BRAZIL YAIBANA CROATIA 3 - 1
Neymar akishangilia bao lake la kwanza. Neymar akifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti. Wenyeji wa kombe la dunia Brazil ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/brazil-yaibana-croatia-3-1.html
Neymar akishangilia bao lake la kwanza.
Neymar akifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti.
Wenyeji wa kombe la dunia Brazil walitoka nyuma na
kuilaza Croatia mabao 3-1 katika mechi ya kufungua fainali ya dimba la
mwaka huu iliyochezwa katika uwanja wa Sao Paolo (Arena de Sao Paulo).
Mechi hiyo ilikuwa ikitizamwa na mashabiki
65,000 uwanjani humo baada ya kushuhudia tafrija ya ufunguzi
iliyotizamwa na watazamaji zaidi ya bilioni moja kupitia kwa runinga
Wenyeji Brazil walitazamiwa kufunga
bao la kwanza mapema katika mechi hiyo lakini uwanjani mambo yalikuwa
tofauti ,Marcelo alijifunga mwenyewe na kuiweka Croatia mbele baada ya
dakika 11 pekee ya kipindi cha kwanza .
Wenyeji waliotamaushwa na bao hilo walikuwa na
matumaini kuwa kiungo machachari anayechezea Barcelona ya Uhispania
Neymar atawaongoza ''the samba boys'' kutwaa taji lao la sita la dunia
nyumbani.
Na nyota huyo hakuboronga alitumia kila mbinu
ikiwemo kumbo iliyompelekea kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya
njano na refarii kutoka Japan Yuichi Nishimura.
Hata hivyo dakika chache tu baada ya kuonyeshwa
kadi hiyo ya njano Neyma alijifurukuta na kuisawazishia Brazil katika
dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 22
aliiweka Brazil Mbele zikiwa zimesalia dakika 19 mechi hiyo kukamilika
baada ya refarii kutoka Japan Nishimura kupiga kipenga na kuashiria penalti baada ya Dejan Lovren kuonekana kama aliyemtega Fred katika eneo la lango.
Hata hivyo picha za runinga zilizorejelea mara kadhaa hazikuonesha kama Lovren alimgusa Fred. Wachezaji wa Croatia walijaribu kumshawishi mjapan huyo kuwa haikuwa kweli fred alikuwa amejiangusha lakini maoni yao hayakusikika. Neymar kwa mara ya kwanza katika mechi hiyo aliiweka Brazil mbele kufuatia mkwaju huo wa penalti.
Vijana wa Luiz Scolari hawakuwachia hapo
waliendelea kushambulia lango la Croatia na juhudi zao zilizaa matunda
katika kipindi cha ziada Oscar alipompata kipa wa croatia ameduwaa na
kufutamatisha kichapo hicho kunako dakika ya 91 .
Kufuatia ushindi huo wenyeji hao sasa wamejikita katika nafasi ya kwanza katika kundi A wakiwa na alama tatu. Cameroon na Mexico zinashikilia nafasi ya pili na tatu katika kundi hilo .
Timu hizo zitakabiliana hapo Kesho.