuhusu utoaji wa zabuni na utekelezaji wa
mikatabaitokanayo na ununuzi wa umma katika Taasisi 120zikiwemo wizara
na idara zinazojitegemea 32, mashirikaya umma 46 na serikali za mitaa
42. Ukaguzi huuuilihusisha mikataba 5,867 yenye thamani ya
shilingibilioni 1,985.427 ikiwemo miradi 207 ya ujenzi yenyethamani ya
shilingi bilioni 777.2. Ripoti ya ukaguziinaonesha wastani wa
uzingatiwaji wa sheria yaununuzi ulikuwa ni asilimia 64 ambayo ni chini
yalengo la asilimia 80. Maeneo yaliyobainika kuwa naudhaifu mkubwa ni
katika usimamizi wa mikataba nautunzaji wa nyaraka za ununuzi.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara imepanga kutekeleza
yafuatayo: kuandaampango kazi wa usimamizi wa utekelezaji wa Sheria
yaUnunuzi wa Umma ya Mwaka 2011; kuelimisha wadaumbalimbali kuhusu
Sheria mpya na kanuni zake;kuendelea na maandalizi ya kuanzisha mfumo
waununuzi kwa njia ya kielektronic (e-procurementsystem); kufungua ofisi
za kanda Dodoma, Mbeya naMwanza; kushirikiana na TAMISEMI ili
kukabiliana nachangamoto zilizopo kwenye vitengo vya ununuzi
vyahalmashauri mbalimbali; kufanya kazi na Asasi zaKiraia na Wanahabari
ili kuongeza uelewa wa masualaya Ununuzi wa Umma kwa wananchi; na
kuendeleakusimamia ununuzi katika sekta ya Umma.17Huduma ya Ununuzi
Serikalini
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Wakala wa
Huduma ya UnunuziSerikalini imetekeleza yafuatayo: kuongeza vifaa
vyahuduma mtambuka kutoka 86 vilivyokuwepo hadi 181;kuendelea na ujenzi
wa Ofisi na ghala katika mkoa waManyara; kuendelea na ujenzi wa kituo
cha mafutamkoa wa Dodoma; na kununua magari mawilimakubwa yenye uwezo wa
kubeba lita 45,000 za mafutakila moja kwa ajili ya kusafirisha mafuta
toka kwawazabuni kwenda mikoani. Aidha, Wakala wa Hudumaya Ununuzi
Serikalini, imeanza kufunga Mfumo waUdhibiti na Usimamizi wa Mafuta ya
Magari ambaoutaanza kwa majaribio Agosti, 2014 katika mkoa waDar es
Salaam ili kudhibiti matumizi ya mafuta katikamagari ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Wakala wa
Huduma ya UnunuziSerikalini imepanga kutekeleza yafuatayo:
kukamilishakazi ya kufunga Mfumo wa Udhibiti na Usimamizi waMafuta ya
Magari katika mikoa ya Arusha, Mwanza,Dodoma, Iringa na Mbeya; kuanza
kazi za Ujenzi waOfisi katika mikoa ya Njombe na Mara; kukamilishaujenzi
wa visima vya mafuta katika mikoa ya Geita,Katavi na Wilaya ya Ileje;
na kuongeza uwezo wakuhifadhi mafuta kufikia wastani wa lita 50,000
katikavituo vya mikoa ya Arusha, Mwanza, Kigoma, Mtwara,Lindi, Tabora,
Pwani, Tanga na Ruvuma. Aidha, Wakalawa Huduma ya Ununuzi Serikalini
itahuisha muundowake ili kuweza kutoa huduma ngazi ya wilaya na18kuanza
kutekeleza utaratibu wa ununuzi wa magarikwa pamoja.Rufaa za Zabuni za
Umma
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za
Umma imepokea jumlaya mashauri35, kati ya hayo mashauri
matatuyaliondolewa na walalamikaji kabla ya kusikilizwa;mashauri 17
walalamikaji walishinda; mashauri 11walalamikaji walishindwa; mashauri
mawili yalifutwakufuatana na sheria; shauri moja halikutolewa
uamuzikutokana na ukomo wa muda wa kulisikiliza; na shaurimoja lipo
kwenye hatua ya kusikilizwa. Aidha, katikamwaka 2014/15, Mamlaka
itaendelea kusikiliza nakutolea maamuzi malalamiko na rufaa katika
Ununuziwa Umma na kuelimisha umma na wadau juu yakuwasilisha pingamizi
za zabuni kwa mujibu wa Sheriaya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011.Usimamizi
wa Mali ya Serikali
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara iliendelea kuandaa Sera
ya Mali ya Umma.Lengo la sera hii ni kusimamia na kutoa miongozo
yaudhibiti wa mali ya umma. Aidha, Wizara ilifanyauthamini wa mali ya
Serikali katika mikoa mitano nawizarambili,hivyokufanyawiza
ra,idarazinazojitegemea na wakala wa Serikali zilizofanyiwauthamini
kufikia 42. Katika kipindi hicho, usimikaji wamfumo wa uhakiki wa mali
ya umma ulikamilika. Vilevile, Wizara iliendelea na zoezi la kuondosha
mali19chakavu katika wizara na idara za Serikali ambapojumla ya shilingi
bilioni 1.58 zilikusanywa kutokana namauzo ya vifaa hivyo na shilingi
milioni 12.83 kutokanana utoaji wa leseni za udalali.
Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya uhakiki wamali ya Serikali katika
wizara, idara zinazojitegemea nawakala za Serikali kwa lengo la
kudhibiti matumizi yamali katika taasisi hizo. Aidha, Wizara imefanya
uhakikimaalum katika Bohari Kuu ya Madawa ambapo ushauriulitolewa wa
namna ya kupunguza hasara inayotokanana madawa, vifaa tiba na
vitendanishi kuisha mudawake wa matumizi kabla ya kutumika.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka, 2014/15,Wizara imepanga kukamilisha
Sera ya Mali ya Ummana kuisambaza kwa wadau kwa ajili ya kupata
maonikabla ya kuanza utekelezaji wake. Aidha, Wizaraimepanga kufanya
uthamini wa mali katika mikoa sabana taarifa zake kuingizwa kwenye
Daftari la Mali yaSerikali. Vile vile, Wizara itaendelea kuondosha
malichakavu, mali zilizokwisha muda wake na vifaa sinziakwa mujibu wa
Sheria na Kanuni za Fedha za Umma;kushughulikia taarifa za ajali na
potevu za mali yaSerikali;nakuendeleakuchambu a,kufanyamajadiliano na
wadai na kulipa madai ya fidia na kifutamachozi yanayotokana na amri ya
Mahakama.Kadhalika, Wizara itaendelea na uhakiki wa mali katikawizara,
idara zinazojitegememea na wakala za Serikali.Mpango wa
MilleniumTanzania (MCA-T)20ChallengeAccount–
Mheshimiwa Spika, Programu ya MilleniumChallenge Account Tanzania
iliendelea na ukamilishajiwa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya
usafirishaji,nishati ya umeme na maji. Miradi yote ya
barabaraimekamilika isipokuwa sehemu ya Laela- Sumbawangakatika barabara
ya Tunduma- Sumbwanga ambayoinatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa
mwaka2014. Miradi ya umeme na maji imekamilika na ipokatika kipindi cha
uangalizi. Aidha, kutokana nautekelezaji wa kuridhisha, Tanzania
imekidhi vigezo nahivyo itanufaika na awamu ya pili ya msaada waSerikali
ya Marekani kupitia Shirika lake laChangamoto za Milenia (MCC). Katika
awamu ya pili,miradi itakayofadhiliwa ni ya umeme na barabara zavijijini
Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.Ukaguzi wa Ndani
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara imetekeleza yafuatayo:
kutoa Mwongozo waKamati za Ukaguzi katika Sekta ya Umma kwa lengo
lakuhakikisha utendaji wenye tija kwa Kamati zote zaUkaguzi; kutoa
mafunzo ya kuwajengea uwezowakaguzi wa ndani 458, wajumbe wa Kamati
zaUkaguzi na wadau wa ukaguzi wa ndani wapatao 567;kufanya ukaguzi wa
miradi ya maendeleo 11; ukaguziwa orodha ya malipo ya mishahara; na
kuhakiki madaimbalimbali yaliyowasilishwa wizarani kabla ya kulipwa.21
Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudi zaSerikali za kudhibiti
ubora wa utekelezaji wa miradimbalimbali ya maendeleo, Wizara imenunua
vifaa vyakuhakiki ubora wa miundombinu. Vifaa hivyovitatumika katika
ukaguzi wa miradi inayotekelezwa naWizara, Idara, Wakala za Serikali na
Halmashauri zaSerikali za Mitaa katika kuhakikisha kuwa miradi
namiundombinu inayotekelezwa inakuwa na uboraunaokidhi viwango na
hatimaye kupata thamani yafedha. Hatua hii itaenda sambamba na
kuwajengeauwezo wakaguzi wa ndani Serikalini katika kufanyaukaguzi wa
kiufundi kwa miradi inayotekelezwa katikataasisi zao.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara itaendelea kusimamia
kada ya ukaguzi wa ndanina kamati za ukaguzi; kufanya ukaguzi wa Mfumo
waulipajiMishaharaSerikalini;k uhakikimadaimbalimbali ya Serikali kabla
ya kuyalipa; na kufuatiliautekelezaji wa miongozo mbalimbali
iliyotolewa. Aidha,Wizara inatarajia kutoa miongozo ifuatayo: Mwongozowa
Usimamizi wa Viashiria Vya Udanganyifu; Mwongozowa Udhibiti wa Ndani;
Mwongozo wa Ufuatiliaji naTathmini ya Usimamizi wa Vihatarishi; Mwongozo
waUkaguzi wa Ununuzi; na Mwongozo wa Ukaguzi waMikataba. Vile vile,
wizara kwa kushirikiana na Taasisiza Serikali itaendelea kuimarisha
ofisi za MkaguziMkuu wa ndani kwa lengo la kusimamia matumizi
yafedha.Ukaguzi wa Hesabu za Serikali22
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Ofisiya Taifa ya Ukaguzi
imetekeleza kazi zake kwa mujibuwa sheria. Ofisi imeendelea kuwa
mshirika katika Bodiya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa katika kukagua
taasisiza Umoja wa Mataifa. Aidha, Ofisi imeendesha mafunzokwa Kamati za
Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikalina Kamati ya Bajeti kwa lengo la
kuzijengea uwezo wakuimarisha uwajibikaji na utawala bora. Vile
vile,ukaguzi wa mapato na matumizi ya vyama vya siasavyenye usajili wa
kudumu unaendelea.
Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuondoawakaguzi katika majengo ya
wakaguliwa, Ofisi ya Taifaya Ukaguzi imekodi majengo ya ofisi katika
mikoa yaMwanza, Tabora, Tanga, Iringa, Kagera na Geita. Aidha,ujenzi wa
ofisi katika mkoa wa Dodoma unaendeleaukiwa katika hatua za mwisho. Vile
vile, Ofisiimeendelea na uunganishaji wa ofisi zake zilizokomikoani na
makao makuu kwa njiaya mtandaompana. Kwa mwaka huu ofisi 4
zimeunganishwa nahivyo kufanya ofisi zilizounganishwa kufikia 14.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15, Ofisiinatarajia kufanya
yafuatayo: kukagua mafungu yote 49ya Wizara na Idara za serikali, hesabu
za Mikoa yote 25ya Tanzania Bara, Hesabu za Halmashauri zote 161
zaWilaya, Miji, Manispaa na Majiji, Mashirika ya Umma177, Balozi zote 32
zilizoko nje ya nchi na Wakala 33 zaSerikali pamoja na kufanya ukaguzi
wa thamani yafedha katika maeneo sita; kuendelea na ukaguzi wamapato na
matumizi ya vyama vyote vya siasa; kuanzaukaguzi katika sekta ya gesi na
mafuta pamoja na23ukaguzi wa miradi mikubwa inayoendeshwa kwa ubiawa
sekta ya Umma na Sekta binafsi; kuendeleakushiriki kikamilifu katika
jukumu la kukagua taasisiza Umoja wa Mataifa sanjari na wanachama
wenginewanaounda Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.
Mheshimiwa Spika,mambomengineyatakayoteke lezwa katika mwaka 2014/15,
ni pamojana: kuendelea na zoezi la kuwaondoa wakaguzi katikamaeneo ya
wakaguliwa katika wizara zote na katikamikoa 6 iliyobaki; kuendelea
kuzijengea uwezo kwa njiaya mafunzo Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu
zaSerikali na Kamati ya Bajeti katika maeneo ya
kuelewakwaundanitaarifazaukagu ziwahesabuzinazoandaliwa na wakaguliwa;
kukamilisha ujenzi waofisi katika mkoa wa Rukwa pamoja na kuanza
ujenziwa ofisi katika mikoa ya Mara na Iringa; na kutoamafunzo kwa
watumishi ili kuimarisha uwezo waokatika kutumia mfumo wa TeamMate ili
kuendana namabadiliko ya teknolojia katika ukaguzi wa kisasa.Uratibu wa
Utekelezaji wa MKUKUTA
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibuutekelezaji wa MKUKUTA II
kwa kufanya ufuatiliaji,tafiti, na tathmini na kuandaa taarifa ya
utekelezaji nahali ya Umaskini nchini ili kuwezesha maamuzi yakisera,
kibajeti na kiutekelezaji. Kazi ya uandaaji waTaarifa ya Mwaka ya
Utekelezaji wa MKUKUTA IIimekamilika na kuwekwa katika tovuti ya
Wizara.Aidha, Wizara inaendelea kukamilisha Taarifa ya24Maendeleo ya
Malengo ya Milenia. Taarifa ya awaliinaonesha kuwa umaskini wa mahitaji
ya msingi kwaTanzania Bara ni asilimia 28.2 ambapo kwa Dar esSalaam ni
asilimia 4.2, maeneo mengine ya mjini niasilimia 21.7 na maeneo ya
vijijini ni asilimia 33.3.Umaskini wa chakula ni asilimia 9.7 ambapo kwa
Dares Salaam ni asilimia 1.0, maeneo mengine ya mjini niasilimia 8.7 na
maeneo ya vijijini ni asilimia 11.3.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara imepanga kutekeleza
yafuatayo: kukusanya nakuchambua taarifa mbalimbali kutoka katika
Wizara,Idara na Wakala za Serikali ili kuandaa Taarifa yamwaka ya
Utekelezaji wa MKUKUTA II; kuandaa taarifaya mwisho ya kutathimini
utekelezaji wa Malengo yaMaendeleo ya Milenia; kufanya mapitio ya
MKUKUTA II;kukamilisha Mpango wa Utekelezaji wa Kinga ya Jamiipamoja na
kuainisha viashiria vya upimaji juhudi zakinga ya jamii; na kuratibu
mkutano wa kitaifa wakujadili sera za kupambana na Umaskini nchini.
PiaWizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbaliinaandaa mapendekezo ya
hatua zitakazofuata baadaMKUKUTA II kufikia kikomo mwezi Juni, 2015.
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mradi waSELF II imeendelea kutoa
mikopo kwa wajasiriamaliambapo hadi kufikia Aprili 2014, mikopo yenye
thamaniya shilingi bilioni 8.6 ilikopeshwa kwa wajasiriamali4,943
kupitia Asasi ndogo 103. Kati ya waliokopeshwa,wanawake ni 2,040 sawa na
asilimia 41 na wanaume ni2,903 sawa na asilimia 59. Kwa wastani,
urejeshwaji waMikopo ya Mradi wa SELF umeendelea kuwa wa ufanisi25mzuri
katika kiwango cha asilimia 90 hivyo kuwezeshafedha za mkopo kuzunguka
na kuwafikia wananchiwengi zaidi.
Mheshimiwa Spika, SELF II imetoa mafunzo
kwawatendaji280waAsasi115zinaz okopeshawajasiriamali wadogo. Aidha,
mafunzo yametolewa kwawajasiriamali wadogo 1,670 katika taaluma
yauendeshaji miradi ya biashara. Vile vile, MaofisaUshirika 81 kutoka
mikoa ya kanda za Kaskazini naZiwa walipatiwa mafunzo ya utoaji mikopo.
Kadhalika,Mradi umeendelea kuelimisha umma kupitia vituo vyatelevisheni
vya TBC, ZBC na redio za jamii. Katikamwaka 2014/15, Mradi wa SELF
utaendelea namajukumu yake ya kutoa huduma za mikopo kwawajasiriamali
wadogo na kuimarisha huduma zakifedha kwa njia ya kujenga uwezo wa
Asasizinazokopesha wajasiriamali wadogo.Sheria na Miswada ya Fedha
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kwa kushirikiana na
Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali ilifanya marekebisho ya
Sheriambalimbali za Fedha kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka2013 -The
Finance Act, 2013. Lengo la marekebishohayo ni kuweka usimamizi mzuri wa
kodi na fedha zaumma. Aidha, Sheria mbalimbali zilizopitishwa naBunge
ni pamoja na Sheria ya Mfuko wa Akiba waGEPF wa Mafao ya Wastaafu ya
mwaka 2013 -The GEPFRetirement Benefit Fund Act, 2013 na marekebisho
yaSheria ya Ushuru wa Bidhaa ya mwaka 2013 (The26Excise (Management and
Tariff) (Amendment) Act, 2013)yaliyopitishwa na Bunge katika Mkutano wa
13 mweziDesemba, 2013 yaliyolenga kuondoa kodi ya ushuru wabidhaa kwenye
Sim Card.
Mheshimiwa Spika, Wizara pia iliandaa Kanunimbalimbali ili kuwezesha
usimamizi na utekelezaji waSheria za fedha. Kanuni hizo ni pamoja na
Kanuni zaKodi ya Mapato kuhusu Gharama za Kuhamisha -Transfer Pricing
Regulations, 2013, Kanuni za Sheria yaUnunuzi wa Umma, 2013 – Public
ProcurementRegulations, 2013, Kanuni za Uanzishwaji wa Baraza
laUsuluhishi wa Bima, 2013 -The Insurance OmbudsmanRegulation, 2013,
Kanuni za Uanzishwaji wa chombocha kushughulikia Rufaa za masuala ya
Bima, 2013 -The Insurance Appeals Tribunal Regulations, 2013 naKanuni za
Bima Ndogo – The Micro-InsuranceRegulations, 2013.
Mheshimiwa Spika, katika mkutano wa Bunge laBajeti unaoendelea Wizara
inatarajia kuwasilishaMuswada wa kutunga Sheria mpya ya Kodi yaOngezeko
la Thamani – Value Added Tax -VAT na Sheriaya Usimamizi wa Kodi – Tax
Administration Act.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizaraitakamilishamaandaliz
iyakufanyiamarekebisho Sheria ya Msajili wa Hazina – TreasuryRegistrar
Act, Sheria ya Takwimu (Statistics Act) naSheria ya Fedha za Umma
-Public Finance Act. Aidha,Wizara ipo katika maandalizi ya kuwezesha
kutungwakwa Sheria ya Kodi ya Hoteli -Hotels Tax Act na
kufanya27marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada naDhamana za Serikali –
Government Loans, Grants andGuarantees Act.Ubia kati ya Sekta ya Umma
na Sekta Binafsi – PPP
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kupokeana kuchambua maandiko ya
miradi inayokusudiwakutekelezwa kwa utaratibu wa ubia kati ya Sekta
yaUmma na Sekta Binafsi. Katika mwaka 2013/14,Wizara imepokea na
kuchambua miradi minne ya PPP.Katika uchambuzi wa miradi imebainika
kwamba kunaupungufu katika upembuzi yakinifu pamoja na ukosefuwa
Wataalam wa kufanya upembuzi huo. Aidha, Wizaraimeshiriki kutoa
mapendekezo ya kurekebisha Sheriaya Ubia Na. 18 ya mwaka 2010 pamoja na
kanuni zakekwa lengo la kuweka usimamizi mzuri wa ubia.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15Wizara imetenga fedha za
kuanzisha Mfuko waKuwezesha Utekelezaji wa Miradi ya Ubia
-PPPFacilitation Fund.Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Kitengo cha
Udhibiti wa Fedha Haramuimepokea na kuchambua taarifa 46 za miamala
shukuinayohusu fedha haramu na ufadhili wa ugaidi
nataarifa14zakiintelijensia28z imewasilishwa kwenye
vyombovinavyosimamiautekelezaj i wa sheria. Aidha, mafunzo ya
kudhibitifedha haramu na ufadhili wa ugaidi yametolewa kwawatoa taarifa
135 na washiriki 86 kutoka katikavyombo vinavyosimamia utekelezaji wa
Sheria yaUdhibiti wa Fedha Haramu na Mali Athirika. Vile vile,mafunzo
hayo yametolewa kwa washiriki 49 kutokaMamlaka za Udhibiti.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Kitengo cha
Kudhibiti Fedha Haramuitatekeleza yafuatayo: kupokea na kuchambua
taarifaza miamala shuku inayohusu utakasishaji wa fedhaharamu na
ufadhili wa ugaidi; kutoa mafunzo kwavyombo vinavyosimamia utekelezaji
wa sheria na kwawatoa taarifa; kutoa miongozo ya kudhibiti fedhaharamu
na ufadhili wa ugaidi kwa watoa taarifa;kuratibu zoezi la kutathmini
mianya na viashiria vyafedha haramu na ufadhili wa ugaidi katika
sektambalimbali nchini; na kuendelea na hatua za kujiungana Umoja wa
Kupambana na Biashara ya FedhaHaramu na Ufadhili wa Ugaidi Duniani –
EGMONTGroup of Financial Intelligence Units.Tume ya Pamoja ya Fedha
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Tume ya Pamoja
ya Fedha imekamilishaStadi ya Kubainisha Mfumo Bora wa Kodi wa Jamhuriya
Muungano wa Tanzania, pamoja na kuendelea na29Uchambuzi wa Uhusiano wa
Mwenendo wa Uchumi naMapato ya Muungano.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Tume ya Pamoja
ya Fedha inatarajiakukamilisha Stadi ya Kubainisha Mwenendo waUchumi na
Mapato ya Muungano wa Tanzania, nakufanya Stadi ya Uwekezaji katika
Mambo yaMuungano. Aidha, Tume inatarajia kuhuisha Takwimumbalimbali za
Stadi zilizofanywa na Tume.Habari, Elimu na Mawasiliano kwa Umma
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwambaWadau mbalimbali wanapata
taarifa zinazohusu kazina majukumu ya Wizara, Wizara imetoa elimu
kwaumma kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Aidha,Wizara imeandaa
machapisho na vipeperushi kwa ajiliya kuelezea mafanikio, changamoto na
njia zilizotumikakatika kukabiliana na changamoto hizo.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara itaendelea kuandaa
taarifa kuhusu utekelezajiwa majukumu yake na kuelimisha umma
kupitiavyombo vya habari, maonesho, machapisho navipeperushi. Aidha,
Wizara itakamilisha Mkakati waMawasiliano.Masuala ya Watumishi
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuchukuahatua mbalimbali za
kujenga uwezo wake ili iwezekutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Hatua
hizo ni30pamoja na: kupeleka watumishi katika mafunzo yamuda mfupi na
mrefu, kuajiri watumishi 10,kuthibitisha watumishi 21 kazini, kupandisha
vyeowatumishi 131, kuboresha mazingira ya kazi kwakukarabati baadhi ya
ofisi na kununua vifaa vya ofisi.Aidha, Wizara imeendelea kutoa huduma
stahiki kwaWatumishi wa Wizara wanaoishi na virusi vya UKIMWIna kutoa
elimu ya afya kwa wafanyakazi.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara inatarajia kuajiri
watumishi 257 wa kadambalimbali; kupandisha vyeo watumishi 490;
nakuthibitisha kazini watumishi 10. Aidha,
Wizarainatarajiakuwapatiawatum ishi642mafunzombalimbali ya kuwajengea
uwezo katika kutekelezamajukumu yao, kutoa elimu kuhusu magonjwa sugu
nakutoa huduma stahiki kwa watumishi wa wizarawanaoishi na virusi vya
UKIMWI.Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Ofisi ya
Msajili wa Hazina imechambuana kutangaza katika Gazeti la Serikali
mashirika 10ambayo yanatakiwa kuchangia asilimia 10 ya mapatoghafi
katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Hadi kufikiaAprili2014,kiasichashil
ingibilioni25.0kimekusanywa ikiwa ni asilimia 69.4 ya makadirio
yakukusanya shilingi bilioni 36 kwa mwaka 2013/14.31Aidha, katika
kutekeleza zoezi la kuingia mikataba yautendaji na Bodi za mashirika ya
umma, Wizarainakamilisha majadiliano na Bodi za mashirika yaumma. Vile
vile, zoezi la kumpata Msajili wa Hazinalimefikia hatua za mwisho.
Matarajio ni kwamba uteuziutafanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa
fedha.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara inatarajia kutekeleza
yafuatayo: kusimamiautendaji wa Bodi za Wakurugenzi wa mashirika
nataasisi za umma na kuingia mikataba ya utendaji naBodi za mashirika ya
umma; kusimamia mikakati yakurekebisha mashirika ya umma na kufanya
tathminina ufuatiliaji wa Mashirika ya Umma yaliyobinafsishwa;na
kuimarisha usimamizi wa mashirika na taasisi zaumma ili kuongeza mapato
ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Shirika Hodhi
la Mali za Umma (CHC)imeendelea na zoezi la ubinafsishaji na
urekebishaji wamashirika ya Umma. Wizara inaendelea na zoezi
latathminiyautendajiwamashirik amengineyaliyobinafsishwa kwa lengo la
kufahamu kamamakubaliano ya mikataba ya mauzo yanazingatiwa nakuchukua
hatua stahiki.Mafao ya Wastaafu na Mirathi
Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboreshakumbukumbu za Wastaafu,
kulipa mafao na michango32ya kisheria kwa wakati. Hadi Aprili 2014,
kumbukumbuza wastaafu 142,014 zimehifadhiwa kwenye mfumo wakompyuta –
SAPERION na shilingi bilioni 220.79 sawana asilimia 87 ya makadirio
kimelipwa kama mafao yawastaafu wanaolipwa Pensheni na Hazina.
Aidha,Wizara imefanya uhakiki wa wastaafu walio kwenyeDaftari la
Pensheni la Hazina katika mikoa tisa. Vilevile, shilingi bilioni 522.86
sawa na asilimia 76 yamakadirio ya mwaka kimelipwa kama michango
yamwajiri kwa watumishi wa Serikali Kuu na Serikali zaMitaa wanaochangia
kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamiipamoja na michango ya Bima ya Afya.
Mheshimiwa Spika,Wizaraimeendeleakusimami a na kuratibu shughuli za
Mfuko wa Penshenikwa Watumishi wa Umma – PSPF, Mfuko wa Pensheniwa PPF
na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu – GEPF.Utekelezaji wa Mifuko hiyo kwa
mwaka 2013/14ulikuwa kama ifuatavyo:Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa
Umma – PSPF
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2014,Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Ummaulikusanya shilingi bilioni 492.29 ambapo kati ya
hizomichango ya wanachama ni shilingi bilioni 402.24 namapato yatokanayo
na vitega uchumi ni shilingi bilioni90.05. Aidha, shilingi bilioni
490.95 zilitumika kulipamafao ikiwa ni pamoja na mafao ya kiinua mgongo
napensheni za kila mwezi. Katika mwaka 2014/15, Mfukounatarajia
kukusanya jumla ya shilingi bilioni 798.12kutoka vyanzo
mbalimbali.33Mfuko wa Mafao ya Kustaafu – GEPF
Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Mafao ya Kustaafuwa GEPF ambao awali
ulikuwa ukijulikana kama Mfukowa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini,
umebadili mfumowa malipo ya mafao kutoka akiba na kwenda kwenyemfumo wa
pensheni. Mabadiliko haya yamefanywa kwamujibu wa Sheria Na. 8 ya mwaka
2013 iliyopitishwa naBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
HadiAprili 2014, Mfuko umeweza kusajili jumla yawanachama 10,289 ambapo
wanachama 8,138 nikutoka sekta isiyo rasmi. Aidha, michango yawanachama
ilifikia kiasi cha shilingi bilioni 31.68 sawana asilimia 79.95 ya lengo
la kukusanya jumla yashilingi bilioni 39.62 ifikapo Juni 2014. Vile
vile,mapato yatokanayo na vitega uchumi yamefikia shilingibilioni 17.86
ambayo ni sawa na asilimia 84 ya lengo lakukusanya shilingi bilioni
21.26 kufikia Juni 2014.Thamani ya Mfuko hadi mwezi Aprili 2014 imekua
nakufikia shilingi bilioni 239.56.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Mfuko utaendelea na jitihada
zake za kupanua wigo wawanachama na hivyo kusajili wanachama zaidi
katikasekta zote kwa maana ya sekta rasmi na sekta isiyorasmi. Mfuko
unatarajia kusajili jumla ya wanachama23,190 na kukusanya michango yenye
thamani yashilingi bilioni 47.54. Aidha, mapato yanayotokana navitega
uchumi yanatarajiwa kuongezeka hadi kufikiashilingi bilioni 23.99.
Thamani ya Mfuko inategemeakukua hadi kufikia shilingi bilioni 310
ifikapo Juni,2015.34Mfuko wa Pensheni wa PPF
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013, Mfukowa Pensheni wa PPF
ulikusanya shilingi bilioni 278.57ikiwa ni michango ya wanachama ambayo
ni ongezekola asilimia 18 ikilinganishwa na shilingi bilioni
235.89zilizokusanywa mwaka 2012. Aidha, idadi yawanachama wanaochangia
katika Mfuko imeongezekakufikia wanachama 247,418 kutoka
wanachama203,981 mwaka 2012. Vile vile, mapato yatokanayo nauwekezaji
yaliongezeka kufikia shilingi bilioni 305.2kutoka shilingi bilioni
111.15 mwaka 2012 ikiwa niongezeko la asilimia 174.5. Kadhalika, thamani
yamfuko imeongezeka kufikia shilingi trilioni 1.49 ikiwa niongezeko la
asilimia 36.5 ikilinganishwa na thamani yamfuko ya shilingi trilioni
1.092 ilivyokuwa mwaka 2012.78. MheshimiwaSpika,ThamaniyaMfuko
inategemea kukua hadi kufikia shilingi trilioni 1.729ifikapo mwishoni
mwa mwaka 2014. Aidha, mapato yauwekezaji yanatarajiwa kufikia shilingi
bilioni 180.64.Vile vile, Mfuko unategemea kuandikisha jumla yawanachama
80,000 kutoka katika sekta ya Umma nabinafsi.Mamlaka ya Mapato Tanzania
– TRA
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2014,mapato halisi ya kodi
yalifikia shilingi bilioni 7,771.5sawa na asilimia 75 ya lengo la mwaka
la kukusanyashilingi bilioni 10,395.4. Kodi zilizochangia zaidi
ni35pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani, Kodi yaKampuni na Kodi ya
Mapato ya Ajira ambazo kwapamoja zilichangia zaidi ya asilimia 80 ya
mapato hayo.
Mheshimiwa Spika, licha ya hatua mbali mbaliambazo zimechukuliwa
katika kipindi cha mwaka2013/14, kumekuwa na changamoto katika
kufikialengo la makusanyo ya mapato. Sababu zilizochangiakutofikia
malengo ni pamoja na: mapato pungufu yaKodi ya Kampuni kuliko
ilivyotarajiwa kutoka kwenyebaadhi ya kampuni za madini; kushuka
kwamakusanyo hususan Kodi ya Zuio kutokana nakupungua kwa makusanyo
kwenye shughuli za utafitiwa gesi na mafuta. Sababu nyingine ni pamoja
nakufutwa kwa Tozo ya Kadi za Simu SIMcard levy; namakusanyo hafifu
kutoka kwenye Ushuru wa Bidhaawa Huduma za Uhawilisho wa Fedha (Money
Transfers).Kwa upande wa Forodha sababu zilizochangiakutofikiwa kwa
lengo la makusanyo ni ukuaji mdogo wauingizwaji wa bidhaa kutoka nje, na
ongezeko lakuingiza bidhaa kupitia njia zisizo rasmi (panya roads)na
bandari bubu.
Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kudhibitiukwepaji kodi, wizara
kupitia TRA inachukua hatuakadhaa za kudhibiti upotevu wa mapato kupitia
bandaribubu na panya roads, kwa kufanya upelelezi ilikuzigundua njia
hizo na kuzidhibiti kwa kutumia KikosiKazi cha Kuzuia Magendo (Flexible
Anti-SmugglingTeam). Aidha, elimu kwa wafanyabiashara na
wananchiwanaozunguka eneo la Pwani imeendelea kutolewa,ushirikiano na
vyombo vingine vya udhibiti yaani Polisi36Uhamiaji na Usalama wa Taifa
umeanzishwa; nakufanya doria katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuimarishamakusanyo ya kodi,
Mamlaka inaendelea kuimarishamatumizi ya Mashine za Kieletroniki za
kutoa Risiti(Electronic Fiscal Devices-EFDs) ambapo kwa sasainakamilisha
zoezi la kuwaingiza wafanyabiashara wotewanaostahili kuanza kutumia
mashine hizo, kuanzishaMfumo wa Uthamini wa Mizigo ya Forodha
TanzaniaCustoms Integrated System-TANCIS ambao umeanzakutumika mwezi
Aprili 2014 pamojamatumizi yamfumo wa kuthamini magari chakavu; na,
kuanzishaKitengo cha Kodi ya Kampuni za Kimataifa InternationalTax Unit
kwa lengo la kubaini na kudhibiti mianya yakupotea kwa kodi inayolipwa
na kampuni za kimataifazilizowekeza nchini.
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka yaMapato Tanzania imeanza
kutekeleza makubaliano yaJumuiya ya Afrika Mashariki ya kuweka mazingira
yakuanzishwa kwa Mfumo wa Himaya Moja ya Forodha(Single Customs
Territory – SCT) kuanzia Januari, 2014.Ili kuhakikisha kwamba mizigo ya
nchi jirani haiuzwinchini kinyume na utaratibu wa forodha, mfumo wa
ki-eletroniki wa ufuatiliaji wa mizigo inayosafirishwautatumika. Kupitia
mfumo huu, mizigo na ama vyombovya usafirishaji hufungwa lakili ya
ki-eletroniki(electronic seal) na kifaa cha mawasilaino
ambavyohuunganishwa na mfumo mkuu ili kuonesha37mwenendo mzima wa
usafiri hadi mzigo husikautakapovuka mpaka wa nchi. Aidha, mbinu
nyingine zaudhibiti saidizi kama doria, usuluhishi wa
taarifa(reconciliation) na ukaguzi zitatumika ili kuongezaudhibiti.Rufaa
za Kodi
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Bodiya Rufaa za Kodi,
imepokea jumla ya rufaa 129 namaombi 37, na imesikiliza na kutolea
maamuzi rufaa116 na maombi 28. Aidha, Bodi ipo katika hatua yakuchapisha
Ripoti ya Maamuzi yaRufaa za Kodizilizoamuliwa kuanzia mwaka 2009 –
2010. Kwa upandewa Baraza la Rufaa za Kodi, jumla ya rufaa 34 namaombi 4
yamepokelewa ambapo rufaa 41 na maombi9 yamesikilizwa na kutolewa
maamuzi. Idadi hiiinajumuisha rufaa na maombi ambayo
hayakusikilizwamwaka 2012/13.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Bodi ya Rufaa
na Baraza la Rufaa zaKodi itaendelea kupokea, kusikiliza na
kutoleamaamuzi rufaa za kodi; kutoa elimu kwa walipa kodijuu ya taratibu
za kukata rufaa za kodi; na kutoamafunzo kwa wajumbe wa Bodi na Baraza
juu yataratibu za kutatua migogoro ya kodi itokanayo nasheria za Kodi
zinazosimamiwa na Mamlaka ya MapatoTanzania. Aidha, Bodi ya Rufaa na
Baraza la Rufaa zaKodi linatarajia kuchapisha Ripoti ya Maamuzi ya
Rufaa38za Kodi zinazojumuisha maamuzi yaliyotolewa mwaka2011 hadi 2012
kwa ajili ya rejea kwa wadau wake.Huduma za KibenkiBenki Kuu ya Tanzania
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Benki Kuuimeendelea kusimamia Sekta
ya Kibenki ambapo katiya kipindi cha Machi 2013 na Machi 2014, idadi
yabenki na taasisi za fedha imeongezeka kutoka 51 namatawi 585 hadi 53
na matawi 625 kote nchini. Jumlaya mali ya sekta ya kibenki imekua
kutoka shilingitrilioni 17.9 hadi shilingi trilioni 21.1. Kiwango
chamitaji kilifikia wastani wa asilimia 18.5 ikilinganishwana kiwango
cha asilimia 10 kinachotakiwa kwa mujibuwa sheria. Aidha, Mfumo wa
Taarifa za Wakopaji CreditReference Bureau unaendelea vyema, ambapo hadi
sasakampuni mbili zimepewa leseni ambazo ni: kampuni yaCreditinfo
Tanzania Limited iliyoanza kazi Juni 2013,na kampuni ya Dun &
Bradstreet Credit Bureau (T)Limited iliyoanza kazi Septemba 2013.
Kampuninyingine kwa jina la Transunion, nayo hivi karibuniimepewa leseni
ya muda na inajiandaa kuanza kufanyakazi.
Mheshimiwa Spika, Kampuni hizi kwa sasazinaandaataarifazawatejaku
tokakwenyekumbukumbu ambazo zinahifadhiwa Benki Kuu.Taarifa hizi bado
zinafanyiwa uhakiki kabla ya kuanzakutumika rasmi.Mara baada ya data
bank hiyo39kukamilika, makampuni haya ya Credit Referenceyataanza
kufanya kazi hiyo kikamilifu na kwa usahihi.Benki Kuu inaendelea
kuyahimiza mabenki ambayobado hayajawasilisha taarifa kufanya hivyo.
Mheshimiwa Spika, Tarehe 30 Novemba 2013,Marais wa Afrika Mashariki
walitia sahihi Itifaki yaUmoja wa Fedha ya Afrika Mashariki. Tukio hili,
ndilolimeanzisha safari yetu ya kwenda kwenye hatua yakuwa na sarafu
moja ifikapo mwaka 2024. Chini yaItifaki hii, tumekubaliana vigezo
ambavyo tutatakiwatufikie kabla ya kuingia kwenye umoja huo na roadmap
ya miaka 10 ambayo itaanza kutekelezwa mara tubaada ya nchi zote
kuridhia utekelezaji wake. Katikampango huo, mambo muhimu ni;
kukamilishautekelezaji wa Umoja wa forodha na Itifaki ya soko lapamoja;
kuoanisha mifumo ya kifedh, sera zaubadilishaji wa fedha za kigeni, sera
za bajeti, namifumo ya malipo; uhuisha mifumo ya takwimu na;kuhuisha
sheria zote zinazohusiana na uanzishwaji waumoja wa kifedhaBenki ya
Maendeleo TIB – TIB Development Bank
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, TIBDevelopment Bank (zamani
Benki ya Rasilimali)iliendelea na marekebisho ya ndani ambapo shughuli
za40Benki zimegawanywa katika kampuni mbili ambazo niTIB Development
Bank Limited inayohusika na shughuliza maendeleo na TIB Corporate
Finance Limitedinayohusika na shughuli za biashara.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka ulioishiaDesemba 2013, Benki ya
Maendeleo TIB ilipata faida(kabla ya kodi) ya shilingi bilioni 11.9
ikiwa ni ongezekola asilimia 78 toka shilingi bilioni 6.7
zilizopatikanamwaka ulioishia Desemba 2012. Aidha, waraka mizaniawa
benki ulifikia shilingi bilioni 408.7 ikilinganishwa nashilingi bilioni
338.4 Desemba 2012;Mikopoiliongezeka kufikia shilingi bilioni 307.0 toka
shilingibilioni 242.9 Desemba 2012.
Mheshimiwa Spika, Dirisha la Kilimo katika Benkiya Maendeleo TIB
liliendelea kutoa mikopo kwawakopaji mbalimbali kwa riba nafuu. Tangu
kuanzakwa Dirisha mwaka 2010 hadi kufikia Aprili 2014,maombi yenye
thamani ya shilingi bilioni 58.8yaliidhinishwa. Kati ya hizo, shilingi
bilioni 33.6zilikopeshwa kwa kampuni za wakulima wadogo na wakati,
shilingi bilioni 8.7 zilienda kwa taasisi ndogo zafedha zinazokopesha
wakulima wadogo na wa kati; nashilingi bilioni 16.5 zilikopeshwa kwa
vikundi vyakuweka na kukopa (SACCOS).Benki ya Maendeleo ya Kilimo – TADB
Mheshimiwa Spika, kufuatia uamuzi wa Serikalikuanzisha Benki ya
Kilimo, Wizara imetekelezayafuatayo: kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa
Benki;41kukamilisha zoezi la upatikanaji wa Mtendaji Mkuu naWakuu wa
Idara; kuandaa Muundo wa Benki naMuundo wa Utumishi; kuandaa majukumu
yawafanyakazi; kuandaa rasimu ya Mpango wa Biashara;na kupatikana kwa
ofisi za Benki. Mwaka 2014/15,Benki ya Maendeleo ya Kilimo inatarajia
kupata leseniya biashara, kuajiri wafanyakazi na kuanza
kutoahuduma.Twiga Bancorp
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Twiga Bancorp imeendelea kutoa
huduma kwa kutumiamatawi makubwa matano na madogo matano. Hadikufikia
Aprili 2014, mikopo ya shilingi bilioni 41.9ilitolewa kwa wateja
mbalimbali. Uwekezaji kwenyeDhamana za Serikali na Amana katika Benki
zingineulikuwa shilingi bilioni 3.6 na mapato yaliyokusanywana Taasisi
yalifikia ya shilingi bilioni 3.86.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15Wizara itaendelea kuboresha
utendaji wa Taasisi kwakuimarisha uongozi. Aidha, Taasisi itaongeza wigo
wahuduma kwa kuanzisha huduma mbalimbali kama vileMax Malipo, Tigo
Pesa, M-Pesa na Airtel Money nabiashara kwa uwakala. Vile vile, Taasisi
inatarajiakufungua tawi jipya Kigamboni.Benki ya Posta – TPB
Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wabiashara na kupeleka huduma
za kibenki vijijini, Benkiya Posta kupitia ofisi za Shirika la Posta
Tanzania42imeziunganisha ofisi nane za Tunduma, Makambako,Peramiho,
Masasi, Njombe, Nachingwea, Kilwa naKahama katika mtandao wa TEHAMA na
hivyokuongeza idadi ya ofisi za Shirika la Posta ambazozinatoa huduma za
kibenki kufikia 17. Aidha, hudumakwa wateja zilitolewa kwa kutumia
mashine 185 zaATM.
Mheshimiwa Spika, amana za wateja ziliongezekakutoka shilingi bilioni
138.86 mwaka 2012 hadi kufikiashilingi bilioni 170.03 mwaka 2013 sawa
na ongezeko laasilimia 22.4. Aidha, uwekezaji katika dhamana zaSerikali
uliongezeka kutoka shilingi bilioni 39.67 hadikufikia shilingi bilioni
45.73 katika kipindi hicho sawana ongezeko la asilimia 19.8. Aidha,
thamani ya mikopoinayotolewa kwa wateja iliongezeka kutoka
shilingibilioni 100.89 hadi kufikia shilingi bilioni 119.73 ikiwani
ukuaji wa asilimia 18.7. Vile vile, faida kabla ya kodiimeongezeka
kutoka shilingi bilioni 5.67 hadi kufikiashilingi bilioni 6.99 sawa na
ongezeko la asilimia 23.4.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014, TPBinatarajia kufikia malengo
yafuatayo: kukuza rasilimaliza benki hadi kufikia shilingi bilioni
237.10; kuongezaidadi ya wateja wapya 300,000; kuongeza amana zawateja
kufikia shilingi bilioni 200.10; kuongeza mikopoya wateja kufikia
shilingi bilioni 47.16; kupata faidakabla ya kodi ya shilingi bilioni 8;
na kuendelea nataratibu za kurekebisha sheria iliyoianzisha Benki
ilikuisajili chini ya Sheria ya Kampuni.43Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo
za Kifedha
Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza kufanyamapitio ya Sera ya Taifa ya
Huduma Ndogo za Kifedha -National Microfinance Policy, 2000 ili
kuondoamapungufu ya kisheria yaliyojitokeza katika utekelezajiwake kwa
lengo la kuzingatia mabadiliko ya kiuchumina kijamii pamoja na kuweka
mazingira mazuri katikaukuaji wa sekta hiyo. Aidha, katika mwaka
2014/15,Wizara itakamilisha maandalizi ya Sera ya Taifa yaTaasisi Ndogo
za Huduma za fedha pamoja na kutungaSheria ya Taasisi ndogo za huduma za
kifedha -Microfinance Act.Huduma za BimaMamlaka ya Usimamizi wa
Shughuli za Bima – TIRA
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Mamlaka ya
Usimamizi wa Shughuli zaBima imekamilisha na kutoa Mkakati wa
KuendelezaBima ya Watu wa Kipato cha Chini – National MicroInsurance
Strategy 2014-2017. Aidha, hadi kufikia Aprili2014, kampuni 30, madalali
100 na mawakala 500 wabima walisajiliwa. Vile vile, mauzo ya bima
yaliongezekakutoka shilingi bilioni 406.7 mwaka 2012/13 hadikufikia
shilingi bilioni 481.7 sawa na ongezeko laasilimia 18.5.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,TIRA inatarajia kutekeleza
yafuatayo: kuendelea namaandalizi ya kufungua ofisi nyingine za
kanda;44kuendelea na utaratibu wa uoanishaji sheria na kanuniza soko la
bima katika eneo la Afrika Mashariki na lilela nchi za SADC; kuendelea
na tafiti za bima ya kilimo,mifugo, pamoja na bima za watu wa kipato cha
chini;na kukamilisha taratibu za kuanzisha bima ya Takaful.Shirika la
Bima la Taifa – NIC
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara ilikamilisha
urekebishaji wa Shirika la Bima laTaifa na usimikaji wa mfumo wa TEHAMA
kwa lengo lakuongeza ufanisi. Utendaji wa Shirika kibiasharauliendelea
kuimarika ambapo mapato ya bimayaliongezeka kutoka shilingi bilioni
27.38 mwaka 2012,hadi kufikia shilingi bilioni 31.53 mwaka 2013,ongezeko
hilo ni sawa na asilimia 15. Mapato hayayalitokana na makusanyo ya bima
za mtawanyo, vitegauchumi na mapato mengine.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Desemba 2013,NIC ililipa madai ya
wateja ya shilingi bilioni 8.31.Malipo hayo yalilipwa kwa wateja wa bima
za maishakiasi cha shilingi bilioni 5.71 na wateja wa bima zakawaida
kiasi cha shilingi bilioni 2.60.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15,Wizara itaendelea na mkakati wa
kuligawa Shirikakatika kampuni mbili, ambayo ni Kampuni ya Bima zaMaisha
na Kampuni ya Bima za Kawaida. Aidha,Shirika litaendelea na mkakati wa
kujitangaza zaidi na45kuongeza biashara kwa kubuni bima mpya
zinazokidhimahitaji ya wananchi.Masoko ya Mitaji na DhamanaMamlaka ya
Masoko ya Mitaji na Dhamana
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Mamlaka ya
Masoko ya Mitaji naDhamana imeendelea kusimamia Soko la Hisa la Dar
esSalaam, kampuni za udalali na ushauri wa uwekezaji,mipango ya
uwekezaji wa pamoja na kampunizilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa .
Aidha, Mamlakaimetekeleza yafuatayo: kuzindua Soko la KukuzaKampuni na
Ujasiriamali ambapo Benki ya Maendeleoiliorodhesha hisa zake; na
kuendelea na maandalizi yauanzishwaji wa soko la Hatifungani za
Manispaa.
Mheshimiwa Spika, katika kutimiza azma yaSerikali ya kuhakikisha
kampuni za Mawasiliano, Gesina Madini zinaorodhesha hisa zake kwenye
soko la Hisala Dar es Salaam, Wizara kupitia Mamlaka ya Masokoya Mitaji
na Dhamana kwa kushirikiana na wadauiliandaa taratibu zinazotakiwa
kuzingatiwa. Aidha,Mamlaka iliendelea kuelimisha umma kuhusu masokoya
mitaji na uwekezaji kwa kupitia warsha, matangazokatika vyombo vya
habari, vipeperushi na machapisho.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Mamlaka ya
Masoko ya Mitaji naDhamana imepanga kutekeleza yafuatayo:
kukamilishamaandalizi kwa ajili ya uzinduzi wa Soko la Bidhaa;kuzindua
mfumo wa uwekezaji kwa kutumia mitandao46ya simu za mikononi (M-akiba)
kwa wawekezaji wadogo;kutayarisha taratibu za kisheria na usimamizi
wabidhaa na huduma mpya zinazotarajiwa kuingizwasokonizikiwemohatifun
ganizahalmashauri;kukamilisha uandaaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa
waMaendeleo ya Masoko ya Mitaji na; kuanzisha misingiya kusimamia masoko
kwa kuzingatia uzito wa athari.Aidha, Mamlaka itaendelea kuboresha
programu yaelimu kwa umma ili kuboresha na kupanua ushiriki wawananchi
katika masoko ya mitaji.
Mheshimiwa Spika, Serikali iko katika hatua zamwisho za kupata
taasisi mbili zitakazoendesha zoezi latathmini ya kupima uwezo wa nchi
wa kukopa nakulipa madeni yake. Mwezi Februari 2014, Wizarailiziandikia
kampuni za Fitch, Moody’s InvestmentServices na Standard and poors
kuwasilisha fomu zaoza mikataba kwa hatua za uchambuzi. Tayari kampuniya
Fitch na Moody’s zimewasilisha fomu za mikatabakupitia kwa mshauri
mwelekezi Citi Group. Aidha,kuchelewa kwa zoezi hili kulitokana na
kampuni hizi zaupimaji (Rating Agencies) kutokukubaliana na aina yafomu
za mikataba zinazoandaliwa na serikali pamoja nakuleta nyongeza ya
gharama nje ya makubalianoyaliyosainiwa awali.Soko la Hisa Dar es Salaam
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Soko la Hisa Dar es Salaam
liliorodhesha Hatifunganiza Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni
690 ambazoni asilimia 83 ya makadirio ya mwaka. Kwa upande wahisa za
kampuni, Soko liliorodhesha hisa za Benki ya47Maendeleo zenye thamani ya
shilingi bilioni 4.5 na hisaza ziada na upendeleo za kampuni ya TOL
Gases Ltdzenye thamani ya shilingi bilioni 4.5. Aidha, Kampuniya Swala
Oil and Gas (T) Ltd (Australia), MwanzaCommunity Bank ya mkoani Mwanza
na UchumiSupermarket(Kenya)ziliwa silishamaombiyakuorodheshwa. Maombi
haya yako katika hatuambalimbali za kuidhinishwa.109.
MheshimiwaSpika,Thamaniyasokoi meongezeka kutoka shilingi trilioni 14.10
Julai 2013hadi shilingi trilioni 18.06 Aprili 2014, ambayo ni sawana
asilimia 28. Mafanikio haya yametokana naongezeko la bei ya hisa za
kampuni zilizoorodheshwapamoja na kuorodheshwa kwa kampuni mpya
sokoni.Aidha, idadi ya wawekezaji iliongezeka kutoka 180,458mwezi Julai
2013 hadi 192,419 mwezi Aprili 2014.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai2013 hadi Aprili 2014 hisa
zenye thamani ya shilingibilioni 245 ziliuzwa na kununuliwa. Aidha,
hatifunganiza Serikali zenye thamani yashilingi bilioni 286ziliuzwa. Kwa
ujumla mwenendo wa shughuli za Sokokatika kipindi kilichoishia Aprili
2014 ulikuwa wakuridhisha na viashiria vya mwenendo wa sokovinaonesha
mwelekeo chanya.111. MheshimiwaSpika,shughulinyingi nezilizotekelezwa na
Soko la Hisa Dar es Salaam nipamoja na: uboreshaji wa Mfumo wa Mnada
kwakuweka Mfumo Mpana – Wide Area Network48unaowawezesha madalali kuuza
na kununua hisawakiwa mahali popote nchini. Aidha, Soko la Hisa Dares
Salaam limekamilisha ukarabati wa jengo la OfisiMbadala Wakati wa
Majanga – Disaster Recovery Site najengo hilo limeanza kutumika.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Soko la Hisa Dar es Salaam
linatarajia kutekelezayafuatayo: kuendelea kuhamasisha na
kuelimishakampuniumuhimuwakuji orodheshaSokoni;kurahisisha shughuli za
minada kwa kutumia simu naintaneti; kuboresha mfumo wa kuuza na kununua
hisasokoni; na kuendelea na juhudi mbalimbali zinazolengakuongeza
ufahamu wa masuala ya masoko ya mitajikwa umma.Dhamana ya Uwekezaji
Tanzania – UTT
Mheshimiwa Spika, Dhamana ya UwekezajiTanzania imebadilisha muundo
wake na kuanzishataasisi ndogo tatu ambazo ni: Taasisi ya Miradi
naMaendeleo ya Miundombinu (UTT Project andInfrastructure Development
Plc), Taasisi ya UtoajiMikopo (UTT Microfinance Institution – UTT MFI),
naTaasisi ya Usimamizi wa Rasilimali za Uwekezaji naHuduma Kwa
Wawekezaji (UTT Asset Management andInvestor Services – UTT AMIS). Hadi
kufikia Aprili, 2014mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 4.3 imetolewa
naUTT MFI kwa wananchi 5,785, wanawake wakiwa 4,744na wanaume 1,041.49
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,UTT MFI inatarajia kuanzisha
aina mpya ya mikopo ilikukidhi mahitaji mbalimbali ya wananchi. Mikopo
hiyoni: mikopo kwa ajili ya wafanyabiashara nawakandarasi; mikopo kwa
ajili ya huduma za afya;mikopo kwa ajili ya kilimo na viwanda vidogo
vidogo;mikopo kwa wakala wa huduma za fedha; na mikopo yamatengenezo ya
nyumba.
Mheshimiwa Spika, UTT AMIS inasimamiamifuko mitano ya uwekezaji wa
pamoja ambayo niMfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko waWatoto,
Mfuko wa Jikimu na Mfuko wa Ukwasi. Katikakipindi cha Julai 2013 hadi
Aprili, 2014, thamani yamifuko hiyo iliongezeka kutoka shilingi bilioni
119.03hadi shilingi bilioni 167.37 sawa na ongezeko la asilimia40.62.
Ongezeko hili lilitokana na mauzo ya vipandepamoja na ongezeko la
thamani za rasilimali zaDhamana ya Uwekezaji. Katika mwaka 2014/15,
UTTAMIS imepanga kuanzisha mfuko wa uwekezaji wapamoja katika majumba
(Real Estate Investment Trust –REIT).Taasisi za Kitaalam na Huduma
NyinginezoOfisi ya Taifa ya Takwimu
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Ofisi ya Taifa ya Takwimu
imetekeleza yafuatayo:kutayarisha takwimu za mfumuko wa bei kila
mwezi;kutayarisha na kusambaza Takwimu za Pato la Taifakwa Robo ya
Kwanza na ya pili ya mwaka 2013;50kutayarisha Takwimu za Pato la Taifa
kwa mwaka 2013kwa bei za mwaka 2001; na kukamilisha matokeo yaawali ya
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya BinafsiNchini wa Mwaka 2012.
Aidha, Ofisi ya Taifa yaTakwimu imefanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali
zaSensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na kutoaChapisho la Kwanza la
Mgawanyo wa Watu kwa Umrina Jinsia katika Ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya,
Kata naShehia; Chapisho la Pili lenye Taarifa za Msingi zaMgawanyo wa
Watu Kiumri na Kijinsia. Vile vile,Chapisho la Tatu lenye Taarifa za
Msingi zaKidemografia, Kijamii na Kiuchumi kwa Jamhuri yaMuungano wa
Tanzania, Tanzania Bara na TanzaniaZanzibar limekamilika.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Ofisi ya Taifa ya Takwimu
itaendelea kuboreshatakwimu rasmi za kiuchumi na kijamii na
kutoamachapisho mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu naMakazi ya mwaka
2012.Aidha, Ofisi itaendeleakuboresha takwimu za Pato la Taifa kwa
kurekebishamwaka wa kizio wa bei za 2001 kwenda 2007 ikiwa nimoja ya
hatua za kuboresha takwimu za kiuchumi nakijamii ili zilingane na hali
halisi ya maendeleo yauchumi. Vile vile, Ofisi ya Taifa ya Takwimu
itaendeleakufanya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kaziwa mwaka
2014; Utafiti wa Ajira na Bei wa Mwaka2014; Sensa ya Viwanda ya Mwaka
2014; Utafiti waKilimo wa mwaka 2014/15; na kuendelea namaandalizi ya
Sheria mpya ya Takwimu.Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu51
Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2014, Bodi yaTaifa ya Wahasibu na
Wakaguzi wa Hesabu imeendeshamafunzo ya kitaaluma na kuhudhuriwa na
jumla yawashiriki 2,242. Aidha, Bodi imekamilisha silabi mpyaya mitihani
ambapo mitihani ya kwanza inatarajiwakufanyika Novemba, 2014. Vile
vile, wahitimu 228wamesajiliwakamawatunzavita bu;Wahasibuwahitimu
wanaopatiwa uzoefu wa kazi 2,631; WahasibuwaliosajiliwangaziyaCP
A1,270;Wahasibuwaliosajiliwa kama Wakaguzi wa Hesabu katika ngaziya
CPA-PP 492; Kampuni za Ukaguzi wa Hesabuzilizosajiliwa na Bodi ya Taifa
ya Wahasibu na Wakaguziwa Hesabu 170; na Kampuni za Uhasibu
zilizosajiliwana Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu19. Vile
vile, Bodi imeendelea na awamu ya pili yaujenzi wa Kituo cha Taaluma ya
Uhasibu eneo la Bunju- Dar es Salaam unaotarajiwa kukamilika
mwaka2014/15.Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi
na Ugavi imesajiliwataalamu 2,404 katika ngazi mbalimbali kwa mujibuwa
sheria. Aidha, Bodi imeendesha mafunzo yakitaaluma yaliyolenga kuboresha
uwezo wa utendajiunaozingatia maadili. Vile vile, Bodi imetahini jumla
yawanafunzi 2,455 ambapo wanafunzi 1,115 walifauluhivyo kufanya idadi ya
wahitimu kufikia 24,660. Bodi52pia imeendelea kutoa mafunzo ya vitendo
kwa wahitimukutoka vyuo vya elimu ya juu. Katika mwaka 2014/15,Bodi
inatarajia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwakuboresha mitaala yake
ili iendane na soko la ajira laUtandawazi.Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
imeendelea kutekelezamajukumu yake ya kusimamia michezo ya
kubahatishaambapo hadi kufikia Aprili 2014, jumla ya kodiiliyokusanywa
na Bodi ilifikia shilingi bilioni 10.78 sawana ongezeko la asilimia
14.4. Aidha, Bodi ilichangiashilingi milioni 532.48 katika mfuko mkuu wa
Serikalisawa na ongezeko la asilimia 0.85.Taasisi za MafunzoTaasisi ya
Uhasibu Arusha
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Taasisi ya Uhasibu Arusha
imeendelea kutoa mafunzo53katika fani za uhasibu, ugavi, benki,
Usimamizi waFedha, Usimamizi wa Rasilimali, Utawala wa
Biashara,Teknolojia ya Habari na Sayansi ya Kompyuta naMasomo ya
Kimkakati. Aidha, jumla ya wanafunzi3,341 wamedahiliwa, ambapo kati yao
wanaume ni1,847 sawa na asilimia 55 na wanawake 1,494, sawa naasilimia
45.
Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana naChuo Kikuu cha Galgotias
cha India imeanzishamafunzo ya shahada za uzamili katika sayansi
yakompyuta ambazo ni Master in Software Engineering,Master in
Information Security na Master in Computer Application. Aidha, Taasisi
inaendesha E-learningLibrary ambayo imeonesha mafanikio makubwa na
piaipo katika hatua za awali za kuanzisha E-learningCenter.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2014/15,Taasisi inakusudia kuanzisha
mafunzo katika: Shahadaya Uzamili ya Ununuzi na Ugavi, Shahada ya
MafunzoMkakati -Bachelor in Strategic Studies, Shahada yaSayansi ya
Kijeshi – Bachelor in Military Science naStashahada ya uzamili katika
mafunzo ya bima -Postgraduate Diploma in Insurance.Chuo cha Usimamizi wa
Fedha54
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo cha Usimamizi wa Fedha
kilidahili jumla yawanafunzi 9,998 katika fani mbalimbali. Kati ya
haowanawake 3,532 sawa na asilimia 35 na wanaume6,466 sawa na asilimia
65. Aidha, Chuo kimeanzishaShahada za Uzamili katika fani za Uhasibu na
Fedha,Fedha na Uwekezaji na Rasilimali Watu. Vile vile, Chuokimeanzisha
tawi katika Jiji la Mwanza ambapomasomo kwa wanafunzi wa ngazi ya Cheti
naStashahada katika fani ya Uhasibu na Benki yalianzakutolewa mwaka
2013.Taasisi ya Uhasibu Tanzania
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Taasisi ya Uhasibu Tanzania
ilidahili jumla yawanafunzi 9,769 kati ya hao wanawake 4,776 sawa
naasilimia 49 na wanaume 4,993 sawa na asilimia 51Aidha, Taasisi
ilianzisha kozi mbili mpya ambazo niUhasibu katika Sekta ya Umma -Public
SectorAccounting na Masoko na Uhusiano wa Umma -Markerting and Public
Relations katika ngazi za Cheti,Stashahada na Shahada. Vile vile,
Taasisi imeanzaujenzi wa jengo la mihadhara katika Kampasi yaMtwara
lenye uwezo wa kuchukua wanachuo 500.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Taasisi inatarajia kudahili
wanafunzi 9,729, kufunguatawi jipya katika mji wa Kigoma na kuendelea na
ujenziwa jengo katika Kampasi ya Mtwara.55Chuo cha Mipango na Maendeleo
Vijijini
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo kimedahili jumla ya
wanafunzi 5,052 kati yaowanawake 2,360 sawa na asilimia 47 na
wanaume2,692 sawa na asilimia 53. Aidha, wanafunzi 1,846walihitimu
masomo katika kozi mbalimbali ambapo katiya hao wanaume ni 1,037 sawa na
asilimia 56 nawanawake walikuwa 809 sawa na asilimia 44. Vile vile,Chuo
kimekamilisha ujenzi wa jengo la pili la taaluma.Kadhalika Chuo
kimetayarisha taarifa za Hali yaUchumi na Kijamii za Wilaya (District
Socio-EconomicProfiles) za Halmashauri za Bunda, Ulanga, Kahama,Geita na
Manispaa ya Dodoma.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Chuo kitatoa mafunzo ya muda
mfupi ya kujenga uwezokwa watendaji namna ya kupanga, kutekeleza
nakusimamia mipango ya maendeleo kwenye sehemu zaoza kazi.Chuo cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo kilidahili wanafunzi 269
kati ya hao wanawake108 sawa na asilimia 40 na wanaume 161 sawa
naasilimia 60. Aidha, Chuo kimeanzisha Shahada yaUzamili katika Takwimu
Rasmi na tayari chuo56kimedahili wanafunzi 32 kutoka nchi za
Ethiopia,Ghana, Nigeria, Swaziland na Tanzania.CHANGAMOTO
Mheshimiwa Spika,katikakutekelezamajukumu yake, Wizara ilikabiliwa na
changamotozifuatazo:i. Kuongeza mapato ya ndani ya Serikali ili
kukidhimahitaji yamatumizi ya maendeleo na yakawaida;ii. Mabadiliko ya
hali ya uchumi na uongozi katikanchi za washirika wa maendeleo
ambapozimepelekea kushindwa kutimizwa kwa baadhi yamiadi;iii. Uwezo wa
kusimamia mikataba katika kutekelezabaadhi ya miradi na programu za
maendeleo; naiv. Upatikanaji wa mikopo ya kibiashara kwa
wakatikunakotokana na kubadilika kwa mashartikutoka kwa wakopeshaji.
Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachangamoto hizo, Wizara
imeendelea kuchukua hatuambalimbali ikiwa ni pamoja na:i. Kubuni vyanzo
vipya vya mapato na kudhibitimatumizi pamoja na kupunguza upotevu
wamapato;ii. Kuboreshaushirikianonawashirik awamaendeleo yenye lengo la
kuwa na uelewa sawakuhusu masuala mbali mbali katika
ushirikianowetu;iii. Kuendelea kuzijengea uwezo Wizara, Taasisi
naMamlaka za Serikali za Mitaa katika kusimamia57iv.v.na kutekeleza
mikataba ya miradi na programu zamaendeleo;Kuendelea kutekeleza Programu
ya Maboresho yaUsimamizi wa Fedha za Umma – “Public FinancialManagement
Reform Programme (PFMRP)”; naKushauri Wizara, Mikoa na Mamlaka za
Serikaliza Mitaa kuzingatia vipaumbele wakati wakupanga na utekelezaji
kulingana na bajetiiliyotengwa.Kuanza mazungumzo mapema na wakopeshaji
wamikopo ya kibiashara.Mapitio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu yaWizara
kwa Mwaka 2013/14
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,majukumu ya Wizara
yalitekelezwa katika mafungusaba ya kibajeti. Mafungu hayo ni Fungu 50 –
Wizara yaFedha; Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali;Fungu 22 –
Deni la Taifa; Fungu 21 – HAZINA; Fungu13 – Kitengo cha Udhibiti wa
Fedha Haramu; Fungu 10– Tume ya Pamoja ya Fedha; na Fungu 7 – Ofisi
yaMsajili wa Hazina. Aidha, Fungu 45 – Ofisi ya Taifa yaUkaguzi ambayo
inajitegemea linaombewa fedhaBungeni na Waziri wa Fedha kwa mujibu wa
Sheria.Fungu 50 – Wizara ya Fedha
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Fungu 50ilitarajia kupata shilingi
bilioni 126.48 kutoka vyanzombalimbali vya mapato yasiyo ya kodi ambavyo
nimauzo ya mali, uuzaji wa nyaraka za zabuni na mapato58kutoka katika
Mashirika ya Umma na Taasisi zaSerikali (Gawio, Michango na Marejesho ya
mikopo).Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, makusanyo yalifikiashilingi
bilioni 66.79 sawa na asilimia 52.81 ya lengo.Kiwango hicho kinatarajiwa
kuongezeka katika robo yanne ya mwaka wa fedha baada ya Mashirika
mengikuandaa hesabu za mwaka na ukaguzi wa hesabu hizokukamilishwa.
Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 50 kwa mwaka 2013/14
yalikuwashilingibilioni 54.71 kwa ajili ya matumizi ya kawaida
nashilingi bilioni 233.67 kwa ajili ya matumizi yamaendeleo. Hadi
kufikia mwezi Aprili, 2014, matumiziya kawaida yalifikia shilingi
bilioni 36.60 sawa naasilimia 66.89 ya makadirio na matumizi ya
maendeleoyalifikia shilingi bilioni 219.97 sawa na asilimia 94.14ya
makadirio.Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali
Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 23 kwa mwaka 2013/14
yalikuwashilingibilioni 80.83 kwa ajili ya matumizi ya kawaida
nashilingi bilioni 4.76 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.Hadi kufikia
mwezi Aprili, 2013, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 45.63
sawa na asilimia 56.45 yamakadirio na matumizi ya maendeleo yalifikia
shilingibilioni 1.22.59Fungu 22 – Deni la TaifaMheshimiwa Spika,
makadirio ya matumizi ya Fungu22 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi
bilioni3,319.01. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014 matumizi yafungu hili
yalifikia shilingi bilioni 2,795. 43 sawa naasilimia 84.22 ya
makadirio.Fungu 21- HAZINA
Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yakawaida ya Fungu 21 kwa
mwaka 2013/14 yalikuwashilingi bilioni 1,367.29 na matumizi ya
maendeleoshilingi bilioni 38.15 . Hadi kufikia mwezi Aprili,
2014,matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 420.28sawa na
asilimia 30.74 ya makadirio, na matumizi yamaendeleo yalifikia shilingi
bilioni 19.78 sawa naasilimia 51.85 ya makadirio.Fungu 13
–KitengoHaramuchaUdhibiti waFed ha
Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 13 kwa mwaka 2013/14
yalikuwashilingibilioni 1.94 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
shilingibilioni 0.39 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia
mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 0.91
sawa na asilimia 46.90 yamakadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia
shilingibilioni 0.07 sawa na asilimia 17.95 ya makadirio.60Fungu 10 –
Tume ya Pamoja ya Fedha
Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yakawaida kwa Fungu hili
yalikuwa shillingi bilioni 2.06,hadi kufikia Aprili, 2014 matumizi
yalifikia shilingibilioni 1.04 sawa na asilimia 49.76 ya makadirio.Fungu
7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina
Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 7 kwa mwaka 2013/14
yalikuwa shilingi bilioni38.08 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
shilingibilioni 1.66 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia
mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 33.06
sawa na asilimia 86.8 yamakadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia
shilingibilioni 0.62 sawa na asilimia 37.35 ya makadirio.Fungu 45 –
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 45 kwa mwaka 2013/14
yalikuwashilingibilioni 57.4 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
shilingibilioni 21.45 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia
mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 43.11
sawa na asilimia 75.1 yamakadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia
shilingibilioni 2.97 sawa na asilimia 13.84 ya makadirio.61MAKADIRIO YA
MAPATO NA MATUMIZI KWAMWAKA WA FEDHA 2014/15MapatoMheshimiwa Spika,
katika mwaka 2014/15, Wizaraya Fedha Fungu 50 inakadiria kukusanya
mapatoyasiyo ya kodi yapatayo shilingi126,188,104,000(bilion i
126.19Maombi ya FedhaFungu 50 – Wizara ya Fedha.
Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama
ifuatavyoa)(b)Matumizi ya kawaida Shilingi 66,239,790,000(bilioni
66.23). Kati ya hizo mishahara ni shilingishilingi5,620,668,000(
bilioni5.62)namatumizi mengineyo shilingi 60,619,122,000(bilioni
60.61).Miradi ya Maendeleo Shilingi 29,803,232,000(bilioni 29.71).Kati
ya hizoi) Fedha za Ndani – Shilingi 19,350,000,000(bilioni 19.35).(ii)
Fedha za Nje – Shilingi 10,453,232,000(bilioni 10.45).Fungu 23 – Idara
ya Mhasibu Mkuu wa Serikali:62
Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama
ifuatavyoa)Matumizi ya kawaida – Shilingi 82,170,024,000(bilioni 82.17).
Kati ya hizo mishahara shilingi5,012,762,000(bilioni 5.01) na
matumizimengineyo shilingi 77,157,262,000 (bilioni77.16).(b)Miradi ya
Maendeleo – Shilingi 7,950,000,000(bilioni 7.95) Kati ya hizoi) Fedha za
Ndani -Shilingi 4,800,000,000(bilioni 4.80).(ii) Fedha za Nje-Shilingi
3,150,000,000(bilioni 3.15).Fungu 22- Deni la Taifa
Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha Shilingi
4,354,865,076,000(bilioni 4,354.86). Kati ya hizo mishahara ni
shilingi10,341,136,000 (bilioni 10.34), Deni la Taifa
shilingi3,650,612,000,000 (bilioni 3,650.61) na matumizimengineyo ni
shilingi 693,911,940,000 (bilioni693.91).Fungu 21 – HAZINA
Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama
ifuatavyo:63(a)(b)Matumizi ya kawaida Shilingi 790,325,216,000(bilioni
790.32). Kati ya hizo mishahara nishilingi4,015,511,000(bilion
i4.01)namatumizi mengineyo shilingi 786,309,705,000(bilioni 786.31)
ambazo ni kwa ajili ya matumiziya Idara na Taasisi zilizo chini ya Fungu
hili,nyongeza ya mishahara ya Watumishi wa Serikalina matumizi
maalum.Miradi ya maendeleo ni shilingi 57,417,015,000(bilioni 57.42).
Kati ya hizo;(i)Fedha za Ndani- Shilingi 17,000,000,000(bilioni
17.0)(ii)Fedha za Nje- Shilingi 40,417,015,000(bilioni 40.42)Fungu 13
–Kitengo Haramu: cha Udhibiti wa Fedha
Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama
ifuatavyoa) Matumizi ya kawaida – Shilingi 2,000,000,000(bilioni
2.0).(b) Miradi ya Maendeleo, fedha za nje Shilingi195,000,000 (bilioni
0.19).Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha:
Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha Shilingi
2,318,661,000 (bilioni642.32) kwa matumizi ya kawaida. Kati ya fedha
hizo,shilingi 318,661,000 (bilioni 0.32) ni kwa ajili yamishahara na
shilingi 2,000,000,000 (bilioni2.0) nimatumizi mengineyo.Fungu 7 – Ofisi
ya Msajili wa Hazina:
Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama
ifuatavyoa)Matumizi ya kawaida – Shilingi 88,455,278,000(bilioni88.45).K
atiyahizoshilingi670,328,000 (bilioni 0.67) ni kwa ajili yamishahara na
shilingi 87,784,950,000 (bilioni87.78) ni matumizi mengineyo.(b)Miradi
ya Maendeleo – Shilingi 1,943,000,000(bilioni 1.94)Kati ya hizoi)Fedha
za Ndani –Shilingi 650,000,000(bilioni 0.65).(ii)Fedha za Nje-Shilingi
1,293,000,000(bilioni 1.29).Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
Mheshimiwa Spika, katika fungu hili
kwamwakawafedha2013/14,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama
ifuatavyoa) Matumizi ya kawaida shilingi 69,843,825,000(bilioni 69.84).
Kati ya hizo mishahara ni shilingi6510,408,402,000 (bilioni 10.41) na
matumizimengineyoshilingi59,43 5,423,000(bilioni59.43).(b) Miradi ya
maendeleo shilingi 13,011,432,000(bilioni 13.01), kati ya hizoi)Fedha za
ndani shilingi 8,000,000,000(bilioni 8.0).(ii) Fedha za nje shilingi
5,011,432,000 (bilioni5.01).
HITIMISHO
Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zadhati kwa Wakuu wa Idara
na Vitengo, Wafanyakazi waWizara ya Fedha wakiongozwa na Katibu Mkuu
Dkt.Servacius B. Likwelile na Naibu Makatibu WakuuNdugu Elizabeth J.
Nyambibo, Prof. Adolf F. Mkenda naNdugu Doroth S. Mwanyika kwa kazi
kubwawanayoifanya katika kutekeleza majukumu ya Wizara.Vile vile,
napenda kuwashukuru Wakuu wa Taasisi naWakala wa Serikali chini ya
Wizara kwa michango yaokatika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.
Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.
Hotuba hii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara(www.mof.go.tz)
- Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.