TBL KUWAJENGEA KISIMA CHA MAJI CHA SH MIL. 29 WANANCHI WA SARANGA, DAR
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris M...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/tbl-kuwajengea-kisima-cha-maji-cha-sh.html
Ofisa Uhusiano wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi mfano wa hundi yenye
thamani ya sh. mil 29 za msaada wa ujenzi wa kisima cha maji katika
mtaa huo uliopo Kata ya Saranga, Kinondoni Dar es Salaam. Hafla hiyo
ilifanyika katika mtaa huo mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia makabidhiano
hayo ni Mkandarasi wa kisima hicho, Onesmo Sigala (wa pili kulia) wa
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MO Resources Limited,na Mjumbe wa
Kamati ya Maji ya Mtaa wa King'ongo, Anna Kibwana ( wa pili kushoto).
Ofisa Uhusiano wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu akimkabidhi Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya ukandarasi ya MO Resources Limited, Onesmo Sigala
(kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 29 za msaada wa ujenzi
wa kisima cha maji katika mtaa huo uliopo Kata ya Saranga, Kinondoni
Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika katika mtaa huo mwishoni mwa
wiki.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Mjumbe wa Kamati ya Maji ya Mtaa
wa King'ongo, Anna Kibwana (wa pili kushoto),Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa wa King'ongo, Benetris Mapesi.