Mtoto Fatuma Hassan (9) anyedaiwa kufungiwa ndani kwa siku tatu kisha kuchomwa moto mikononi na mama yake mkubwa aliyetajwa kwa jina m...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/mtoto-achomwa-moto-kisa-sh-500.html
Mtoto
Fatuma Hassan (9) anyedaiwa kufungiwa ndani kwa siku tatu kisha
kuchomwa moto mikononi na mama yake mkubwa aliyetajwa kwa jina moja la
Diana (38), mkazi wa maeneo ya Tandale.
Mama mkubwa wa mtoto Fatuma Hassan anyetuhumiwa kumtesa mtoto huyo.
Stori: Chande Abdallah na Denis Mtima
UNYAMA ulioje?
Mtoto Fatuma Hassan (9) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hekima
iliyopo Tandale, Dar anadaiwa kufungiwa ndani kwa siku tatu kisha
kuchomwa moto na mama yake mkubwa aliyetajwa kwa jina moja la Diana
(38), mkazi wa maeneo hayo, kisa kikielezwa kuwa ni shilingi mia tano.
Tukio hilo lilitokea Juni 10, mwaka huu katika maeneo hayo ya Tandale
Sokoni ambapo mama huyo alikuwa akiishi na mtoto wa mdogo wake kwa kile
kilichodaiwa kuwa alimchukua kwa ahadi ya kumsomesha lakini kuna madai
kuwa badala ya kufanya hivyo, alimnyanyasa.
Taarifa zilidai kwamba mama huyo aliamua kumfanyia ukatili mtoto huyo
akidai kuwa alichukua fedha hizo akiwa na mwanaye wa kumzaa kwa ajili ya
kwenda kutumia kununulia sambusa na juisi shuleni.
Ilisemekana
kwamba kitendo hicho kilimkera mama huyo na kuamua kuwasubiri warudi ili
awaulize kama kweli walichukua fedha hizo ambapo walikiri kuzitumia
shuleni.
Wakizungumza na wanahabari wetu, majirani wa eneo hilo walisema kuwa
walimuona mtoto Fatuma akipigwa na mama’ke huyo mkubwa fimbo na kumchoma
moto mikononi pasipo kumpeleka hospitali huku akimpa onyo kali na
kumfungia ndani.
Walisema kuwa mwanamke huyo amekuwa akimfungia ndani na kwenda kwenye genge lake.
Mjumbe wa eneo hilo, Said Sundi na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Pakacha, Ally Mdee wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Wananchi walifikia hatua ya kufananisha tukio hilo na lile la mtoto
aliyefungiwa kwenye boksi mkoani Morogoro, Nasra Mvungi (marehemu),
walimkamata na kupiga simu katika Kituo cha Polisi cha Magomeni ambapo
askari walifika na kumchukua mwanamke huyo.
Pia walimpeleka mtoto Fatma kwenye Hospitali ya Magomeni anakopatiwa
matibabu huku mwanamke huyo akishikiliwa na polisi kwa ajili ya
mahojiano na alifunguliwa kesi ya kujeruhi yenye jalada namba
MAG/RB/5676/2014.