TAARIFA ZA UVUMI WA KIFO CHA WAZIRI WA ELIMU SHUKURU KAWAMBA ZAKANUSHWA, SOMA HAPA
Taarifa hii imetoka kwenye akaunti ya facebook ya Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na inasomeka kama ifuatavyo…. Ndg Watanzania...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/06/taarifa-za-uvumi-wa-kifo-cha-waziri-wa.html
Taarifa hii imetoka kwenye akaunti ya facebook ya Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na inasomeka kama ifuatavyo….Ndg
Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo
na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko
yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne
Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa
Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani
anaelekea Mwanza.
UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.

Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze
Mbunge -Chalinze