WAMBURA RUKSA KUGOMBEA URAIS SIMBA

  Mgombea wa nafasi ya urais klabuni hapo, Michael Wambura RASMI Kamati ya rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemrej...

 Mgombea wa nafasi ya urais klabuni hapo, Michael Wambura



RASMI Kamati ya rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemrejesha Mgombea wa Urais wa Simba SC, Michael Richard Wambura kwenye mbio za kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya amewaambia Waandishi wa Habari mchana wa leo (jana) ofisi za TFF katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kwamba Wambura amerejeshwa baada ya kikao chao kilichodumu kwa siku mbili.

Baada ya mlolongo mrefu tangu juzi Saa 5:00 asubuhi hoteli ya Courtyad, Upanga, Dar es Salaam hadi jioni ya jana (juzi), Wajumbe wa Kamati hiyo waliamua kupiga kura kuamua na Wambura akapata kura tatu kati ya tano za kumkubalia aendelee na mbio za Urais Simba SC.
Ikumbukwe Wambura alikata rufaa TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumuengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC chini ya Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro ilimuengua Wambura kwa sababu alikiuka Katiba ya klabu hiyo, TFF na FIFA kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani.

Related

KINANA NA MSAFARA WAKE WATINGA WILAYANI MOMBA LEO ASUBUHI

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisalimiana na viongozi wa wilaya ya Momba mkoani Mbeya, katika mpaka wa wilaya hiyo na Ileje leo saa 5 as...

SOMA ALICHOWEKA ZITTO KABWE LEO KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK...PATA STORY

Why I think my party’s (#CHADEMA) decision is wrong! 27/11/2013Uncategorized Disclaimer: This entry is objective. It is written after much reflections and thoughts. It is an expression of m...

ZANZIBAR INA MWELEKEO MZURI WA KUIMARISHA AFYA

Na Khamis Haji, OMKR Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema mafanikio yaliyoweza kupatikana katika sekta ya afya miaka ya hivi karibuni ni ishara kuwa Z...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904765
item